Hotuba ya Mama Samia Inatoa Mwelekeo wa Tanzania Mpya

Hotuba ya Mama Samia Inatoa Mwelekeo wa Tanzania Mpya

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Hotuba ya mama inatoa uelekeo wa Tanzania mpya. Ameongea mambo mengi lakini nitatoa maoni kwenye manne;

1. KODI Mama hataki matumizi ya nguvu kwenye kodi. Anajua wafanyabiashara wanatishwa kupewa kesi za uhujumu uchumi ili kulipa kodi. Huu ndio ulikua mchezo wa TRA kwenye utawala wa "mwendazake". Sasa mama amepiga stop ubabe wa TRA.

Lakini naomba asiishie hapa, apitie pia kesi zilizopo mahakamani, huenda wapo waliobebeshwa mzigo mkubwa wa kodi wakashindwa kulipa wakapewa kesi za uhujumu uchumi, awaachie huru.

Amehoji kuhusu wafanyabiashara kudaiwa malimbikizo ya kodi ya miaka iliyopita, wakati wana tax clearence kutoka TRA. Hili ni suala ambalo Tundu Lissu alihoji mwaka jana, akasema si sahihi kudai malimbikizo ya kodi wakati kila mwaka mtu analipa na mnampa tax clearance. Mlimpaje clearence kama hakumaliza kulipa?

Lakini kama kawaida MATAGA wakamtukana. Wakamuita Kibaraka. Na wakasema serikali isiyokusanya kodi ni dhaifu. Mwendazake nae akapigilia msumari kuwa kulipa kodi sio hiyari, ni lazima. Basi TRA wakapata nguvu ya kuendelea kunyayasa watu.

Leo mama ameongea kile alichoongea Lissu mwaka jana. Kutumia mabavu kupata kodi sio njia sustainable. Unaweza kumtisha mtu akakulipa mabilioni leo lakini akafunga biashara yake. Je kesho utatoza wapi kodi?

Lissu alieleza kisa cha rafiki yake aliyefunga kiwanda baada ya kudaiwa kodi Bilioni 48. Yani gharama ya kodi inazidi thamani ya kiwanda. TRA wakatia kofuli kiwanda na kwenda kufreeze account zake bank. Wafanyakazi zaidi ya 300 wakapoteza ajira, mashine zikaharibikia na jamaa akashindwa kutoa hata senti moja kwenye account zake maana wamezifreeze.

Fikiria serikali imepoteza mapato kiasi gani kwa mtu kama huyu? Alikua analipa maji, umeme, kodi ya ardhi, ushuru halmashauri, kodi ya TRA, bado wafanyakazi wake wanakatwa kodi kwenye mishahara yao. Leo vyote hivyo vimepotea kwa sababu ya "ujinga" wa TRA kutaka kodi kubwa kwa mabavu.

Mama amesema huo ujinga uishe kuanzia leo. Ni muhimu watu kulipa kodi, lakini sio kwa dhuluma. Watu wapewe elimu, na TRA wasimamie ukusanyaji kwa mujibu wa sheria sio kwa mabavu. Mama kasema kodi ya dhuluma hataki.

2. UhuruWaVyomboVyaHabari; Mama kasema hataki kusikia vyombo vya habari vimefungiwa na vilivyofungiwa vifunguliwe haraka. Kama media zikifanya makosa basi zipewe adhabu mbadala lakini sio kufungia. Huu ni ushindi mkubwa kwenye uhuru wa habari. Uhuru wa habari ulionekana hauna maana. Ukiongea jambo lisilomfurahisha "mwendazake" unafungiwa au unashtakiwa.

Ridhiwani aliwahi kusema baba yake akiwa Rais aliwahi kusemwa vibaya na gazeti fulani. Akamuuliza, hivi haya yanayosemwa huyasikii? Mzee JK akamjibu "mwanangu Katiba imenipa power kubwa sana, nikisema nitumie power hiyo kwenye kila jambo linaloniudhi nitaumiza watu wengi sana. Waache waongee, kwa sababu hata wakiongea bado nitabaki kuwa Rais wao" Hii ilikua hekima kubwa sana.

Lakini wakati wa "mwendazake" mambo yakawa tofauti. Media zilipigwa spana, na akatamka hadharani kwamba "msifikiri mna uhuru to that extent". Baada ya hapo tukashuhudia magazeti yakifungiwa, TV zikifungiwa, radio hadi online TV zikifungiwa. Nchi ikaingia gizani.

Hakuna kuisema serikali wala kuikosoa tena. Kuna wakati media ziliogopa hata kualika viongozi wa upinzani kwenye interview kwa hofu ya kufungiwa.

Sasa mama kasema imetosha. Watu wapewe haki yao ya kusema. Na mpe viongozi wasikilize yote, yanayowafurahisha na yasiyowafurahisha then wataamua yapi wafanyie kazi, lakini katika yote watapata la kujifunza.

Aliyekua Mwenyekiti wa TUCTA Nicholus Mgaya aliitisha mgomo wa wafanyakazi kudai nyongeza ya mishahara. Siku chache kabla ya mgomo alifanya press pale idara ya habari (Maelezo). Akaponda sana uongozi wa JK na alipomaliza akaenda TBC kuongezea vidonge. Hakuzuiwa na mtu.

