Hotuba ya Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, Dr. Rugemeleza A.K. Nshala katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria

Hotuba ya Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, Dr. Rugemeleza A.K. Nshala katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria

Baada ya kusikiliza na kusoma hotuba zote ikiwemo ya Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika TLS na sifa aliyotoa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa TLS kuna jambo lililoongelewa la kuwapa imani waTanzania na wawekezaji.

Ni matumaini yangu sheria mpya iliyopitishwa na Bunge haitasainiwa na Mh. Rais bila ya kwanza kurudishwa bungeni kufanyiwa mabadiliko ili hicho kilichoongelewa kurudisha imani ya uhuru wa wanasheria na TLS kufanya shughuli zao bila kuingiliwa sana na serikali uonekane upo na kurudisha imani.

Bila hivyo kampeni za kushawishi wawekezaji na pia haki za asasi za kiraia na za mtu mmoja mmoja kuongelewa huku sheria kandamizi zikipitishwa itakuwa ni kazi bure na kutazidi kuwepo hali ya sintofahamu juu ya utawala huu wa CCM Mpya na serikali yake.

Muda ndiyo muamuzi kutuambia na kutuonesha kama kweli kuna nia njema toka ktk vyombo vya serikali, bunge na watawala waliopo madarakani.
 
Tuna mfumo ovyo kabisa wa sheria. Na watawala wanafurahia kwa sababu mioyo yao ni mibaya kuliko ya wakoloni. Kama laiti wangekuwa wanauchukia ukoloni, ugandamizaji, sheria zote za ovyo zingekuwa zilikwishaondolewa miaka mingi. Lakini badala yake tunazidi kutunga sheria za ovyo kuzidi hata zile za wakoloni.
 
Baada ya kuondoka manguli wa sheria Tundu Lisu na Fatma Karume, mmenaki vilaza ndipo anakuja kwenye mkutano wenu!

Sent using Jamii Forums mobile app

Bado mapambano ya kudai haki ya kuishi, sheria zisizo gandamizi na kuzingatia katiba yanaendelea na suala hili si la Dr. Rugemeleza Nshala, Tundu Antipas Lissu au Fatma Karume bali sote sisi ktk nafasi mbalimbali. Tukibaki watazamaji hakuna mabadiliko yanayoweza kutokea. Hata mijadala ktk mitandao ya kijamii kuongeza uelewa na mbinyo kwa watawala waache njia zao ovu.

Kamati ya Mabunge kuja Tanzania kuonana na mamlaka zinazohusika

 
Pascal Mayalla,
Kama msomi uliyesoma digrii ya sheria ulitakiwa unene maneno na paragraph nyingi zaidi. Kwa kuichambua hotuba hii ya Rais wa TLS ili uweze kutoa mchango wako kwa JamiiForums na waTanzania kwa ujumla wake.
Duh...!, Mkuu Bagamoyo, kumbe siku hizi jf hadi tuna monitors kuwapangia members za kuchangia!, kwanza mimi sio msomi kihivyo, pili kusomea sheria na kuwa na decree ya sheria, hakumfanyi mtu kuwa mwanasheria au mchambuzi wa sheria. Mimi japo ni kweli nimesomea sheria lakini kwanza sijawahi kujiita "the learned brothers", pili sijawahi kujiita mwanasheria, mimi siku zote ni mwandishi wa habari and I will remain mwandishi wa habari.
P
 
Duh...!, Mkuu Bagamoyo, kumbe siku hizi jf hadi tuna monitors kuwapangia members za kuchangia!, kwanza mimi sio msomi kihivyo, pili kusomea sheria na kuwa na decree ya sheria, hakumfanyi mtu kuwa mwanasheria au mchambuzi wa sheria. Mimi japo ni kweli nimesomea sheria lakini kwanza sijawahi kujiita "the learned brothers", pili sijawahi kujiita mwanasheria, mimi siku zote ni mwandishi wa habari and I will remain mwandishi wa habari.
P

Pascal Mayalla, ndiyo maana nimekutambua kama msomi na nashukuru kwa kulikubali hilo. Na uchambuzi wa mwandishi wa habari msomi siku zote unatambulika na kuheshimika. Nadhani kama ilivyo kwa wasomi naamini tayari una cha kuchangia kimawazo, lakini unajaribu kupiga polish mchango wako wakisomi na siyo masaa mengi utatoa maoni kama unaona inafaa kufanya hivyo. Hii ni heshima kubwa kutambuliwa ktk jamii.
 
13 Feb 2020
Arusha

Mahakama ya Rufani ya Afrika Mashariki yatoa hadi Mei kujua hatma ya rufani ya serikali ya Tanzania
Mahakama ya Rufani ya Afrika Mashariki imetaka mpaka kufikia mwezi Mei mwaka huu hatma ya rufani ya Tanzania ya kupinga hukumu ya mahakama hiyo iliyodai vifungu 18 katika sheria ya huduma za habari vilivyopitishwa na Bunge la Muungano la Tanzania na kutiwa saini na Mh. Rais Dkt. John Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vinakiuka mkataba wa kuundwa kwa jumuiya ya Afrika Mashariki.


Source : Azam TV
 
Back
Top Bottom