Hotuba ya Warioba: Wabunge 9 wa Zanzibar watishia kujitoa CCM baada ya kikao cha usiku

Hotuba ya Warioba: Wabunge 9 wa Zanzibar watishia kujitoa CCM baada ya kikao cha usiku

Haaaa finally wizi wa Tanganyika dhidi ya wazanzibar utapungua kuisha ni mpaka watengane
 
Vyema tukiwapata wabunge ishirini wa Zanzibar wenye msimamo kama huu muungano utavunjika na kutupatia Tanganyika yetu.
 
Mungu atasimamia yote na kutenda haki. Hao wanaong'ang'ania Serikali mbili wataumbuka muda si mrefu.
 
Itakuwa kitu cha ajabu kwa Zanzibar kuendelea kuwa nchi na watu bado watu wanataka serikali mbili. Hili ni la zege. Hivi katika muungano wa mtindo huo itakuwaje kama rais wa jamuhuri ya muungano, je kuna uwezekano akatoka Zanzibar? Ikiwa na maana wazanzibar wataongoza nchi yao na ya Tanzania bila kuwa na mtanganyika. Hili halitowezekana. Bunge la katiba lilazimishe Zanzibar isiwe nchi vinginevyo serikali tatu hazikwepeki. Mimi napendekeza kama kweli serikali mbili zinahitajika futa kwanza nchi pia katengeneze system ambayo kutakuwa na makamu wawili wa rais wa JMT. makamu wa kwanza awe pia rais wa either Zanzibar auTanganyika kutegemea rais anatoka nchi ipi. Vinginevyo hatuna jinsi.
 
Kila mtanzania mpenda maendeleo na tanganyikakwa dhehebu lake la dini tufunge na kuomba ili mungu ayafunge haya mapenda madaraka ma ccm yashindwe na yalegee kabisa
 
Tena waliitambua wenyewe viongozi sisi waTanganyika wala hatukuhusishwa. kwa hiyo Zanzibar ni nchi sasa inaungana nannchi ipi ile kufanya muungano wa nchi mbili? Zikiungana nchi mbili si aidha inakuwa nchi moja na katiba moja au nchi mbili na katiba moja ya muungano. Au nchi mbili kila moja na katiba yake na katiba nyingine ya muungano!

Ushauri wangu ni kwamba tunakimbilia wapi au nini katika kupata katiba mpya? Muda wa kutosha utolewe ili kila mwananchi apate fursa ya kujua nini kinaendelea na maridhiano ya kila namna yafanyike halafu ndio wabung wakae waendelee na utungaji au upitishaji wa rasimu ya katiba.

Namshauri Rais avunje hili bunge atoe muda wa kutosha kusawazisha mambo hata kama ni kutunga katiba ya Tanganyika a.k.a Tanzania bara.
 
hii mibunge ya ccm kutoka tanganyika inatia aibu sana ! Badala ya kupigania nchi yao inahangaika na visiwa vidogooo!

Kaka sio visiwa vidogo Ni visiwa vizitto kihistoria....Chi za mwazo barani Afrika.....Misri......Ethiopia na Zanzibar...ukweli ndo huo....uliza ipi ilikuwapo mwanzo baina Zanzibar na Tanganyika.....Kenya au Uganda...
 
Ebu yupige kura sisi
members wa jf, niwangapi wanaunga mkono muungano waserikali tatu
nawangapi serikali mbili

Nenda kwenye jukwaa la KATIBA kuna poll pale wamei stick ya kuhusu kupiga kula muundo wa muungano habari ni kwamba mpaka sasa serikali tatu inaongoza ikifuatiwa na serikali moja
 
Wakulaumiwa ni Mtakatifu Kambarage Julius Nyerere ndie alieiua Tanganyika.

ni ukweli ambao wanaomwona nyerere alikuwa mungumtu hawapo tayari kuusikia..Nyerere aliiua Tanganyika. Period
 
Back
Top Bottom