Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Naunga mkono hoja mkuu
 
Mh warioba amesema wamepokea mapendekezo ya muundo wa serikali 3 yametolewa hata na taasisi na idara za serikali ambazo katika maoni yao waliyo wasilisha kwa tume kimaandishi yamependekeza 3gvnt,miongoni mwa taasisi na idara hizo ni ofice ya waziri mkuu,ofice ya makamu wa rais,baraza la wawakilishi znz na bunge la jamhuri ya muungano wote wametaka uwepo wa serikali ya tanganyika,zanzibar na ya muungano,hivyo wale ccm wanaopinga mfumo wa serikali 3 wanapata wapi kiburi hicho?
 
i believe umeongea point ya maana hapa hili bunge bado sijaliamini iy is another rubber stamp ya ccm kupitisha kitu wqnachotaka
 
Labda nisaidie kidogo kuhusu utafiti wa maoni na takwimu zake. Ni hivi. Ni kweli kujua maoni ya Watanzania huhitaji kuwauliza wote M 45. Najua kwa uhakika kuwa sampuli ya kisayansi kwa Tanzania haijavuka watu 3000 wa kuhojiwa. Lakini msisitizo hapa uko ktk sayansi. Kanuni mojawapo ya utafiti wa maoni kisayansi ni kuwa wanaohojiwa hawafuatwi kwa kuwapenda, au kudhani wanajua. Na hawatakiwi kujileta kwa wakusanya maoni. Anayehojiwa ni ambaye tarakimu ya random numbers imemwangukia ili kila mtu awe na uwezekano sawa wa kuhojiwa. Wakijileta watakuwa wamejihamasisha kwa msimamo mmoja unaofanana, kwa hiyo mawazo hayatakuwa wakilishi tena. Kosa hili limefanywa na Tume zote za maoni ya Katiba. Ile Kamati ya Kisanga ndiyo ilitia fora kwenye kosa hili, ila waliojihamasisha nakujileta walikuwa wapenda serikali mbili, ambao asilimia yao ilivuka 90 , hadi ikawa kichekesho kwa Kamati hiyo kupendekeza serlkali tatu dhidi ya aslimia hiyo. Tume ya Warioba imefanya kosa hilo hilo kisayansi, ila waliohamasika ni wa serikali tatu. Tume hii iliambiwa hili, ikapuuza. Ndiyo sababu takwimu zake hazina uhalali mkubwa. Ukosoaji wa asilimia hizo kwa kutumia takwimu za Tume yenyewe, kama walivyofanya wasomi fulani, ni sahihi, lakini kosa kubwa ni msingi wa ukusanyaji maoni. Hii haina maana kuwa takwimu za Tume hazifai kabisa, maana hata wanaotaka yeyote anayejisikia atoe maoni kwa jambo fulani kwa simu au barua pepe hupata matumizi fulani ya takwimu zake. Lakini uzito wa ushahidi wa takwimu hizo hupungua sana. Ndiyo sababu Tume ya Warioba haiwezi kuhalalisha serikali 3 kwa takwimu zake za maoni tu, au kuzuia mabadiliko ya rasimu yake kwa ku invoke ukuu wa maoni ya wananchi
 
Hotuba ya Warioba itaishi Milele,haina unafiki hata Kidogo,imeeleza ukweli usiopendwa
 
tena hizo dvd zitufikie na ss huku kalenga
 
Mkuu unaweza ukawa sahihi, ila mimi nipo hapo kwenye numbers....Unafikiri ni nini kingefanywa ili kupata uwakilishi sawia/sahihi wa wananchi? Je kila mmoja wetu alitakiwa atoe maoni yake? If yes, katika muundo gani/upi rahisi? Manake hata ukirudi kwenye uchaguzi mkuu, tunakuta kuwa ni watu milioni 5 tu ndio waliopiga kura kumchagua rais! Sasa kwenye population ya watu 40m+, kweli raisi achaguliwaye ndiye kipenzi chetu wote?

