Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jana nilipokua nafuatilia bunge mwenyekiti wa bunge alimpa nafasi waziri wa nchi sera uratibu na bunge ndg Lukuvi nafasi ya alichokiita kujibu alichosema prof Limbumpa baada ya hicho alichokiita majibu kwa Lipumba, mh Lukuvi alimsifia sana Mrema kwa mchango wake uliomfurahisha bila shaka na kuwafurahisha wakubwa wa ccm mpaka akafikia kumuahidi kwamba atahakikisha Mrema anapata mafao yake ,maswali ya kujiuliza
1. je ni haki ya Mrema kupata hicho Lukuvi anachookiita mafao au ni rushwa baada ya kuwafurahisha kwa mchango wake bungeni
2.kama ni haki yake inahitaji kujipendekeza kwao ndio upate haki yako?
3. hii inatufundisha nini kwamba mpaka tujipendekeze kwa ccm ndio tunaweza kupata haki yetu?
4. kwanini Watanzania tunaruhusu mambo ya kijinga haya yatokee katika nchi yetu kwanini tunaruhusu waziri atumie ofisi ya umma na rasilimali za umma kwa manufaa ya chama chao na serikali iliyoko madarakani
5.ni wangapi wataanza kujipendekeza kwa ccm na serikali yake ili wapate wanachokitaka je tutajenga demokrasia kwa njia hizi?
inakera sana
Mie nilitegemea mheshimiwa Rais angemkemea Lukuvi na si Lissu. Nakumbuka waziri mmoja katika awamu ya mzee Mkapa aliishatoa kauli mbaya sana kwa waliokuwa wanamlilia Nyerere wamfuate huko aliko?Ndio wawakilishi wa JK,its true. birds of the same wings fly together.
Na za kumwamisha afisa wa Takukuru aliyemkamata na Rushwa wakati wa kura ya maoni hizo ndo akili zake.Nyingine alizo nazo kwenda kutishia watu kanisani huku yeye akiabudu vinyago na mizimu!!Lukuvi ni hasara ya taifa.lukuvi ana akili za kuvukia barabara tu
Kwani UBUNGE aliupataje?Si kwa njia hiyohiyo?Aliyekwambia Mrema ni mpinzani nani?Unajua wanasema hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho!Wenzetu hawa wanajisahahu mno.
Mie nilitegemea mheshimiwa Rais angemkemea Lukuvi na si Lissu. Nakumbuka waziri mmoja katika awamu ya mzee Mkapa aliishatoa kauli mbaya sana kwa waliokuwa wanamlilia Nyerere wamfuate huko aliko?
Mkuu, ni Ali Karume na si Amani Karume.Kama baba kavua NGUO kasimama mbele ya wanawe alafu akajiziba uso kwa viganja vyake, je watoto wake watafanya nini?
Kauli ya Lukuvi kanukuu kwa JK wakati anahutubia bunge. Kauli hiyohiyo kairudia Amani Karume pale Mwembeyanga temeke siku chache baada ya JK kuihalalisha bungeni. Kinana ananukuu kauli hiyohiyo nchi mzima. Swali la kujiuliza, je UKAWA watamchukulia hatua mtoto aliekaa uchi na kumwacha babake ambae ndo kaanza kusaula?
Kweli mkuu, kama rasimu hii bora ingeheshimiwa nchi nzima ingetulia na kupata katiba mpya ila kwa kuwa Rais hayupo radhi kuipata ndio maana tunaona juhudi nyingin mno zinafanywa kuikwamisha kwa kuingiza mambo ambayo hayamo kwenye rasimu kama matusi, kuvunja muungano, jeshi kupindua nchi na kadhalika.ccm wachochezi na wameshavuruga Amani ya nchi.
Mkuu, pana mmoja alisema Mapinduzi walifanyika Unguja na Pemba palipandishwa bendera tu. Hii Rais haioni ila kaona ukosoaji wa Lissu tu ndio mshiko.Nami natamani kupata CD 1 tafadhali durufuni nyingi muwape 'machinga' watuuziye huko mitaani kwetu.
Hivi hekima ndani ya chama chetu hiki kikukuuu imekwisha kabisa, hamna aliyesalia anayeweza kuwakemea waste a hovyo hovyo! Yale mashindano ya hoja siku hizo yamegeuzwa ni mashindano ya vioja, kazi tunayo.
Eti wengine wananufaika na muungano wa serikali mbili kwa sababu ya vitunguu; na wengine wanaambiwa Mapinduzi hayakuja kirahisi, hivyo kama Pemba inahitaji kuongoza sharti wajiandaye kupindua la hasha; hawataongoza visiwa kamwe!
Wananchi ndo mnajukumu la kuweka mambo sawa; kazi kwenu
Hivi hatuwezi kumshitaki Lukuvi kwa hili?
Kama baba kavua NGUO kasimama mbele ya wanawe alafu akajiziba uso kwa viganja vyake, je watoto wake watafanya nini?
Kauli ya Lukuvi kanukuu kwa JK wakati anahutubia bunge. Kauli hiyohiyo kairudia Amani Karume pale Mwembeyanga temeke siku chache baada ya JK kuihalalisha bungeni. Kinana ananukuu kauli hiyohiyo nchi mzima. Swali la kujiuliza, je UKAWA watamchukulia hatua mtoto aliekaa uchi na kumwacha babake ambae ndo kaanza kusaula?
Mwenye link ya Youtube ya hiyo hotuba ya Lukuvi Kanisani aitupie hapa.
Twataka tujuwe mbichi na mbivu.
Tumemsikia Lipumba alivyoeleza na tumesikia Lukuvi akijiuma uma bila kutaja aliyoyaongea. Tunataka hiyo video tujisikilizie wenyewe na tuamue nani mkweli, Lipumba au Lukuvi.
Muda mwingine si elimu peke yake inayosaidia,bali hata umri na busara pia uwa ni msaada tosha!tunapoelekea siko kwenyewe kabisa