Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Kuwa kiongozi ( I mean Leader and true Leader) unahitaji kuwa na maono ambayo pengine wengine hawana au kufikiria. Ni swala la muda tu wanafiki wataadhirika, japo kuwa wanakamtaji kadogo wanakokashikiria (ignorance of the majority).
 
Nina mashaka juu ya gharama za serikali ya muungano. Hawa wazanzibari sijui kama watachangia. Pia sijajua kama gharama hizo zitakuwa sawa kwa sawa baina ya pande mbili hizi

Sawa kwa sawa vipi kaka? Warioba amelieleza hili vizuri sema tu umeshaamua kuweka pamba masikioni. Nchi washirika zitachangia kuendana na uwezo wao kiuchumi, ukubwa nchi na idadi ya watu. Sio sawa kwa sawa.
 
Akiwasilisha rasimu ya pili ya katiba bungeni na huku akishangiliwa kwa nguvu na wajumbe , Jaji Warioba amewajibu wale wote waliokuwa na hoja hafifu za kwamba Mwl Nyerere alitaka serikali mbili kwamba wakati huo kulikuwa na nchi moja yenye serikali mbili. Amesema baada ya marekebisho ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 yakaitambua Zanzibar kama nchi basi hakuna tena uharali wa serikali mbili. "Huwezi kuwa na muungano wa nchi mbili na serikali mbili aidha utakubali iwe moja au tatu".

Aliendelea kufafanua "haiwezekani mfano kusema mafuta na gesi ya Zanzibar yatabaki kuwa Zanzibar na mafuta na gesi ya bara yawe ya serikali ya Muungano......." Aliongeza "haiwezekani upande mmoja uwe na hadhi na mamlaka kamili na upande mwingine usiwe na mamlaka na hadhi kamili!

Tafakari!
 
Mkuu CHAZA

Nchi kwanza vyama baadae watanzania wengi wanataka serikali tatu hakuna haja ya kuwakatilia.

Kaka umenena vyema nchi kwanza vyama baadae wananchi ndicho wanachotaka wapewe
 
Last edited by a moderator:
Warioba alizidi nifurahisha alipowaambia maCCM kuwa ..sheria iliiwekea mipango TUME ILA HAKUNA ILIPOWAWEKEA WANANCHI MIPAKA NA HIVYO wakatafsiri kuwa wananchi walitakiwa waseme kila kitu kwa uhuru na hawakuwa na mamlaka ya kuwazuia. Hii ilikuwa mwima kwa maCCM waliopiga debe ktk vipindi vya dkk 45 na vingine kuwa tume iliweka maawzo yao wenyewe...JK atajilaumu sana kuwa hakuona hilo...tunaojua fikra za CCM n akukumbuka walichosema kwa fahari hata waliposhtuliwa kuwa wamepotoka..tulikuwa tunayaona maumivu makali sana kwa werema, na maccm yote.
 
hakika hayo ndo mawazo ya wananchi wengi na nafikiri na naamini kabisa kwa hoja hizo kabisa,warioba katema kweli tupu.serikali tatu ndo suluhisho za hizo problems za wazanzibar na watanganyika
 
Tunaofahamu suluhu ya muungano ni serikali moja, tuko pembeni tunaangalia watu wanabishania aina za muungano ambazo hazitaleta muungano wa kudumu na wenye tija.

Vyovyote itakavyokuwa, kitakachotutoa hapa ni ama serikali moja ama muungano usiwepo,... it is just a matter of time...tusubiri.
 
Warioba came and saw and most important understood humble Zanzibaris. Long live Warioba, Mungu ibariki Tangayika, Mungu ibariki Zanzibari.
 
wamesemaje jamani?? tupeni nondo...wanataka govt 3 au moja?
 
Vijana wenzangu tuwe macho sana na hawa wazee, hili swala la katiba tusiingie kichwakichwa matokeo ya serikali mbili au tatu yatalifaidisha kundi mojawapo ndani ya ccm na sio wewe wala ndugu yako, CCM imegawanyika mara mbili kuna wa serikali 2 na tatu kwa maslahi bnafsi ila wote ni marafiki na hawako tayari kuharibu chama wako pamoja, wanapambana kwa hoja jioni wanakula bata huku wakipeana tano. Cha msingi tuconcetrate na na maswala muhimu kwenye katiba yetu kama afya, miundombinu, elimu na malazi. katiba inasema nini juu ya haya, hata wao wakiamua nchi iongozwe na jaji mkuu au spika au jeshi hayo ni yao wanasiasa. Usifikiri Warioba,JK,Sitta,Lowassa +wana ccm kwa ujumla lao sio 1. chondechonde tuache mihemko kama wakenya sasa wanaandamana kila kukicha na watawala ni walewale wanabadilishana nyadhifa tu.:flypig:

karibu tujadili na kuelimishana kama vijana maana sisi ndo bado tuna safari ndefu kwa mstakabari wa nchi yetu.
 
Back
Top Bottom