Mr.Froasty said:
Hapa unaonekana kuonesha kama huu ni ubaguzi, lakini hii hoja haina mshiko.Chukulia mfano Hong-Kong na wachina wa kawaida.Ukiwa wewe ni mchina wa kawaida kuingia Hong-Kong ni sawa na unakwenda Europe, ni lazima ufanyiwe control za immigration na kila kitu.
Lakini alieko Hong-Kong, anaingia sehemu zengine za China kama kawaida.
Sasa hii sio bahati mbaya, kwani wakiachiwa hao wachina wote watakimbilia Hong-Kong na athari zake zinajulikana.
Sasa na Tanganyika kuwekewa vizingiti Zanzibar ni sawa kabisa, kwani watanganyika wote hawawezi kuingia visiwani humo.Ni sehemu ndogo, na ardhi yake ni ndogo.Watanganyika 0.5Mil tuu wahamie Zanzibar, tayari hiko ni kishindo na visiwani huwezi hata kujamba.
Aidha kwa suala la dhahabu na madini mengine Zanzibar inanufaika vipi?Mie sioni jinsi wanavyonufaika.Hii ni general case ya muungano kuwa unanufaisha Tanganyika tuu na kuiwekea guu Zanzibar isiende mbele wala isifurukute.Bajeti yote ya Tanzania ni kuhusiana na Tanganyika tuu, sijawahi kumsikia JK akisema bajeti hii ni kujengea barabara kule Msuka (North-Pemba).
Sasa FUTA wacha wazenji wale peke yao acheni uroho, kuleni Tanzanite....hamushibi?
Mr.Froasty,
..tunachotaka ni usawa ktk muungano huu. kama suala hilo haliwezekani baina ya Tanganyika na Zenj ni bora Muungano uvunjwe.
..ninachosema mimi ni kwamba Wazenj wawekewe masharti yaleyale wanayokumbana nayo Watanganyika wanapofika Zenj.
..nakumbuka majuzi hapa kuliibuka suala la vibali vya kazi Zenj. ilielekezwa kwamba Watanganyika watakuwa-treated kama raia wengine wa kigeni ktk masuala masuala ya kazi Zenj. yaani Mtanganyika anakuwa hana tofauti na Msudan,Mnigeria etc.
..kama ni mashirikiano ktk muungano, basi yasielemee kwa wa Tanganyika kama ilivyo sasa hivi.
..kwa mfano: kama mnadai Zenj ni ndogo sana, na uwezo wake ni kupokea wahamiaji 1000 tu kwa mwaka toka Tanganyika, basi Tanganyika nayo isipokee Wazenj zaidi ya 1000 kwa mwaka.
..kwasasa hivi Mzenj akiingia Tanganyika anakuwa na haki zote kana kwamba amezaliwa upande huu. lakini hilo haliwezekani kwa Watanganyika kwanini? kwanini hakuna usawa ktk muungano huu?
..pia si kweli kwamba Wazenj hawafaidiki na madini na rasilimali nyingine zinazopatikana huku Tanganyika. Wazenj wana uwezo wa kumiliki ardhi huku Tanganyika. kuna maeneo ktk miji ya Tanganyika ambako Wazenj wana majumba makubwa makubwa, mashamba makubwa, biashara, na hakuna anayewasumbua.
..pia Wazenj wanayo haki ya kumiliki machimbo ya madini[dhahabu,tanzanite,ruby,... yoyote yale yanayopatikana Tanganyika. sasa hii habari kwamba waZenj hawafaidiki na "dhahabu" za Tanganyika yanatoka wapi?
NB:
..kuhusu suala la bajeti ni kweli huwezi kusikia suala la barabara za Zenj ktk bunge la muungano. hii ni kwasababu suala la barabara siyo la muungano. lakini inaposomwa bajeti ya wizara kama ulinzi, au ile ya mambo ya ndani, basi Zenj iko-included humo. hapa ni suala la kuelewa tu wizara zipi zinashughulika na masuala ya muungano.
..nilitegemea ungekwenda mbali zaidi na kuuliza kwanini wabunge toka Zenj huhudhuria na hupokea posho za vikao vya bunge vinavyozungumzia masuala yasiyo ya muungano?