chawa wa mama
JF-Expert Member
- Jun 8, 2020
- 292
- 1,084
Waarabu waliwakusanya kwa kuwakamata waafrika na kuwauza Amerika na Ulaya., Biashara ile imeisha, tunaona sasa wamebadili mtindo wa utumwa, mnachukua watoto wa masikini vijijini na kuwafanyia kazi za ndani kwa ujira mdogo.
Ni ukatili tu, wengi wa hao watumwa wenu ambao mnawaita wadada wa kazi wanapitia magumu sana, wengi wao walikatiza ndoto zao za elimu kwa ajili ya umaskini, hawana namna, mnawafanyisha kazi kama punda, na wengine ni under 18.
Msiniambie habari za favour kuwa Kuna wanaosomeshwa hata kuishi nao vizuri kama ndugu, ni kweli ila ni wachache sana, na hata wakati wa utawala wa utumwa kuna watumwa walipewa favour kama hizo tu.
Najua utumwa huu hausemwi kwa kuwakamata ni sisi kwa sisi na tunaona sawa,.
Najua leo mapovu yatakuja hadi niloe, ruksa!!!!