Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Athari ya vita vya Gaza inazidi kuenea duniani kwa vikundi vidogo kujiamini kupambana na wababe wa dunia.
Msemaji wa wanamgambo wa Houth ,Yahya Saree amesema kikosi chake kimoja kimefanikiwa kupiga meli ya kubebebea ndege (Aircraft carrier) iitwayo Eisenhower.
Kwa maelezo ya msemaji huyo kombora lililoelekezwa kwenye meli hiyo lilfanikiwa kupiga moja kwa moja kwenye meli hiyo kubwa ya kijeshi ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikivinjari kwenye bahari inayopakana na Yemen kutoa doria kwa meli za kibiashara zinazopita eneo hilo.
Hapo jana Marekani na Uiengereza zilipandwa na hasira kwa mara nyengine na kurudi kushambulia maeneo ya Yemen baada ya Houth kufanikiwa kutungua drone ya 6 aina ya reaper ambayo ni ya ghali sana inayotumiwa na jeshi la Marekani kufanyia upelelezi kwenye maeneo ya Yemen na mengine yenye vita.
Katika mashambulio hayo ya Marekani na mshirika wake jumla ya watu 16 walikufa maeneo mbali mbali ya Yemen na ndipo Houth nao wakaamua kuipiga meli hiyo.Jeshi la Marekani bado halijakiri kufanikiwa kwa kombora la Houth kutua kwenye meli hiyo ambayo yenyewe ina mifumo ya kisasa ya kujilnda dhidi ya mashambulizi mfano wa shambulio la Houth.
Kujiamini kwa Houth kushambulia meli ya kivita inayosifika ya Marekani ni dalili ya kuwa vita vya Gaza ambavyo havikuweza kusimamishwa japo ingewezekana kutaifanya dunia iwe ni uwanja wa fujo zaidi kwani makundi mengi yatajiamini kupambana na wababe wa dunia waliokuwa wakiogopewa.