Kumbe kuna wakati Sabodo alibeba dhamana ya Nchi kwenye uhaba wa Mafuta (nadhani ni diesel na Petroli) , cha kushangaza anasubiriwa Mbowe ndio ayaseme haya ! hivi viongozi wanaoficha historia hii hawaijui au hawataki ?
Iko haja ya viongozi wapya wachanga wa nchi hii kufundishwa kwanza walioifikisha hii nchi hapa ilipo badala ya kupewa vyeo kwa mtindo wa Koneksheni na Uchawa .
Uhakika ni kwamba over 90% ya viongozi wa nchi hii wakiwemo mawaziri na viongozi wa ccm hawajui Uzalendo wa Sabodo na ni Aibu kwao na Aliyewateua , Unateuaje watu wasioijua Nchi yao ?
Anyway Sabodo alikuwa mjanja wa mjini.
Hayo mafuta Toka Iran tuliyapata ila kwa mkopo .Iran Haikutoa bure.Ilitaka lazima ilipwe pesa zake.Tukashindwa kulipa deni lao cash wala haukuwa na riba .Ila nchi ikawa choka mbaya.Ieleweke Sabodo huo mkopo haukuketwa bure na yeye hakufanya hiyo kazi bure.Ni agent dalai mjanja fulani hivi .Na kila dalai huwa na chake.Niishie hapo Mafuta tukapata toka Irani lakini sio bure.Walitukopesha.Tukashindwa kulipa hali ngumu pesa za kigeni hamna.Hawakuwa na shida kudai hilo deni kipindi cha Raisi Mwinyi muislamu mwnzao akiongea kitu walikubali kwa shingo upande ila pesa zao walitaka
Kipindi raisi Mkapa Mkristo kashika Iran wakachachamaa wanataka pesa zao sababu waliogopa Mkristo aweza kataa deni wakiamini muislamu ndio mwaminifu kulipa deni
Mkapa akaona aoengee na waislamu wanazuoni wazalendo wa uhakika waaminiwa na serikali na umma waliotulia kiimani na wenye hekima kubwa Wazee wa hekima wanaojali nchi yao Tanzania kuwa jua liwake mvua inyeshe wako na Tanzania
ukatumwa ujumbe mzito wa waislamu nchi hii wazalendo kwenda Iran sitaki kuwataja toka misikitini ,serikalini nk wakaomba hilo deni la Iran lilipwe sio kwa fedha taslimu za dola wakaomba lilipwe kwa fedha za Tanzania au chochote kinacholingana na hizo pesa za den la Irani ila badala ya kwenda Iran ziende kwa waislamu wa Tanzania kutatua changamoto zao
.Iran iliposikia kuwa zitaenda kwa waislamu kutatua changamoto zao ikakubali na kiatoa msamaha mkubwa tu wa deni.Zilizobaki wakasema wakaulizwa mnataka ziende hawana chuo kikuu cha kiislamu wala hawana uwezo wa kujenga Mkapa akakubali mahesabu yakapigwa waislamu wakapewa chuo kikuu cha Morogoro kilichokuwa chuo cha Tanesco pale Morogoro na serikali ikamalizana na lile deni na Irani .Serikali ikawapa waislamu kwa faida yao kama ilivyokubalika
Kuna kesi nyingi za nchi kudaiwa na kurudisha mali zilizotaifishwa za makanisa nk kulipia madeni nchi ilishindwa kulipa viongozi wa makanisa wanatumwa nchi zao dini za Kikristo na viongozi wakiristo serikalini nk wanatumwa kujadili na nchi kupata ufumbuzi unapatikana kupitia viongozi wa dini tu
Mbowe na upinzani Tanzania bado watoto sana wanaendekeza individual politics nchi kama nchi ina deal.na mambo mazito far above individuals na sifa za kibinafsi za majukwaani au mitandaoni za ohh sijui huyu alifanya hivi kuna mengine hayawekwi wazi other side
Usione viongozi wa dini wanakaa vitu vya mbele raisi akiwepo au shughuli ya kitaifa ikiwepo they deserve
Utawaona wamekaa kama wajinga fulani hivi .Wanaelewa mambo mengine mazito solutions zake kuliko wanasiasa au viongozi wa serikali wanaotembea na misafara