S.M.P2503
Platinum Member
- Nov 25, 2008
- 3,689
- 7,145
HOJA YA MWANZO: Tume haina jipya… CCM kaeni na Chadema…
1: Tume hii haitakuwa na jipya kwa sababu ni tume ya kufunika ukweli, si kuutafuta.
Hakuna tume inayoundwa na mtuhumiwa na ikaweza kutoa majibu ya kweli.
Huwezi kuwa kiongozi wa tukio, mshukiwa wa kosa, mwigizaji wa tukio, halafu ujiteue kama mwamuzi wa tukio. Hicho ndicho kinachoitwa kesi ya kuku kumuaminisha Nguchioro awe hakimu- lazima kuku aliwe tu.
2: CCM haiwezi kukaa na Chadema kwa sababu tatizo sio Chadema, tatizo ni CCM.
Wahasimu sio vyama vya siasa; wahasimu ni mfumo wa mabavu, tume haramu, polisi wanaotumika vibaya, na viongozi waliozoea uhalali wa urithi badala ya ridhaa ya wananchi.
Tatizo la nchi si Chadema, tatizo ni udhalimu uliokithiri.
TWENDE KAZI : HOTUBA YA RAIS - HOJA KWA HOJA:
“Tumsifu Yesu Kristu na asaal alieikum …aliye turejesha pamoja…”
Kuanza kwa kulitaja jina la Mungu haihalalishi ukandamizaji.Hata madikteta wengi wameanza na “Tunamshukuru Mungu.” Mungu hawezi kuhusishwa kwenye tume ya kupaka rangi damu ya wananchi waliodhulumiwa au kuuwawa.
3. “Tume ya ndani kwanza, nje baadaye…”
Hiyo ndiyo hadithi iliyotumika kuficha ukweli kila mara:
“Tume ya ndani kwanza, halafu nje.”
Lakini kwa uzoefu, tume za ndani zinatupatia:
– majibu ya ndani,
– uongo wa ndani,
– usanii wa ndani,
– uhalalishaji wa ndani wa uovu wa ndani.
Ukweli tunahitaji tume huru: UN, AU, EU au mchanganyiko, si tume ya watu walioteuliwa na mhusika anayeshutumiwa.
4.“Tukio halikutarajiwa kwa sababu historia yetu ni ya amani…”
Historia ya amani haimaanishi kukubali ukandamizaji. Amani ya kukandamiza haki sio amani, ni ukimya wa wanyonge. Wananchi hawakutoka barabarani kwa sababu wanapenda vurugu; walitoka kwa sababu hali imewadia shingoni. Hakuna tume inayoweza kufuta kilichosababisha hasira ya wananchi.
Majukumu ya Tume: Rebuttal kwa kila kipengele
1. “Kutueleza chanzo halisi cha tukio.”
Chanzo kipo wazi: uchaguzi haramu, matokeo yenye utata, kuporwa ushindi, na kukataa mageuzi ya lazima. Hayo hayataki tume; yanataka uhalali na uwajibikaji.
2. “Kuchunguza madai ya vijana waliodai haki.”
Vijana hawakudai “haki hewa”, walidai haki ambazo zimependekezwa mara mia:
– Tume huru ya uchaguzi
– Katiba mpya
– Uchaguzi unaoaminika
– Uhuru wa mikutano
– Uhuru wa siasa
Hivi ni vitu vinavyojulikana.
Tume haiwezi kuuliza swali ambalo limejibiwa kwa miaka 12 na Zaidi, kila mtu anajua jibu lake, unless kama tume hii ni ya Watanzania wanaoishi Mbinguni ndio hawajui ni nini kinachotakiwa kufanyika, sio kurembesha rembesha maneno..
3. “Kuchunguza kauli za upinzani kama ‘kitawaka’, ‘hakuna uchaguzi’, ‘lazima aondoke’.”
Kauli hizi si uchochezi; ni utambuzi wa ukweli. Huwezi kufanya uchaguzi bila uchaguzi.
Na ukivuruga uchaguzi, ni lazima watu waambiane ukweli: mfumo unaowatesa lazima uondoke. Kuchunguza kauli badala ya kuchunguza matendo ni kugeuza wahanga kuwa wahalifu.
4. “Kuchunguza mchango wa wadau wengine, NGOs, fedha, n.k.”
Hii ndiyo fimbo ya kutengeneza adui wa nje ili kuficha shida ya ndani. Wananchi hawakupokea fedha; walipokea uchungu. Umasikini, udhalimu, na ubabe haviitaji ufadhili kutoka nje, Uchungu na maumivu ya watu mioyoni mwao unatosha kuwasha moto wenyewe.
5. “Kuchunguza hatua zilizotumiwa kudhibiti vurugu.”
Hii si uchunguzi; ni kuhalalisha nguvu kupita kiasi. Nchi haihitaji majeshi ya zamani kututumia kama majaribio ya vita. Hatua zilizotumika zilikuwa za kupindukia kwa sababu tatizo lilikuwa kisiasa, si la kijeshi.
6. “Tume imepewa miezi mitatu…”
Tume nyingi za miezi mitatu zimezaa majibu yaliyofungwa kwenye droo ya ofisi ya rais.
Hii haitakuwa tofauti.Mapendekezo hayatatekelezwa kwa sababu tatizo sio kukosa mapendekezo, tatizo ni kukataa kuyatekeleza. Insanity ni kufanya kitu kile kile, miaka nenda rudi na mutegemee majibu tofauti. Nyie wajumbe wa tume , muje na roadmap ya namna ya kuhakikisha mapendekezo yenu yanatekelezwa , sio hizo ngonjera za kila siku.
7.“Wapo wanaodai tume ya nje, lakini mimi nina imani na hii ya ndani.”
Imani ya rais sio mbadala wa uaminifu wa taifa.Tume huru ni lazima iwe na mandate huru, wajumbe huru, na chanzo huru cha uteuzi. Tume ya uteuzi wa upande mmoja haiwezi kuwa huru.
8. Maoni yangu- hoja nzito kuliko zote, kwenye hii hotuba ya leo: “Chadema ndio target… CCM walikataa minimum reforms, je full reforms watazikubali?” tusipotezeane muda kwa mambo yaliyo wazi … vinginevyo ni kuchezeana tu akili na weledi wa Watanzania million zaidi ya 60.
Ni kweli, CCM ilikataa minimum reforms kwa ushauri wa watu mbalimbali ikiwemo kutoika humo humo ccm yenyewe, kama ni kweli, sasa ni kwanini ijivike roho ya kukubali full reforms?
Haiwezekani leo wanatengeneza timu ya kufufua mfumo, halafu kesho wakubali kuubomoa.
Tume hii si suluhisho; suluhisho ni:
1. Mazungumzo ya kisiasa ya wazi, sawa, na ya uwazi.
2. Katiba mpya.
3. Tume huru ya uchaguzi.
4. Uwajibikaji wa waliokiuka haki za binadamu.
Tume iliyozinduliwa leo si daraja la maridhiano, ni bendera ya kufunika majeraha ya taifa.
Suluhisho haliko kwenye tume; lipo kwenye meza ya mazungumzo, sio kwenye jukwaa la propaganda. Hatuwezi kutatua mgogoro kwa kutumia watu waliosababisha mgogoro.
HOTUBA KAMILI HII HAPA:
View: https://www.youtube.com/live/GOfjDHTNSzQ?si=J28cnnkFW6KD-TiC