Maslahi ya mtoto vs. Unyanyapaa.
Nadhani hapo ni wewe kupima, kwa kawaida mtoto hawezi kuambukizwa simply kwa kulelewa na mtu mwenye maambukizi. Ndio maana hata mama mwenye maambukizi anaweza kuzaa na kulea mtoto asiye na maambukizi. Lakini kuna elimu inayoambatana na namna ya mama kumkinga mtoto wake. Kama dada hana elimu yoyote basi anaweza kumwambukiza hata kwa bahati mbaya, ukizingatia mtoto mchanga ni rahisi kuambukizwa magonjwa.
Lakini kuna uwezekano pia wa dada kumwambukiza kwa makusudi mtoto, hii inategemea na nyie mnavyoishi naye hapo nyumbani. Tumeshaona akina dada wa kazi wakiwafanyia vitendo vya kikatili watoto, kwa hiyo sio ajabu akiamua kumwambukiza kwa makusudi kama njia ya kulipa kisasi kwenu.
Mwisho wa siku maamuzi ni yako. Nenda kampime mtoto. Kama yupo salama, basi tafakari, je dada wa kazi anaweza kumwambukiza kwa makusudi?? Je kuna mazingira ambayo mtoto anaweza kuambukizwa kwa bahati mbaya? Kama majibu ni hapana basi maisha yaendelee.
Kama mtoto tayari anamaambukizi jizuie usifanye maamuzi utakayojutia baadae.