Itakuwa kitu cha ajabu kwa Zanzibar kuendelea kuwa nchi na watu bado watu wanataka serikali mbili. Hili ni la zege. Hivi katika muungano wa mtindo huo itakuwaje kama rais wa jamuhuri ya muungano, je kuna uwezekano akatoka Zanzibar? Ikiwa na maana wazanzibar wataongoza nchi yao na ya Tanzania bila kuwa na mtanganyika. Hili halitowezekana. Bunge la katiba lilazimishe Zanzibar isiwe nchi vinginevyo serikali tatu hazikwepeki. Mimi napendekeza kama kweli serikali mbili zinahitajika futa kwanza nchi pia katengeneze system ambayo kutakuwa na makamu wawili wa rais wa JMT. makamu wa kwanza awe pia rais wa either Zanzibar auTanganyika kutegemea rais anatoka nchi ipi. Vinginevyo hatuna jinsi.