Zanzibar 2020 Hotuba ya Seif imenitoa chozi, nashauri Rais Magufuli, Mwinyi na Maalim Seif wakutane wagonge glass kidogo

mimi nimefurahi alipowaondoa kwenye serikali wale watoto wa royal family.
  1. mohammed aboud
  2. haji omar kheri
  3. ali karume
  4. seif ali iddi
  5. n.k

kuna eneo fulani nimepita asubuhi ya leo nikaambiwa hii ni nyumba ya balozi seif
dah! nilipigwa na butwaa
Ulipita Mangapwani 😀 ukaona mjengo wake au? taja tu sehemu usiogope. Maana naskia jamaa uko Mangapwani kafukua makaburi auze kiwanja!
 
Kilichozungumzwa na Maalim ni muhimu, lakini hakuna jipya kitachofanyika zaidi ya yeye kulamba malupulupu na ving'ora Basi...Wazanzibar bado wana safari ndefu
 
Dunia ina viumbe wa ajabu sana yaan leo babu mandevu baada ya kucompromise amekutoa machozi,alivyokua analalamika watu wanakufa haikukutoa machozi?Dah hii nchi ya Lumumba ni kinyonga asiyekwepo duniani kwingine
 
Huyo ni kuku wenu hakuna haja ya manati
 
tunachotaka wazanzibari ni nchi yenye mamlaka kamili sio kupangiwa dodoma.

Hizo ajira zikitoka uwe na kad ya chama tawala kwanza afu ndio utizamwe kama ww ni muunguja au mpemba.

Nimeona kuwa kuna taasisi zinahamishiwa dodoma, sijaelewa mantiki ya hili suala.

Yaani mtu ata kama umewekwa as a puppet, have some respect for yourself, vyeo vinakwisha duniani ukifa huendi nacho!
 
Hawa wazee bwana huwa mpaka leo siamini Raila na Uhuru wanakula meza moja
 
Wewe kweli kichaa. Usitokwe na machozi walivyouawa watu Zanzibar kwa sababu ya uchaguzi aje kukutoa machozi Maalim!? Hao waliouawa wanafufuliwa kutokana na hayo makubaliano yao!? Maumivu ya walioumizwa yanaponywa!? Muwadhulumu watu kisha mjifanye mnataka kunywa nao kahawa, ninyi si wendawazimu tu.
 
TunduLissu aliongea nini baada kufika Belgium? alimtaka Magufuli aunde serikali itakayoleta umoja kwa Watanzania., kwa msingi wa maneno haya ni kwamba amemtambua kama ni Rais sasa Je. - huu nao ulikuwa unafiki kwa watanganyika? Ukiongea unafiki kwanza ongea wa Tundu Lissu kuwatelekeza watanzania waliokuwa na matumaini naye akakimbia siku 2 baada kutangazwa Magu akidai eti kapigiwa sim na mtu atakayemuua
 
Hivi unaingia muafaka na mwenzako kila kikifika kipindi cha uchaguzi anakugeuka, anauwa wanachama wako, anaiba kura.
 
Hiyo hotuba ni mjarabu na sawia kwa muda tuliopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…