Tume ya Katiba
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,896
- 1,862
Jaji warioba he good in making analysis and making clarification clearlly
Ulitaka kusema nini wewe junior Member? Tumia kiswahili kama hii lugha ya malikia inakushinda
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jaji warioba he good in making analysis and making clarification clearlly
akikutumia nami nitumie kupitia email hii skypejf@gmail.com
Warioba na tume yake wanastahili pongezi hasa kwenye serekali 3.Simuelewi kwenye uraia mmoja wakati nchi ni 2.pia raia wa kila upande waweze kutumia huduma sawa wakati uchangiaji si sawa?unyonyaji wa Tanganyika!Hio ndio Nguvu ya hoja toka kwa jaji msomi
Na mzalendo wa nchi hii Joseph Sinde Warioba
Waliokuwa wanataka elimu ya serikali tatu Leo
Wamepata shule itakayodumu kwa vizazi vyote
Sio ile elimu uchwara ya ole sendeka ya Jana
Star tv . Angepewa na yeye Leo asalimie wajumbe
Hovyo sana huyu mzee wa kimasai
warioba ni jembe, huyo sendeka hana lolote kazi kupayukapayuka tuu, anafikiri yuko simanjiro na wamasai wenzake,nimeangalia sana hili bunge kuanzia mwanzo kupitisha kanuni sendeka alikuwa msumbufu sana ,tungekuwa na kiranja angemwandika kwenye orodha ya wasumbufu akapewa adhabu.yeye yuko kichama zaidi na siyo ki utaifa.
Waasisi walituachia Nchi mbili na serikali moja-Warioba
Kila kitu kinapangwa na kuwekwa kutegemeana na hali iliyopo. Ninyi wote nitawasifu kama mutaleta hoja inayoeleweka. Hamtaki Serikali 3, munasema haiwezekani kwa nini? Kenya kuna serikali za majimbo, munajuwa kuna majimbo mangapi na serikali ngapi? Amerika kuna serikali za majimbo mangapi? Nahisi tatizo lenu ni neno serikali au neno Rais. Munakuwa kama Idd Amini aliyezuiya mtu yeyote kujiita Rais hata kama ni wa chama cha waalimu.
Semeni hizo mbili ziweje? Mbona hamusemi moja? Semeni moja maana kama nchi moja serikali 3 ni tatizo kwenu, hata nchi moja serikali mbili ni tatizo! Tuondoe ujinga tusiwe watu tunaoweza kukumbuka tuliyoyasikia tu bila hata nafasi ya kujiuliza ya kwetu. Wengine mumekimbilia suala la gharama, huyu ambaye ni waziri mkuu mstaafu amewaonyesha jinsi serikali mbili zinavyoendeshwa kwa gharama kubwa kuliko hata hizo 3.
Waziri mkuu Pinda ni waziri mkuu wa serikali ipi? Z'bar wanamtambuwa? Serikali yake ni ipi?
Kuna kundi la Wa Zenj ambao wao wanapenda wawe na serikali lakini hawataki kuiendesha wenyewe. Wanataka serikali yao iendeshwe na bara, hiyo NO! kwa kuwa wana katiba yao, bendera yao, serikali yao lazima waiendeshe, kama hawawezi, wakope bara na walipe mikopo! Mambo ya kudeka hatutaki kabisa! Ukideka unaachiwa utembee mwenyewe, kama ni kilio, we lia baadaye ukinyamaza utakuwa na akili.
Bara wote hatuwezi kuwa kama akina Nape. Huyo Sitta naye analazimisha watu kufundishwa mambo ya muunganao eti na wale wanaoujua muungano. Akina nani hao walioujua muungano kwa miaka 50 bila kuwaeleza wengine, halafu leo ndo wanakuja kujidai kuwaeleza wengine.
Shit and stupid!
STOP TRIBALISM!...Usimhukumu kama Masai, mhukumu Kama OLESENDEKA..
Ajabu kabisa..katika maelezo ya Jaji Warioba..michango ya Taasisi nyeti nchi hii...ZIMEPENDEKEZA mfumo wa Serikali 3...ingawa sio wa moja kwa moja...Mfano...Ofis ya Wazir Mkuu imetaka kuwepo na Mawazir Wakuu 3...na Raisi Mmoja tu...manake hawa wawili...kila mmoja ata deal na mambo ya Upande wake....alaf huyu wa katikati ndo ata deal na ya muungano...manake ni nini..ni zile zile serikali 3 katika version tofaut.......wameumbuka hawa
Binafsi sina bifu na Mmasai yeyote, lakini namchukia OLE SENDEKA kwa kujifanya mwenye hii nchi peke yake kana kwamba wengine ni kenge tu, ajifunze kuwa nguvu ya demokrasia inataka wengi wape, siyo kubaki na misimamo ya kijingakijinga.
Sitakuwa na sababu ya kupiga kura ya maoni endapo katiba hii itatambua serikali 3, kama ni serikali 2 ni lazima saa 12 asubuhi nitakuwa kwenye kituo cha kupigia kura kuikataa hiyo katiba. Wapenda maendeleo na demokrasia ya kweli bila kujali chama, utanganyika wala uzanzibari tuungane katika hili, tumechoka kuendeshwaendeshwa na kikundi cha watu wachache.
Sasa jana walikataa nini na leo wanakubali nini!!
Kijiweni tunaapa kulinda Tanganyika na Zanzibar.
mkuu ccm ni chama hatari sana