Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Kwa wazanzibari na sio kwa wazanzibara
Natumai ulikuwa na maana ya Raza.....Kwa vile hakuna wahindi au mafisadi papa Zanzibar? Hao wakina Reza, Yasmin Aloo n.k....
Amandla......
Natumai ulikuwa na maana ya Raza.....
.Kinachonihangaisha mimi kwenye sherehe hizi za Mapinduzi Daima ni itifaki inavyovurugwa. Rais wa JMT anaonekana mdogo kwa Rais wa SMZ! Hili liko hivi kwa muda mrefu tu tangu enzi za Mwalimu. Katiba ya JMT inawekwa kando kwenye sherehe hii!
.
Zile Sherehe za Mapinduzi, sio sherehe za muungano, ni sherehe za ile nchi ilikuwa Zanzibar kabla ya muungano
Nchi hiyo haipo! si ndio ule mjadala ulivyoishia. Au kuna mwingine uliisha tofauti?Hapo naona Pasco unaendeleza ule ukoloni wako, kwa kusema Zanzibar si nchi tena baada ya Muungano.
Zanzibar ni nchi hata baada ya muungano...licha ya Pinda kusisitiza kama Zanzibar si nchi.
Taifa hili la Zanzibar lipo na wananchi wake bado tuko hai, na wala halitaondoka katika ardhi ya dunia.Licha ya ndoto za Pinda za kulifuta taifa hilo duniani.
Cheers...
Tangu lini dhahabu, almasi n.k. vimekuwa vya watu wa bara peke yao? Mapato yake yote si yanakwenda kwenye wizara ya fedha ambayo ni ya muungano? Jeshi,mabalozi, vyuo vikuu si vyote vinahudumiwa kutokana na mapato hayo? Vyote hivi si vinatoa huduma kwa Zanzibar pia? Mahospitali nayo si yanahudumiwa kutokana na mapato hayo? Wazanzibari si wanapata huduma katika hizi hospitali kama mtanzania mwengine yeyote? Mimi ningeelewa kuwa hayo madhahabu, matanzanite, gesi, pamba, kahawa ni vya watu wa bara peke yao kama wangekuwa na wizara yao ya fedha na bajeti yao peke yao. Katika hali iliyopo sasa, si sahihi kusema kuwa hivyo ni vya bara. Wakitaka iwe hivyo basi tuwe na wizara ya fedha yetu kama ilivyo Zanzibar. Hapo nasi tutafaidika na hayo madini kama vile wenzetu wanavyofaidika na karafuu yao!
Amandla......
[/LIST]Mimi kwa kawaida yangu ni kama tomaso huwa siwaamini sana wanasiasa
tatizo si kusema tatizo ni kutenda inapofika kwenye utekelezaji wako tayari hata kupinga walichosema jana yake,
Kwanza kauli yake 'hatogombea kwa mjibu wa katiba ' ni sawa, lakini ina maana ingekuwa si katiba alikuwa bado anataka kuendelea, je katiba ingasema vipindi kumi ina maana asingepisha wengine angekuwa raisi maisha? nina wasi wasi na kauli hiyo nasubiri vitendo.
Vile vile si mara ya kwanza kutoa hakikisho la uchaguzi huru na wa haki Zanzibar kila mara viongozi wamekuwa wakiimba hilo hata Komandoo Salimin ndio ulikuwa wimbo wake wa kila siku hatujasahau eti kila uchaguzi unapokuja wenyewe ni mashaidi wa vurugu za Zanzibar zikiongozwa na jenjewedi na polisi, sipingi kama kweli ana nia nzuri lakini nasubiri utekelezaji wake.
Rais Karume amesema mara ngapi kwamba kila Mzanzibar mwenye sifa ya kupiga kura ataandikishwa kila mwenye ZaID ataandikishwa matokeo yake nini masheha ndio wamekuwa waamuzi wa nani aandikishwe wakiongozwa na ma-DC yote yamekuwa yakifanyika kupingana na kauli za rais sijui ni kitu gani special alichofanya leo kinifanye niamini, ndo maana nimesema mimi ni kama tomaso.
Kuhusu suala la mafuta na gesi kuwa ni ya Zanzibar tu au la, hili sina uhakika nalo zaidi kwa sababu hata hayo mafuta ndo bado yanatafutwa hadi yatakapopatikana. Siwezi kwa sababu sijui yatapatikana wapi Unguja, Pemba, Mafia au Lindi sasa yakipatikana Mafia sijui wazanzibar watasema yao au yakipatikana baharini sijui mipaka ya Rep. of Tanzania inaishia wapi. Whatever the case kama dhahabu huwa inaenda hazina basi chochote kitakachopatikana kwenye mafuta na gesi kiende hazina, nafikiri hazina wana fomula ya mgawanyo wa kila kitu.
