Houthi wanatumia mbinu za kivita ambazo zitaichosha Marekani kama ilivyotokea Ukraine

Houthi wanatumia mbinu za kivita ambazo zitaichosha Marekani kama ilivyotokea Ukraine

[emoji3578] Sasa mtu mpaka aombe Muungano na Nchi zingine ndio waende Frontline, sasa huyo kweli ana nguvu...?

[emoji3578] Na kuhakikishia hata Kama Iran haina Hizbullah,Houth na Hamasi, huyo US hati pua hao hapo Iran.

[emoji3578] Na siku zinavyodi kwenda hao Iran wanaendelea kujiwekea utawala hapo Middle East.
Nandio ukweli kwa sasa iran hashikiki yaani hakuna taifa linaloweza kwenda beto ya moja kwa moja na iran

Anakuja Mmarekani mmoja wa jf anasema wanamtaftia sababu

Ukimuuliza iraq syria libya vietnam Afghanistan walitafta sababu gani anakimbia
 
Tamko kwamba Marekani haina tena pesa kuisaidia Ukraine limekuwa ni la wazi na hata taifa hilo limesema jukumu la kuendelea kuisaidia Ukraine kupigana na Urusi imewaachia wenzake 50 wafanye hivyo.

Pamoja na tamko hilo kutokana na uchofu katika vita hivyo, Marekani pia imesema haina mpango wa kwenda kutengeneza silaha za kivita ambazo zimeharibika.

Mbinu za kivita zinazotumiwa na wanamgambo wa Houth katika kuendelea kuzuia safari za meli za mataifa yanayoisaidia Israel kuleta janga Gaza zinazopita bahari nyekundu, nazo zimetajwa huenda zikapelekea kuchoka kwa Marekanini kwa mara nyengine kupambana na wanamgambo hao.

Mpaka juzi Marekani ilikuwa imeshafanya mashambulizi dhidi ya maeneo ya wanamgambo hao kwa siku 8 tofauti.Katika kila siku ya mashambulia Marekani ilitoa takwimu za mafanikio ya mashambulio hayo na kusema ilikuwa imeharibu rada za kufuatilia safari za meli na za kuongozea mashambulizi ya kundi hilo.

Pamoja na matangazo ya mafanikio hayo mashambulio ya Houth bado hayajasita ambapo juzi hiyo hiyo walifanikiwa kuzilenga na kuzipiga bila madhara makubwa meli mbili za mizigo zilizokuwa zikipeperusha bendera ya Marekani.

Wanamgambo hao wa Yemen wameelezwa kuwa kutokana na vita vyao na Saudi Arabia vya miaka kadhaa kabla ya kusitishwa mwaka 2022 wamepata uzoefu mkubwa wa kuficha silaha zao.

Sehemu kubwa ya wapiganaji wa jeshi hilo huwa wanapata mafunzo na kusambaa maeneo mbali mbali bila kuwa na kambi maalumu. Teknolojia za kivita wamekuwa wakipata kwa msaada kutoka wataalamu wa Hizbullaha na wale wa Marekani.

Rada na silaha zao muhimu huwa wanaziweka kwenye gari ndogo ndogo ambapo mara baada ya kufanya shambulio moja huondoka eneo hilo na kuelekea kituo kingine. Marekani tayari ina droni za upelelezi aina ya Reaper juu ya anga la Yemen kufuatilia mienendo ya kundi hilo. Hata hivyo kutokana na mfumo wa kupiga na kuhama imetajwa kuwa droni hizo hazitoweza kuleta tija kubwa katika kuzuia mashambulio ya Houth.

Kuhusu silaha wanazotumia Houth ni uhakika kuwa nyingi zinatokea au kupitia Iran baadae kusafirishwa kwa meli ndogo ndogo kupelekwa Yemen. Kutokana na wingi wa meli hizo na pamoja na ujasusi mkubwa inaofanya Marekani kufuatilia silaha hizo nako kumeelezwa haitokuwa rahisi kuzipekua meli zote hizo kuzuia silaha hizo zisiwafikie Houth.

Wiki mbili zilizopita jaribio la kuzuia silaha kutowafikia wanamgambo wa Yemen zilipelekea askari wawili wa Marekani kuzama na kupoteza maisha. Haikuwekwa wazi mazingira yaliyopelekea askari hao kuzama na hatimae kupotea moja kwa moja

Mwisho wa yote matarajio ni kuwa katika vita baina ya Marekani na wanamgambo wa Houth kutapelekea hasara kubwa kwa Marekani na hatimae kuchoka bila kufanikiwa kuwazuia wanamgambo hao kuendelea kuzichagiza meli za mizigo zinazopita kwenye lango la bab Mandeb kuelekea au kutoka mfereji wa Suez.
Jana Wamarekani meli yao moja ya kijeshi imepigwa wakatoka mbio na meli zao nyingine za kijeshi.

Wamarekani wanafikiri dunia ya leo ni ya miaka 30 nyuma. Mambo yamebadilika, ni kama dunia ilivyotoka kwenye kupigana kwa mishale ilipogunduliwa bunduki. Sasa duniani missiles watu wanatengeneza hata uwani tu.

Siku hizi ubabe wa kizamani unaadhirika tu miji ya watu:

 
✍️ Sio Kwa Iran ya sasa, wameshachelewa wakati huu wao wenyewe wapo hoi huko Ukraine...

✍️ Iran ya sasa ni mkubwa mwenzao sema jeuri tuu zimewajaa, ila wataelewa tuu.
Mkubwa wakati anahangaika na vikwazo uliwahi kuona Iran anamuwekea mtu vikwazo.
 
Kama uko vizuri kichwani ungechukua baadhi ya mistari niliyoandika ukatafuta ukweli wake halafu ukanisaidia pale ambapo ungeona nimekosea.
Nadhani modi wa JF wananiamini na wanafanya kazi ya kutathmini.Wewe huna uwezo huo.
mod wa JF anahusika vipi na porojo unazoweka hapa, tulikubaliana ukiweka thread unakuja na source otherwise tunapuuza tu ulichoandika, huwezi kuja na interest zako hapa kwasababu kuna mtu anakuamini jf .,nonsense..!, hii forums inapitiwa na watu wengi wasomi
 
Kuiondoa utawala wa mahayatollah nchini Iran ndio mpango mzima. Huo utawala hauna mustakbali wowote huko tuendako.
𝗜𝗦𝗥𝗔𝗘𝗟𝗜 𝗠𝗔𝗡 𝗝𝗔𝗜𝗟𝗘𝗗 𝗙𝗢𝗥 𝗥𝗘𝗙𝗨𝗦𝗜𝗡𝗚 𝗧𝗢 𝗦𝗘𝗥𝗩𝗘 𝗜𝗗𝗙 𝗪𝗜𝗟𝗟𝗜𝗡𝗚 𝗧𝗢 𝗥𝗘𝗧𝗨𝗥𝗡 𝗧𝗢 𝗣𝗥𝗜𝗦𝗢𝗡 𝗔𝗚𝗔𝗜𝗡

An 18-year-old Israeli man, jailed for refusing to serve in the Israeli military, has told Sky News he is prepared to go to prison again because, in his opinion, the war in Gaza is not a way to achieve peace with Palestinians.

Read more: news.sky.com/video/israel-h…

#IsraelHamasWar #GazaGenocide #IDF
 
Back
Top Bottom