Hotuba ya Rais Magufuli imewatandika wengi wateule

Hotuba ya Rais Magufuli imewatandika wengi wateule

Mkuu mbona umesahau kuweka namba ya halotel maana voda inaweza isipatikane wakuu wakikupigia
 
Lakini amewakumbusha kuwa kama yeye hajakukubali huwezi toboa,hata upigiwe kura ukaongoza kwa 90% huna uhakika wa kupitishwa chamani.

Mchakato ndani ya CCM ni mgumu sana kipindi hiki.
wengi watalia na kusaga meno,kwa fedha na muda walioupoteza kisha majina yao kukatwa na mtu mmoja kwa matakwa yake mwenyewe kisha wanasema chama kongwe lenye demokrasia kumbe hamna kitu,hebu tujiulize kama wa ndani ya chama chake anawafanyia hivi je walionnje ya chama chake je?
 
Yeye ni alfa na omega na ameshasema anaongoza mhimili uliojichimbia chin zaid
 
Juni 18, 2020
Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui
Unguja, Zanzibar
Tanzania

Balozi Major General (retired) Issa Suleiman Nassor achukua fomu kutia nia Urais SMZ 2020

Video toka Maktaba AFCON Egypt

Hili ni jina geni katika masikio ya wengi panapohusika siasa za Tanzania, lakini sio geni katika uwanja wa kijeshi. Major General Issa S. Nassor alifikia ngazi ya Mkuu wa Mafunzo na Operesheni wa JWTZ (Head of training and operations of the Tanzania People’s Defence Forces TPDF)

Jenerali Nassor amelitumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa miaka mingi kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi nchini Misri kutoka mwaka 2017 hadi 2019. Makao yake yakiwa Cairo, Misri huku pia akiiwakilisha Tanzania katika nchi za Lebanon, Palestine, Libya, Iraq, Syria na Jordan. Major General Issa Suleiman Nassor aliwahi pia kuhudumu ktk Ubalozi wa Tanzania nchini India kama mwambata wa kijeshi Defence Attache ubalozini kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wetu nchini Egypt (2017-2019).

Picha toka maktaba:
Oktoba 5, 2017.

Picha baada ya kuapishwa kwa Balozi H.E. Major General Mstaafu Issa Suleiman Nassor kuwa balozi wa Tanzania nchini Misri akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais John Pombe Joseph Magufuli na Mkuu wa Majeshi General Venace Mabeyo, Ikulu Dar es Salaam 05 October 2017.

Japo si jina kubwa katika siasa, duru visiwani Zanzibar zinamuelezea kama mtu asiye na mafungamano na siasa za makundi.

Naye anatajwa kubebwa na karata ya utiifu wake lakini hana umaarufu katika siasa za Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Hatima ya nafasi yake ikiwa ataingia katika kinyang'anyiro itaamuliwa na
 
Duh! Kumbe zile kura za maoni kule majimboni ni kazi bure hata na wale wanaochukua fomu za urais kule ni bure nahisi tayari wazanzibar washachaguliwa wa kuwaongoza
 
TUMEMSKIA MH RAIS MAGUFULI LEO?


Na Elius Ndabila
0768239284

Leo Mh Rais akimuapisha Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya za Morogoro, Monduli na Arusha mjini ametoa hotuba ambayo inaweza kuwa msumali wa moto kwa baadhi ya viongozi. Hotuba ya Mh Rais ilikuwa na dhima nyingi, lakini ninataka nizungumze neno alilochomekea la *MRIDHIKE* na nafasi zenu.

Mh Rais amewataka wstumishi wa umma wote, hasa viongozi wake wateule kuridhika na nafasi wanazopewa. Amesema hakuna sababu ya kiongozi kutoridhika na nafasi yake aliyonayo wakati anafanya vizuri na ana miaka mingi. Amesema atawashangaa sana. Ametumia mfano IGP, CDF na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kama wanatamani kugombea ili akawateue Uwaziri. Mh Rais amesema ni haki yao kidemokrasia, lakini wanapoenda wawe na uhakika wa kushinda. Amesisitiza kuwa hata ukiwa wa kwanza si lazima iteuliwe kugombea kwani ninaweza kumteua hata mtu wa nne, anazungumza huku akitolea mfano Naibu waziri wa Mambo ya nje aliyeshika nafasi ya nne lakini akateuliwa kugombea.

Kwa tafsiri rahisi hotuba ya Mh Rais ilijikita kufikisha ujumbe kwa watumishi wengi ambao sasa ofisi zao hazifanyi vizuri na wako busy kusaka ubunge. Mh Rais inaonyesha wazi anajua kuwa wateule wake wengi wanaona sasa majukumu waliyopewa ni nonsense na kuona Ubunge ni bora. Kitendo cha Mh Rais kuzungumza hadharani inaonyesha wazi amekasirishwa na hatua hizo za wateule wake kuacha kazi na kumkimbiza na harakati za majimboni. Mh Rais amesisitiza kuwateua kugombea kwenye uchaguzi kunatokana na alivyoamka siku hiyo kwani anaweza kuwakata hata kama wanaongoza kura.


Dhana ya kutoridhika inaonyesha ndiyo iliyowaondoa aliyekuwa mkuu wa mkoa Wa Arusha na DC wake kwa kuwa wamekuwa wakigombana kwa miaka miwili mfululizo bila kufanya kazi zao vizuri. Ukimsikiliza kwa umakini Mh Rais akitoa wosia kwa wateule wapya amesema hakuridhika na migogoro kwa viongozi hao. Hata hivyo wadadisi wa mambo ya kisiasa wanasema Mh Rais kumtumia IGP, CDF na RC Iringa ilikuwa ni kufikisha ujumbe kwa Mh Gambo ambaye amekuwa akitajwa kugombea ubunge Ilala au Arusha kitu kilichopelekea kutotimiza vizuri majukumu yake na kutumia mda mwingi kugombana na wasaidizi wake na kuchochea migogoro ya kujipatia umaarufu.

Rai kwa watumishi wote wenye nia ya kwenda majimboni, jitafakarini kwanza, ongeeni na Mungu wenu kwanza kama mko tayari kurudi Misiri kama safari ya Kanani itashindikana. Mh Rais amekuwa mwema mno kusema hadharani hasa kutahadharisha. Wewe kama unaona bado Mungu hajasema nawe endelea kutimiza majukumu ambayo Mungu amemtumia mteule wake Mh Rais kukuamini, lakini kama wakati wa Bwana unasema sasa hapo ulipo umeshatumika vya kutosha na sasa ni wakati wa kwenda kuwawakilisha wananchi kwenye chombo cha kutunga sheria na kuishauri serikali nenda jimboni.
Rubbish post unapiga preiz? Namba ya nini? Na ww ni miongoni mwa wasomi kwa familia yako? Majanga
 
Back
Top Bottom