Nakubaliana nawe kuwa wanasiasa hawaaminiki lakini si huwa tunawachaguwa baada ya kusikiliza ahadi zao? Basi hatuna budi kuwasikiliza na pili kwani hapo nyuma si alikuwa muwazi kueleza tunayoyaona mabaya? Basi ni hatuwa kuwa sasa angalau anazungumza mazuri, natufarijike kidogo tukingojea hali halisi.
Ama hili la Mafuta na Gesi , kutopatikana au kupatikana muungwana hangojei matokeo kueleza msimamo wake na Zanzibar huo ni msimamo wao iwapo yatatoka Bara yatakuwa ya Bara peke yao na yakitoka Zanzibar yatakuwa yao peke yao, pana tabu hapo?
Ndugu Matumizi ya Serikali yanafanywa kwa kupitia Bajeti. Naomba nijibu maswali mawili
!. kwenye kikao kule Dodoma Waziri gani wa Wizara huwasilisha Bajeti ya Wizara za Zanzibar na tunajuwa kuwa Wizara ya Fedha haitumii fedha bila idhini ya Bunge.
2. Ule wakati wa Bajeti kule Baraza la Wawakilishi uliwahi kusikia lini kuwa Wizara ya Fedha ya Muungano imetowa Fedha za kugharamia hiyo Bajeti?
Naomba unipe majibu hayo ili tuendelee na hayo ya Mabalozi, Hospitali na vyuo.
Naona hata wanachama na wapenzi wa CUF wameunga mkono muafaka huo, kama inavyoonekana kwenye picha hii, ambapo wanacuf wakipita mbele ya Rais Karume...
Picha kwa hisani ya Father Kidevu
Nchi hiyo haipo! si ndio ule mjadala ulivyoishia. Au kuna mwingine uliisha tofauti?
Yes, ni ngumu sana kuwaamini wana siasa maana wameamua kusema lolote lile tunalotaka kulisikia bila kujari litakuwa na matatizo gani mbele ya safari.Nimefarijika kuwa akina Tomaso tuko wengi. Hata siku moja siwezi kumuamini mwanasiasa. Siasa ni kusema kile watu wanataka kusikia wakati huo hata kama kitu hicho unajua ni ndoto za alinacha. Kwangu mimi sikiliza hotuba za wanasiasa wakati mwingine ni sawa na kuangalia watoto wanaocheza kidari po! Nothing is real and genuine! Tusubiri hadi Oct tuone.
Poleni sana. Tatizo ni kuwa hamtaki kuuulewa huu mfumo wa Muungano wetu wenyewe. Zanzibar wanataka mafuta yakionekana Zanzibar yawe ni ya Zanzibar (ambayo ipo kwa mujibu wa mfumo). Na yakionekana Mafia au Songea au Biharamulo hayo ni ya Tanzania-kwa sababu hakuna kitu Bara au Tanganyika. Hivyo vimefutwa. Hamtaki kuelewa tu jamani?Wapi wazanzibari wametamka kuwa mafuta yakipatikana bara yawe ya bara peke yao na sio ya Muungano?
Amandla......
Mr.Froasty said:Hapa unaonekana kuonesha kama huu ni ubaguzi, lakini hii hoja haina mshiko.Chukulia mfano Hong-Kong na wachina wa kawaida.Ukiwa wewe ni mchina wa kawaida kuingia Hong-Kong ni sawa na unakwenda Europe, ni lazima ufanyiwe control za immigration na kila kitu.
Lakini alieko Hong-Kong, anaingia sehemu zengine za China kama kawaida.
Sasa hii sio bahati mbaya, kwani wakiachiwa hao wachina wote watakimbilia Hong-Kong na athari zake zinajulikana.
Sasa na Tanganyika kuwekewa vizingiti Zanzibar ni sawa kabisa, kwani watanganyika wote hawawezi kuingia visiwani humo.Ni sehemu ndogo, na ardhi yake ni ndogo.Watanganyika 0.5Mil tuu wahamie Zanzibar, tayari hiko ni kishindo na visiwani huwezi hata kujamba.
Aidha kwa suala la dhahabu na madini mengine Zanzibar inanufaika vipi?Mie sioni jinsi wanavyonufaika.Hii ni general case ya muungano kuwa unanufaisha Tanganyika tuu na kuiwekea guu Zanzibar isiende mbele wala isifurukute.Bajeti yote ya Tanzania ni kuhusiana na Tanganyika tuu, sijawahi kumsikia JK akisema bajeti hii ni kujengea barabara kule Msuka (North-Pemba).
Sasa FUTA wacha wazenji wale peke yao acheni uroho, kuleni Tanzanite....hamushibi?