Kesho yake JK akaitisha mkutano na wazee wa Dar es Salaam akajibu hoja zote za Mgaya. Na akajibu huku akitabasamu. Mgaya hakukamatwa, hakutishwa wala hakutekwa. Huu ndio uhuru wa maoni tunaoutaka. Hoja inajibiwa kwa hoja. Unafikiri JK alishindwa kumdhibiti Mgaya kibabe? Angeweza lakini hakuona sababu ya kufanya hivyo.

Lakini Mgaya angethubutu kufanya hivyo kwenye utawala wa "mwendazake" angekiona cha moto. Kwanza asingeruhusiwa kufanyia press pale Maelezo kwa sababu ni ukumbi wa seeikali. Na kama wangemruhusu basi Mkurugenzi angefutwa kazi haraka. Na hata angefanyia press nyumbani kwake media zisingeruhusiwa kwenda, na ambayo ingeenda ingefungiwa.

Hao TBC ambao Mgaya alienda akapewa airtime ya 'kumsimanga' Rais, ingekua wakati wa "mwendazake" wangekiona cha mtema kuni. Kwa hiyo lazima tukubali kuwa tulifika mahali pabaya sana kwenye uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza. Angalau mama ameonesha nia ya dhati ya kutaka kurudisha uhuru huo. Tumpongeze na kumtia moyo.

UhusianoWaKimataifa; Mama kamwambia Waziri Mulamula kuwa ana kazi kubwa sana ya kurejesho mahusiano na mataifa ya nje. Pigia mstari neno KAZI KUBWA SANA. Maana yake ni kwamba mama anajua tulishavuruga sana huko duniani. Yani tunanuka. Tulimtukana kila mtu tuliyeona ana mawazo tofauti na sisi.

Maiti za watu zilipookotwa kwenye viroba, mataifa yaliyosema uchunguzi ufanyike tukawatukana na kuwaita mabeberu, eti wanataka kuingilia mambo yetu ya ndani.

Walioshauri tutumie mbinu za kitaalamu kupambana na Covid tukawatukana kuwa ni vibaraka. Walioshauri kwamba tuimarishe diplomasia yetu kimataifa tukawajibu hovyo kwamba sisi ni nchi huru na ni matajiri hatubabaishwi.

Kwa kifupi tulizorota sana kwenye masuala ya diplomasia ya kimataifa. Zaidi ya Burundi na Uganda hatukua na rafiki mwingine wa kueleweka, maana tulishawavuruga wote. Tulikua radhi kukosana na Marekani anayechangia 60% ya bajeti yetu ya afya, halafu tunamkumbatia Burundi anayekuja kukopa mahindi kwetu akalishe watu wake. Hivi kweli tuna akili?

Ndio maana mama amesema Waziri Mulamula ana kazi kubwa sana ya kurudisha mahusiano ya kimataifa.

4. #COVID19; Mama kasema hatuwezi kuendelea kupambana na corona kienyeji. Ameshauri njia za kitaalamu zitumike. Utafiti ufanyike na tuone tunawezaje kuwa salama kama taifa.

Hii ni hoja ambayo imezungumzwa sana na wapinzani lakini wakaishia kutukanwa na kuitwa vibaraka wa mabeberu. Hatuwezi kupambana na corona kama tunapambana na mapepo. Corona sio mapepo, lazima mbinu za kisayansi zitumike.

Na kutumia mbinu za kisayansi haimaanishi kwamba tumemuacha Mungu. Mungu hajasema tupuuze sayansi, ndio maana tukipata ajali tukavunjika tunaenda hospitali tunatibiwa lakini haimaanishi tumemuacha Mungu.

Lakini "mwendazake" alituaminisha kwamba kutumia sayansi ni kumuacha Mungu. Na kwa ujinga wetu tukaamini. Hatukumuuliza mbona watu wakiugua malaria hatuwazuii kwenda hospitali tuwaambie wamtegemee Mungu?

Kumtegemea Mungu haina maana uache kutumia njia za kisayansi kukabiliana na magonjwa. Ukijifanya unamjua Mungu sana ukaacha kutumia akili, naye atakuacha aone "ujuaji" wako utakufikisha wapi. Ukiikataa sayansi, ikatokea umepigwa na corona utakufa. Na Mungu hataingilia, kwa sababu alikupa akili zikusaidie ukakataa.

Kwahiyo mama katoa uelekeo mzuri kuhusu maambukizi ya corona. Kwanza ametaka takwimu ziwe wazi. Sio unafuatilia takwimu za maambukizi ya corona duniani ukifika Tanzania unakuta dash. Hapana. Takwimu ziwe wazi.

Takwimu zitatusaidia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kujua namna ya kujikinga. Tikijua idadi ya wagonjwa tulionao itasaidia kujua tatizo linaongezeka, au linapungua na tukabiliane nalo kwa njia gani. Lakini kama hutaki kujua takwimu utakabilianaje na tatizo? Ni sawa na nyoka wameingia ndani kwako halafu hutaki kujua wapo wangapi. Sasa utapambanaje nao? Jua kwanza idadi yao, kisha ndio utengeneze mbinu za kupambana nao.