Siko katika kupingana na hoja yako, ila najaribu kuangalia uwakilishi wetu wote kwenye mchakato tu. Je, tumeikimbiza sana ili hali tulihitaji muda zaidi ili angalau asilimia 90% ya wananchi itoe maoni yake?
 
Unazijua njia zote ambazo tume ilitumia kukusanya maoni?

Hata wale waliopo nje ya nchi walikuwa na nafasi ya kufanya hivyo:

Utaona kuwa kila mwananchi alikuwa huru kupeleka maoni kwenye tume kwa kutumia njia mojawapo kati ya zilizokuwepo. Nakumbuka hili lilipigiwa kelele sana, watu tu wazito sana kushiriki mambo ya msingi ya taifa letu lakini sisi ndio wa mwanzo kulalalama. Sitashangaa kama wewe ni mmoja kati ya wananchi wengi ambao waliona sio wajibu wao kupeleka maoni yao kwa tume na hukupeleka maoni yako! Tume ilikuwa haina mamalaka ya kuwalazimisha watu kutoa maoni.
 
Labda nisaidie kidogo kuhusu utafiti wa maoni na takwimu zake. Ni hivi. Ni kweli kujua maoni ya Watanzania huhitaji kuwauliza wote M 45. Najua kwa uhakika kuwa sampuli ya kisayansi kwa Tanzania haijavuka watu 3000 wa kuhojiwa. Lakini msisitizo hapa uko ktk sayansi. Kanuni mojawapo ya utafiti wa maoni kisayansi ni kuwa wanaohojiwa hawafuatwi kwa kuwapenda, au kudhani wanajua. Na hawatakiwi kujileta kwa wakusanya maoni. Anayehojiwa ni ambaye tarakimu ya random numbers imemwangukia ili kila mtu awe na uwezekano sawa wa kuhojiwa. Wakijileta watakuwa wamejihamasisha kwa msimamo mmoja unaofanana, kwa hiyo mawazo hayatakuwa wakilishi tena. Kosa hili limefanywa na Tume zote za maoni ya Katiba. Ile Kamati ya Kisanga ndiyo ilitia fora kwenye kosa hili, ila waliojihamasisha nakujileta walikuwa wapenda serikali mbili, ambao asilimia yao ilivuka 90 , hadi ikawa kichekesho kwa Kamati hiyo kupendekeza serlkali tatu dhidi ya aslimia hiyo. Tume ya Warioba imefanya kosa hilo hilo kisayansi, ila waliohamasika ni wa serikali tatu. Tume hii iliambiwa hili, ikapuuza. Ndiyo sababu takwimu zake hazina uhalali mkubwa. Ukosoaji wa asilimia hizo kwa kutumia takwimu za Tume yenyewe, kama walivyofanya wasomi fulani, ni sahihi, lakini kosa kubwa ni msingi wa ukusanyaji maoni. Hii haina maana kuwa takwimu za Tume hazifai kabisa, maana hata wanaotaka yeyote anayejisikia atoe maoni kwa jambo fulani kwa simu au barua pepe hupata matumizi fulani ya takwimu zake. Lakini uzito wa ushahidi wa takwimu hizo hupungua sana. Ndiyo sababu Tume ya Warioba haiwezi kuhalalisha serikali 3 kwa takwimu zake za maoni tu, au kuzuia mabadiliko ya rasimu yake kwa ku invoke ukuu wa maoni ya wananchi
 
Hotuba ya Warioba imegusa nyoyo za watanzania na kuumiza nyoyo za watu wenye fikra mgando.
 
Kama kuna mtu mwenye softcopy au audio atuwekee tudownload maana wengine hatukuifaidi.
 
Dina, nimelipenda jibu lako, pokea like yangu.
 
Nadhani kuwa jeshi letu la Navy litapanuliwa zaidi kwa sababu ya jukumu la ziada la kulinda mpaka baina ya Zanzibar na Tanganyika! Idara ya Uhamiaji itatakiwa kufanya kazi zake kwa makini sana kuhakikisha kuwa wapemba wote wanaondoka kwenye ardhi ya Tanganyika mara moja kwa vile terms zilizopwapa haki ya kuishia na kumiliki mali Tanganyika zitakuwa zimekwisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…