Chadema Diaspora
JF-Expert Member
- Oct 25, 2010
- 480
- 644
Hotuba ya Warioba: Wabunge 9 wa Zanzibar watishia kujitoa CCM baada ya kikao cha usiku
Habari kutoka chanzo chetu cha kuaminika ni kuwa kulikuwa na kikao cha CCM siku ya Jumanne usiku baada ya hotuba ya jaji Warioba Bungeni. Kikao hiKi kiliisha saa nane za usiku bila kuwa na muafaka.
Agenda kubwa ya kikao ilikuwa kujaribu kuwalazimisha wabunge wa Zanzibar wakapitishe mswaada kwenye Bunge la Zanzibar kutengua kipengele ambacho kilipitishwa 2010 kuwa Zanzibar ni nchi. Agenda hii ilizua mabishano makali kati ya wabunge wa Zanzibar na viongozi wa Tanzania Bara. Viongozi wa Bara (CCM) walionekana kulaamu maamuzi yaliyo fanyika 2010 ya kuitambua Zanzibar kama nchi kikatiba na walikuwa wanalazimisha wabunge wa Zanzibar wakatoe kipengele hicho.
Ajenda hii ilipata pingamizi kali kutoka kwa wabunge wa Zanzibar ambapo wabunge tisa (9) wa Zanzibar waliahidi na wametishia kujitoa CCM endapo hili swala litaendelea kulazimishwa na kupitishwa.
Tutaendelea kuwahabarisha kuhusu hili kila tunapo pata updates kutoka kwenye intelegencia yetu ambayo tumefanikiwa kuipandikiza ndani ya kamati kuu ya CCM.
WE REPORT, YOU DECIDE