PostGE2025 Hotuba ya Rais Samia yawabubujisha Machozi ya Furaha watanzania

PostGE2025 Hotuba ya Rais Samia yawabubujisha Machozi ya Furaha watanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Embu acha ujinga wako hapa wewe unayeonekana kuwa mhamiaji Haramu. Maana Rais Samia ni kipenzi cha watanzania na ndio tuliompatia kura za ndio kwa kishindo kikuu ili aendelee kututumia.
Mwambie kwanza atupatie maiti za ndugu zetu tukazike halafu abaki na hao watanzania waliompatia kura
 
Unapata wapi tabasamu katikati ya majonzi, wale watu waliomiminiwa risasi za moto na kupoteza maisha damu zao hazitaenda bure.
 
AMENIKWAZA SANA angetakiwa atoe funzo kwa wale majizi, majambazi, vibaka na washenzi walichoma mali za watu binafsi angetangaza kuwanyonga ndani ya wiki 1 kuanzia leo, ni wachache na wangejifunza, hata wanaowatuma wangekoma na wangeacha rasmi, kwa hili nimechukia mpaka nimevunja TV leo

2. NARUDIA MSHAURINI atengue kauli awanyonge haraka hao majambazi ili itume ujumbe ni wachache sana hawafiki hata elfu 2
na yeye ni mwiz na jambaz angenyongwa nao
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika Rais Samia amegusa Mioyo ya watanzania, Amewapa Tabasamu,amewapa furaha . Ni hotuba ya Matumaini,ni hotuba iliyotoa Dira yenye matumaini,ni hotuba iliyounganisha Taifa ,ni hotuba ya kizalendo,ni hotuba iliyoonyesha Uwezo mkubwa wa kiuongozi alionao Rais wetu.

Ni hotuba yenye kuponya majeraha ,ni hotuba yenye kurejea utanzania wetu na Thamani ya undugu wetu. Ni hotuba iliyoonyesha Maana ya kiongozi wa watu na mtu wa watu ,ni hotuba iliyoonyesha maana ya Ukubwa ni Jalala.

Kwa Hakika Sijapata kuona Furaha , tabasamu na bashasha waliyonayo watanzania kama hii leo waliyokuwa nayo watanzania. Nimeshuhudia watanzania wakibubujikwa Machozi ya Furaha wakati na baada ya kumalizwa kwa hotuba ya Rais Samia.

Watanzania kwa furaha kubwa waliyokuwa nayo wamejikuta wakishindwa kujizuia kutoa machozi ya furaha na kujikuta mashavu yao yakiloa kwa machozi utafikiri wamepakwa pilipili au kukamuliwa vitunguu vya Igawa.

Imekuwa ni kama nyumba iliyokuwa ikisubiri kupata mtoto baada ya kupita miaka kumi ya ndoa bila kupata mtoto.

Niseme Ukweli wa dhati ya Moyo wangu kuwa kwa hakika Rais Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe. Ni chaguo la Mungu Mwenyewe.kainuliwa kwa mkono wa Mungu Mwenyewe. Kapewa kibali na Mungu Mwenyewe. Ni zawadi kwetu watanzania tunayopaswa kujivunia .

Tunakwenda kuiona Tanzania mpya ,Tanzania ya fursa ya kila aina, Tanzania ya maziwa na asali, Tanzania ya maendeleo ya uchumi,Tanzania yenye kumshirikisha kila mtu katika meza ya chakula , Tanzania yenye kumuwezesha kila mmoja wetu kupata milo mitatu mezani pake, Tanzania ambayo watanzania watakuwa wakila chakula watakacho na siyo kile kipatikanacho.

Tunakwenda kuiona na kuishuhudia Tanzania yenye Kutoa fursa za ajira maelfu kwa Malaki kwa vijana waliosoma na ambao hawajafika vyuo vikuu, Tanzania yenye madawa ya kutosha mahospitali ambapo mtanzania akienda hospitalini atapokelewa vizuri ,kusikilizwa vizuri na kupewa huduma bora na stahiki kwa unyenyekevu na upendo wa hali ya juu sana.

