Hotuba ya Tundu Lisu ni nzuri sana ila wamekosea timing. Alipaswa aanze na nini CHADEMA inatamani kuifanyia nchi hii ikishinda Uchaguzi!

Hotuba yake ya kwanza alitakiwa ahutubie wana Chadema sio taifa wala nini?

Chadema nchi nzima walikuwa wakimsubiri ahutubie kama mwenyekiti mpya ndani ya Chadema ana waza nini kuhusu Chadema na maono yake nini kupeleka Chadema from point A to B nk na mambo ya after uchaguzi nini ni nini?

Lakini kwa kwa kuwa hana political scientists wa kumshauri anategemea kichwa chake tu ndio kikamtumtuma ahutubie taifa
Hotuba yake kifupi ilikuwa irrelevant

Chadema kiko changamoto kibao za after election mtu anakimbilia kuhutubia taifa ??????
Lisu siasa hajui

Unahutubia taifa wakati ndani ya chama kunawaka moto?
 
Halafu kuna jambo Mwenyekiti anatakiwa kuachana nalo kabisa ingawa hawezi kulisahau, hili la risasi za Magufuli!

Linampunguzia credit sana kwa kanda ya ziwa bila yeye kufahamu.

Lilishapita hilo jambo aliache, hasimu wake hayupo ashakufa.

Akiendelea kutoa kauli za bezo kwa Magufuli, anamaanisha kuwatukana sukuma gang na watu wote waliompenda na kumuunga mkono.

Asidhani chuki zake atawavisha wote waliompenda Magufuli kisha wageuke na kumpenda yeye na wamchukie marehemu, hilo haliwezekani, sana sana atajishushia tuu uungwaji mkono.
 
Lazima tujue matamanio na agenda ya wananchi sio Chadema kushinda uchuguzi,
Bali nini Chadema itawapa baada ya uchaguzi

Matamanio aliyoelezea mkiti kushinda uchaguzi ni kipaumbele Cha Viongozi na wagombea wao maana ndo wanufaika wa moja kwa moja na Ushindi wa uchaguzi
 
Hakuna cha kukosea hapo ujumbe umefika vizuri kabisa.
 
Inshu sio kushinda uchaguzi, inshu hapa ni kutetea haki za watz.
Kurejesha mamlaka ya serikali kwa wananchi wenyewe kwa kushiriki kuchagua viongozi kwa uhuru na kwa haki.
Mamlaka lazima yatoke kwa wananchi wenyewe. Haijalishi nani atashinda chaguzi, cha msingi ashinde kwa haki.
 
Ahasante mkuu kwa kuliona hili
Ni moja ya Eneo Lisu ankwama Sana
Kuelezea Kila wakati maumivu yake ,

Kuna kundi linaogopa kumuunga mkono kwa kuwa linaona jamaa bado ana hasira ya kuja kulipiza kisasi
Nelson Mandela aliteseka miaka 27 lakini alikuja kushirikiana na watesi wake kujenga nchi
 
Kwani hiyo agenda ni Leo Chadema wameanza kuelezea wananchi ? Kwanini hawapati uungwaji mkono wa wananchi

Baada ya uchaguzi 2020 Lisu aliitisha maandamano nchi nzima kudai hiyo haki , kwanini hakupata uungwaji wa wananchi hata elfu moja kuandamana

Watanzania ni Aina ya wananchi wenye matamanio na agenda tofauti Sana na wananchi wa nchi zingine

Lazima ujifunze kwenda nao ili upate uungwaji mkono wao sio watu wavurugu Sana au maono makubwa Sana

Na hapa ndipo Ccm inapata Credit
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…