Nimemkubali warioba... big up sana...
Kijana kama bd hujamwelewa huyu mzee, bs hauko sawa kabisaaa,
Warioba hata Ukifa ...leo you are a NATIONAL HERO...
Naona kuna hatihati ya muungano kuelekea kubaya baada ya hotuba hii ya jaji warioba
Wadau, naamini mmeamka salama na akili zimetulia baada ya yale yaliyotokea jana.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum ambayo ameyatoa jana usiku, ni kwamba Bunge litaendelea na kikao chake leo saa tatu kamili asubuhi. Kwamba, baada ya dua, wabunge ambao walikuwa hawajaapa watakula kiapo. Baada ya kiapo hicho ndipo Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba atakapowasilisha Rasimu ya Katiba. Na kwa mujibu wa makubaliano waliyofikia, ni kwamba Warioba ataongea hadi atakapomaliza hotuba yake.
Nami kama kawaida kwa kushirikiana na wadau wenzangu akinina Skype, MaishaPesa, Simiyu Yetu, Deo Corleone, kbm, Mkuu ya Kaya na wengine tutaendelea kuwaletea yatakayojiri. Hadi wakati huo, Stay Connceted.
-================================================================
UPDATES
Mwenyekiti anaeleza kilichotokea jana. Kwamba baada ya kutokea kile kilichotokea, ni kwamba waliitisha kamati ya mashauriano. Katika kikao hicho wamekubaliana mambo yafuatayo.
*Kwamba baada ya kiapo watampokea Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti
*kwamba Warioba atahutubia kuanzia saa tatu na nusu hadi atakapomaliza
*semina zilizokuwa na utata zimefutwa badala yake semina ya kanuni itafanyika leo jioni na kesho
*Siku ya Alhamisi kutakuwa na semina itakayoongozwa na Wakenya.
*Semina juu ya historia ya Tanzania Bara, Zanzibar na Muungano imefutwa kwa vile kwa kadri utakavyoteua watakaoendesha semina hiyo, hawataonekana kama wamesimama kati kati
*Siku ya Ijumaa asubuhi, Mwenyekiti atatangaza Kamati 12 za Bunge Maalum
*Siku ya Ijumaa saa 10 jioni, Rais atakuja kulizindua Bunge
==================================================================
UPDATES
Jaji Joseph Sinde warioba ameanza kuhutubia bunge mnamo saa tatu na nusu. Katika hotuba yake amepitia sehemu zote za Rasimu ya Katiba. Masuala muhimu aliyoeleza ni kama ifuatavyo
Baada ya hayo na mengine, akiwa amewasilisha hotuba yake kwa dakika 85, Jaji Warioba alipumzika kwa dakika tatu. Na baada ya hapo anazungumzia muundo wa Muungano. Kwamba muundo uliopendekezwa ni wa Serikali tatu. Warioba anasema kuwa wamefanya utafiti juu ya muungano wetu na utafiti huo umeibua malalamiko kadhaa kwa pande zote za muungano. Ni kutokana na malalamiko hayo ndipo walipofikia uamuzi wa kupendekeza muundo wa serikali tatu
- Mihimili ya dola itaendelea kuwa serikali, mahakama na Bunge
- kuhusu Serikali, Rasimu inapendekeza kuwa matokeo ya Rais yanaweza kupingwa mahakamani na mgombea urais na si mwingine.
- madaraka ya Rais yamepunguzwa hasa kwenye suala la uteuzi
- Mawaziri hawatatokana na wabunge
- Rais hatakuwa sehemu ya Bunge
- Kuhusu Bunge, ukomo wa wabunge ni awamu tatu ya miaka 5
- Spika na naibu Spika hatatokana na Wabunge
- Warioba pia kazungumza juu ya Uraia na amesema kuwa uraia ni wa aina mbili nao ni wa kuzaliwa na wa kujiandikisha. Pia imeelezwa kuwa hakuna uraia wa nchi mbili
upuuzi mtupu