Hotuba ya Lukuvi bungeni kuthibitisha kauli yake kanisani, UKAWA kumchukulia hatua za kisheria

Hotuba ya Lukuvi bungeni kuthibitisha kauli yake kanisani, UKAWA kumchukulia hatua za kisheria

Mm ni muumini wa serikali mbili lakini Mh Lukuvi hapo ameteleza.

siku zote huyo uwa ni mtu wa kauli za ajabu!!!mwingine ni wasira na mwigulu!!!mtu akipenda chongo uita kengeza,ulikuwa kwenye giza,binafsi Mimi sitaki serikali 2,moja ndiyo itapunguza gharama na kuleta mshikamano halisi,changamoto ni nani wa kumvika paka kengere!!kilichobaki ni kuzunguka na tatizo tunaliacha palepale!!
 
Sasa ndio nimeamni kua Lukuvi ni mgonjwa na tena awahi huko India akapate matibabu upesi!
 
kwanini watanzania tunavumilia ujinga kama huu kwanini pesa ya umma itumike kutoa rushwa mchana kwaeupe tena bungeni? je hii inatufundisha nini? kwamba kujipendekeza kwa serikali na dola ni neema hii ni aibu kwa watanzania sijui tumerogwa na nani?
 
Hiyo ndiyo CCM wazee wa Rushwa na TAKRIMA, si unamuona mzee alivyochoka? Kwa nini asimsifie mpiga zomari anaye mchagulia wimbo wa kucheza. Nguvu ya CCM sasa imebaki kwenye matumizi mabaya ya kodi za wananchi na matumizi ya hovyo ya raslimali za wananchi. Nguvu ya ccm sasa imebaki kutumia vibaya vyombo vya dola UWT, JWTZ, polisi nk. Tayari CCM wanajua washapoteza nguvu ya ushawishi kwa wananchi ndiyo sababu wanalazimika kumwaga mipesa halali na haramu kwenye chaguzi zote ili kujiaminisha kwamba bado wanakubalika....
 
Tujieshimu nchi yetu inayumba CCM sasa ni chama cha WAHAFIDHINA lakini na nyinyi UKAWA jamani angalia nchi maskini kama hii nawaomba wote muwe na adabu mshikamano umoja uhuru na amani ndo sifa yetu jamani huko siko ZITTO upo washauri wenzako UKAWA wapunguze kidogo mwendo huu ni hatari pia MIHAFIDHINA CCM muache ushenzi na upuuzi sisi tunaona mnavyo lazimisha kutengeneza katiba yenu naonya tutaivunja nchi hii vipande
 
Tatizo la lukuvi anaongea kwa hisia zake bila ya udibitisho wa kitu anachokisema pia bila kuangalia madhara ya anachokizungumza
 
Wenyewe wanaiita takrima...

Ila hii serikali yetu ni mzigo kweli, ina maana walikuwa hawaoni ulazima wa kumpa stahiki zake Mzee Mrema kwa muda wote huu.

Na kauli ya Lukuvi inatufungua macho na kutueleza kuwa ukiwa unaipamba serikali basi utaishi kama mfalme.
 
Hiyo ndiyo CCM wazee wa Rushwa na TAKRIMA, si unamuona mzee alivyochoka? Kwa nini asimsifie mpiga zomari anaye mchagulia wimbo wa kucheza. Nguvu ya CCM sasa imebaki kwenye matumizi mabaya ya kodi za wananchi na matumizi ya hovyo ya raslimali za wananchi. Nguvu ya ccm sasa imebaki kutumia vibaya vyombo vya dola UWT, JWTZ, polisi nk. Tayari CCM wanajua washapoteza nguvu ya ushawishi kwa wananchi ndiyo sababu wanalazimika kumwaga mipesa halali na haramu kwenye chaguzi zote ili kujiaminisha kwamba bado wanakubalika....

kinachonishangaza ni kwanini Watanzania hatuchukizwi na vitendo hivi vya kijinga ni kwanini tunaruhusu bunge letu litumike kugawa rushwa hivi hii nchi inakwenda wapi?
kwanini watu wanaona kitendo kibaya kama hiki kwamba ni jambo la kawaida tu?!!!!
 
kwanini watanzania tunavumilia ujinga kama huu kwanini pesa ya umma itumike kutoa rushwa mchana kwaeupe tena bungeni? je hii inatufundisha nini? kwamba kujipendekeza kwa serikali na dola ni neema hii ni aibu kwa watanzania sijui tumerogwa na nani?

Wanasema adui yako akiwa anafanya makosa yatayokupa ushindi usimstue!!!!!
 
Rushwa. Period. Alirasimisha rushwa. Si kwa kauli ya kuhusu hicho kinachoitwa mafao ya Mrema pekee (ambacho hakipo by the way kwa sababu hicho cheo hakijawahi kuwepo), bali pia hata aliposema kuwa eti maagizo aliyotumwa na Samuel Sitta kuhusu mafao ya wajumbe ameyafanyia kazi na suala linakwenda vizuri, ilikuwa ni sehemu ya kurasimisha rushwa. Rotten system tu inaweza kuruhusu mambo ya namna hiyo.
 
mrema yupokima slai zaidi hayupo kwaajili ya watanganyika,sifia sifia ndio sera zake ili alipwe mafao yake,m2wa ndimi2.
 
Lukuvi pia aliituhumu Ukawa kwamba imepanga kuigawa Tanzania katika vipande, kwamba Zanzibar itatawaliwa na CUF, Tanzania Bara na Chadema halafu CCM ipewe urais wa Muungano.

Wasiwasi wote wa CCM upo katika matamshi haya, wanahofia mfumo ukibadilishwa tu basi hata misingi ya ufalme wao itakuwa matatani.
 
hata mimi njlishangaa pale aliposema kwamba,atalipwa kwa yale aliyoyasema,alafu kama ni suala la kumuita lukuvi kujitetea mbona wasimuie au kuwaita tume ya katiba kutetea walichoandika?
 
Wananchi tusikubali kuweka madarakani viongozi wasioelewa kwanini wako madarakan. Hapa lukuvi anamaana yeye anawajibika kwa watu wanaotetea masilahi yake tu. Kama nchi ndo inaviongozi wa aina hii rushwa haitaisha mbali itazidi kuongezeka
 
Back
Top Bottom