Tanzania ambayo watanzania watatembea barabarani wakiwa na nyuso za tabasamu na matumaini tele na siyo kuzungumza wenyewe kama vichaa au wendawazimu . Tanzania ambayo kila mmoja ataishi katika nyumba bora na yenye heshima na siyo kwenye mabanda ya bati kama kuku.

Tunakwenda kuiona Tanzania ya Rais Samia ambayo kilimo itakuwa ni fahari na kazi ya kujivunia badala ya kuwa kama adhabu au kazi ya wanavijiji,Tanzania ambayo kila mmoja wetu atajivunia utanzania wake na kutembea kifua mbele akiimba Tanzania nakupenda kwa moyo wooooteee .

Ngoja niishie hapa nakuja kuendelea baadaye kidogo.View attachment 3502023

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Admin staking unipige ban aisee. Pumbu za babu yake mtu.
 
Kwa mauaji hayo ya maelfu ya wananchi wasio na hatia machozi hayawezi kuwa ya furaha, ni ya huzuni mno..

Mauaji ya Mwaka huu October 2025 yamefikia zaidi ya 6,900 yamethibitika kwa Samia kupewa idadi hii na mtu ambaye anawasiliana naye moja kwa moja | JamiiForums Mauaji ya Mwaka huu October 2025 yamefikia zaidi ya 6,900 yamethibitika kwa Samia kupewa idadi hii na mtu ambaye anawasiliana naye moja kwa moja
Acheni uzushi na uongo hapa na kutumika vibaya kulichafua Taifa letu.
 
Rais Samia imeliheshimisha Taifa letu.
naomba vaa viatu vyangu/vyetu wengi , fuatilia post zangu niliumia mno kuharibu mali za watu sio maanamano. mfano mdogo kupata milioni 300 leoo ni kazi kidogo inakuja mtu anakuchomea gas station yako wakati hana ushahidi inahisika na mafisadi, wanamchomea mtu biashara yake ndo anakula hapo , anatunza mke watoto wake hapo na kulea wazazi wake hapo , YEYE AISHI KAMA NANI YAANI ANA UTOFAUTI GANI MKUBWA WA UPEKEE KULIKO MAMA YANGU ALIYENIZAA watoto wangu wanaonikumbatia asubuhi huku waniiita dady we love you, kweli huyo mbwa anayejiita GENZ KIBAKA, MWIZI, JAMBAZI ni wa kumsahehe? leo wamechoma mwendokasi hajui hata anayetumia ni yeye , SAMIA, MWIGULI HATA MIMI SIJAWAHI KUPANDA DALADALA toka 2001 na sintopanda hata basi ya mkoani sipandi lakini watu wangu wanapanda na wanaumia kisa mbwa koko anayejiita GNZ DAWA NI KUTOKOMEZA MBEGU CHAFU YOTE NYONGA WAPIGE RISAS
 
na yeye ni mwiz na jambaz angenyongwa nao
mimi ningekuwa kiongozi ningetunga sheria kali sana mwizi wa mali ya uma au rushwa adhabu yake ni kifo tu , china si unaona wanavyofanya vizuri
 
Hili Mwashambwa, sijui ni lini litakija kupata akili japo ilr ndogo kabisa!! Ni hasara kubwa sana kwa ndugu na wazazi wake
 
Amewapa Tabasamu,amewapa furaha
You need a sense of humor! Ubinadamu unalipa. Jaribu kusikitika na kuwapa pole Watanzania wenzetu waliojeruhiwa katika turmoil wakati na baada ya uchaguzi, waliofiwa na Ndugu ,jamaa, marafiki, na wananchi wenzao. Watakie heri waliotangulia mbele za haki. Kisha walaaninwalioamuru mauaji, walioshiriki mauaji, na walioharibu Mali za umma na za binafsi.
====
Unachoendelea kufanya hapa ni kuzidi kuchonganisha mamlaka na watoa mamlaka
 
Back
Top Bottom