Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kuanzia majuzi wanamgambo wa Houth wameanza kuzipa onyo meli zinazokatiza maeneo yao kabla ya kuzirushia makomboa.
Wakitumia meli yao ya wanamaji wiki iliyopita walimuonya kapteni wa meli ya True Confidence kwamba alikuwa akikatisha njia ambayo si salama kwake.
Kwa mara nyengine akaelekezwa apindishe meli yake kutoka uwelekea aliofuata.Na ilipokuwa dhahiri kapteni huyo wa meli kubwa sana ya mizigo akikaidi onyo la Houth ndipo iliporushiwa kombora na kusababisha vifo vya mabaharia 3 ikiicha meli hiyo kwenye hali mbaya.
Mbinu nyengine za Houth zinazotumika na kuanza kuleta mashaka iwapo wako peke yao au wameanza kupata ushiriikiano kutoka mataifa hasimu na Marekani mbali na Iran, ni kushambulia kwa kutumia kiwingu cha droni kama vile inavyofanyika kule Ukraine.
Hapo jana Houth walirusha droni 37 kwa mpigo kulenga meli za kivita za Marekani na washirika wake pamoja na meli moja ya kibiashara iliyokuwa ikipita eneo hilo.
Kati ya droni hizo 28 zilifanikiwa kudondoshwa kutoka mifumo ya ulinzi ya meli za washirika. Zilizobaki haikutajwa kuwa zilifanikiwa kufikia shabaha zao au zilidondoka zenyewe baharini.
Mambo yakiwa kama hivyo katika bahari nyekundu, kule Gaza jeshi la Israel limekiri kumpoteza komandoo wake wa cheo cha juu kwenye mapiganona Hamas kusini mwa jimbo hilo.