...ndio maana mara zote nawausia watu wachane na kauli kama, "huyo mume/mke hakufai! muache!"... wanandoa ni sawa na siri ya mtungi!
maisha ya ndoa kama safari baharini, kuna mawimbi ya hapa na pale, dhoruba kali saa nyingine, na kuna kipindi shwariiiii,...
hapo nyuma nilitoa mfano wa 'siku mbaya', ambayo kuanzia kumekucha mpaka machweo ni kibano tu!, lakini kama mmoja ataamua kujishusha, aaaah, haichukui hata muda utasikia, sasa nawe unanuna nuna nini... na vicheko vinaanza upya, mikumbatiano na mabusu kama sio nyie...
udugu wa shuka huo!
kwi kwi kwi kwii, umenifurahisha sana. Mimi kusema ukweli huwa tukigombana sometime nashukuru Mungu kwani baada ya hapo najua mambo yanakuwa mazuri sana na inapita kipindi kirefu bila mikwaruzo, halafu unapatikana muda mzuri wa kutoa madukuduku yako yooooooooote na vinyongo vyooote. Baadaye sana tena mnazoeana na kuanza kufanyiana visa hadi siku zogo litokee.