Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Baada ya wasilisho la Warioba uzalendo wangu unarudi polepole. Mungu ibariki Tanganyika, Mungu ibariki Zanzibar, Mungu mbariki Warioba mwangaza wetu kwenye kiza kinene.
 
Warioba na tume yake wanastahili pongezi hasa kwenye serekali 3.Simuelewi kwenye uraia mmoja wakati nchi ni 2.pia raia wa kila upande waweze kutumia huduma sawa wakati uchangiaji si sawa?unyonyaji wa Tanganyika!
 
Hata hivyo sita kaona ccm wanakizunguzungu akawaokoa semina isifanyike kumi na moja ili wakapigwe upepo kidogo wangeweza zimia kwa nondo za jaji
 

STOP TRIBALISM!...Usimhukumu kama Masai, mhukumu Kama OLESENDEKA..
 
75% ya ma ccm leo wamepata somo, na hii soft copy iwe audio au video itumike kuwaelimisha watu,hata yule baharia wa mtera dam naona nae kaelewa
 
Ajabu kabisa..katika maelezo ya Jaji Warioba..michango ya Taasisi nyeti nchi hii...ZIMEPENDEKEZA mfumo wa Serikali 3...ingawa sio wa moja kwa moja...Mfano...Ofis ya Wazir Mkuu imetaka kuwepo na Mawazir Wakuu 3...na Raisi Mmoja tu...manake hawa wawili...kila mmoja ata deal na mambo ya Upande wake....alaf huyu wa katikati ndo ata deal na ya muungano...manake ni nini..ni zile zile serikali 3 katika version tofaut.......wameumbuka hawa
 
Waasisi walituachia Nchi mbili na serikali moja-Warioba



Hapana hajasema hivyo amesema waasisi walituachia nchi moja serikali mbili, sasa tuna nchi mbili serikali mbili. Kwa hiyo wanaotetea muungano huu uliopo kwa kisingizio cha kuwaenzi wasisi hawataki kuelewa kwamba huu sio muungano waliouacha. Hiki ni kitu kingine kabida ambacho hakieleweki. Lisu alikiita kiini macho. CCM wamechokaje. Nimwemwona Werema, pinda, Na wenzao wmeshika tama wakishusha pumzi kwa nguvu tu.
 
Shikamoo JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA wewe umemaliza wacha tuone wao wanaamua nini.
 
serikali ya ccm na maccm tu ndio wamefumba macho!!!ccm ni chama hatari sana
 
Mowapo ya hoja za gwiji wa kujenga hoja kama alivyomtunuka mwanzisha uzi ni kuwa 'Serikali ya Zanzibarimetunga Katiba yake inayopingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania'. Anaendelea kujenga hoja kuwa ndani ya Katiba ya Zanzibar, Zanzibar ni nchi, ina mipaka yake, bendera na wimbo.' Kwa maneno rahisi anasema ' Zanzibar imevunja Katiba ya Jamhuri wa Tanzania' Suluhisho la kuvunja Katiba kwa mujibu wa gwiji wa kujenga hoja ni kuhalalisha kuvunja kwa Katiba kwa kuandika Katiba Mpya inayoridhia uvunjivu wa Katiba. Ni tangu lini mkosaji akikosea tunaifuta sheria ili kumwondolea mkosaji kosa.
Mimi sio mwansheria, lakini najua kuwa sheria inabaki kuwa sheria mpaka itakatungwa sheria inayoibatilisha. Ndiyo hata sheria zilizokwisha ainishwa na tume ya Jaji Francis Nyarali kuwa ni sheria mbaya mpaka leo zinatumika kwa kuwa hazijaondolewa vitabuni. Kutunga Katiba juu ya Katiba ilikuwa ni kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama huo ndiyo ugwiji wa kujenga hoja kinzani/ tata basi na iwe hivyo.
Mimi binafsi ningemwita Warioba mtu mwoga wa kuwambia ukweli Wazanzibar kuwa wametunga katiba inayokiuka Katiba mama. Sheria mahali fulani tu au ya kimila kama inakinzana na sheria ya nchi sheria hiyo huwa batili au batilifu. Japokuwa Zanzibar ni sehemu ya Muungano na Tanzania bara pia lakini nchi hizi mbili zikitunga sheria inakinzana na Katiba ya Jamhuri waMuungano, sheria hiyo inapaswa kuwa batili.
Warioba ni mwoga kumwambia JK KUWA NI RAIS DHAIFU kwa kufumbia macho Zanzibar ilipokuwa inatunga Katiba inayokinzana na Katiba kuu. JK aliapa kuilinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini hajailinda na bado yupo Ikulu.
Ningalikuwa mimi ningalisema Zanzibar iondoe katika Katiba yake vingele vinavyokiuka Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Bila kufanya hivyo hakuna maridhiano. Uwoga unaubatizaje kwa jina UGWIJI?
 
STOP TRIBALISM!...Usimhukumu kama Masai, mhukumu Kama OLESENDEKA..

Binafsi sina bifu na Mmasai yeyote, lakini namchukia OLE SENDEKA kwa kujifanya mwenye hii nchi peke yake kana kwamba wengine ni kenge tu, ajifunze kuwa nguvu ya demokrasia inataka wengi wape, siyo kubaki na misimamo ya kijingakijinga.

Sitakuwa na sababu ya kupiga kura ya maoni endapo katiba hii itatambua serikali 3, kama ni serikali 2 ni lazima saa 12 asubuhi nitakuwa kwenye kituo cha kupigia kura kuikataa hiyo katiba. Wapenda maendeleo na demokrasia ya kweli bila kujali chama, utanganyika wala uzanzibari tuungane katika hili, tumechoka kuendeshwaendeshwa na kikundi cha watu wachache.
 

mkuu ccm ni chama hatari sana
 

serikali mbili zitanifanya nikapige kura ya hapana
 
Kijiweni tunaapa kulinda Tanganyika na Zanzibar.

Tehe tehe tehe, mzee mzima Sitta na maccm wenzake wameumbuka> Ina maana sitta hakujua kwamba kazi waliyofanya tume ilihitaji muda mrefu kuiwasilisha na kutolea ufafanuzi? Je tukisema mlikuwa na ajenda ya siri nyie maccm mtakataa? Saa moja au mawili eti kuwasilisha rasimu, lengo lenu lilikuwa nini?
 
mkuu ccm ni chama hatari sana

Inashangaza sana...inaonekana wanachokihubiri huku nje sio WANACHOKITAKA...nimefurahi Warioba kasema wazi wazi walichopendekeza wao kwa Tume...walipokua wamemkalia kooni KIFICHO kumbe ndani yake karibia Taasisi zote zimekuja na kitu kile kile..cha 3-0 ha ha haaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…