Mama kasema anaunda timu ya wataalamu wa kwenda kufuatilia kujua yanayoyoendelea huko duniani kuhusu covid19. Hii ni habari njema maana MATAGA ndio waligeuka wataalamu wakati wa utawala wa "mwendazake".

Wakawa wanapiga propaganda hata kwa mambo wasiyoyajua. Mara chanjo ni mpango wa wazungu kutuua, mara chanjo inagandisha damu, mara chanjo inazuia watu kuzaliana, na propaganda nyingi za namna hiyo. Na "mwendazake" akawaamini MATAGA kuliko wataalamu. Lakini mama kawapa za uso MATAGA na kuamua kutumia wataalamu.

Maana MATAGA walitumia chanjo ya Astra Zanaca kupotosha kuhusu chanjo zote. Wakasema inagandisha damu, inaua, inafanya watu wasizalianebetc. Wakasahau kwamba chanjo zipo nyingi sio Astra Zanaca peke yake. Kuna zaidi ya chanjo 28 ambazo zimeidhinishwa na WHO kupambana na Covid19.

Kwahiyo wataalamu wakishaenda kuzifanyia utafiti watatuambia ipi inatufaa. Kama Astra Zanaca ni mbaya, tuchague nyingine. Na kama zote ni mbaya basi watushauri kitaalamu nini tufanye. Huo ndio umekua ushauri wetu wa muda mrefu lakini tukaishia kuitwa vibaraka wa mabeberu. Sasa leo Mhe.Rais amepita mulemule. Je nae ni kibaraka wa Mabeberu? MATAGA mtaficha wapi sura zenu?

Halafu suala la chanjo ni hiyari. Kama wataalamu wataona kuna umuhimu wa sisi kupata chanjo, haitakua lazima wote tuchomwe. Wale watakaohitaji watachomwa na wasiohitaji wataachwa. Simple like that.

Lakini kukataa chanjo kwa hoja za MATAGA ni aina nyingine ya ufala. Hadi hapo ulipofikia umechomwa chanjo ngapi? Hao wazungu wanaotaka kukuua kwa chanjo ya corona kwanini wasikuue kwenye chanjo zingine? Umedungwa chanjo ya pepopunda, polio, surua, tetekuwanga, ndui, Homa ya ini etc na zote zimetoka kwa mabeberu lakini hazijakuua, ndio chanjo ya Covid ije kukuua? Huo ni ufala.

Sasa Mama amekataa ufala huo. Ameamua kuunda timu ya wataalamu ituletee majibu ya kitaalamu. Kwahiyo tutapambana na Covid kitaalamu huku tukiendelea kumuomba Mungu.

Sio mtu anakusimanga ukivaa barakoa, anakwambia vua Mungu atakulinda, lakini yeye amezungukwa na walinzi 20 wanamlinda. Unajiuliza mbona yeye hajaacha walinzi amtegemee Mungu? Au Mungu anatulinda kwenye covid tu na sio mambo mengine?

Tuache ujinga. Kutumia sayansi sio kumuacha Mungu. Tutajilinda kwa mbinu za kisayansi na tutaendelea kumuamini Mungu. Mama ndo kashasema. Kama umenuna we nuna tu lakini habari ndo hiyo. Tumebadili gia angani. Tumeamua kuachana na "ramli chonganishi" na "nyungu za kisarawe" sasa tunakwenda kisayansi.

Bado ubao unasoma MAMA 3 MATAGA 0.!

Malisa GJ
 
“Mirerani tumejenga ukuta, kuta la kwelikweli tukaweka na Majeshi, lakini Madini yanatoroshwa kama mwanzo, tukibahatika kuliona linaoneshwa hili hapa, piga picha, bonge la Tanzanite, tunajua mabonge mangapi yamepitishwa chini kwa chini yakatoka?, hatujui”———Rais Samia

“Ndani ya Mirerani kuna vitaru, kitaru C kimewekwa akiba lakini sasa kimeanza kuvamiwa, nataka niseme sitaki kuona mkono wa Mtu kwenye kitaru C, walioanza kugawa vitaru kwenye hilo eneo acheni kina matumizi yake”———Rais Samia

“Mirerani tuongeze ulinzi na ulinzi wa pale sio ulinzi wa mabunduki ya CDF, mnajua wenyewe jinsi ya kuwalinda Wachimbaji wenu wasitoroshe Madini, CDF analinda juu Watu wanatorosha chini ya ardhi wanatokea huko, mkapasimamie vizuri”———Rais Samia
#MillardAyoIkuluUPDATES
 
Mkuu bado mapema Sana pendeni kujipa muda.

Kwasasa Mimi nitakaa kimya kwanza huku nikiendelea kupima utawala wa mama Samia then nikishajilidhisha ndo nitakuja hapa kuanzisha uzi.

Kwasasa bado asubuhi Sana kujua siku itaisha je japo nyota njema huonekana asubuhi.
 
Back
Top Bottom