How Can There Be Free-Will ?

Mara nyingi huwa nasema kuwa suala la uwepo wa mungu ni la imani lakini bahati mbaya watu hawanielewi,sasa mtu anapokwambia umpe uthibitisho katika suala la imani ndipo tatizo linapoanza.

Na ndiyo maana mie huwa sijisumbui na kuthibitisha uwepo wa mungu,suala likishakuwa la imani basi kuna watakao amini na watakaokataa kuamini. Laiti kungekuwa na uthibitisho wa aina wautakao atheists basi hili suala lisingekuwa la imani.
 
Mada inachosha na inaumiza akili....mie tangu niliposoma mahala kwamba Mungu aliufanya moyo wa farao kuwa mgumu asiwaruhusu wana wa israel....wakati huo huo anamtuma musa akanigoshieti kuachiliwa kwao....hapo ndo najua kweli....ubashite unahistoria ndefu sana.
 
Kwanini umesema hivyo? Fafanua kidogo,tungo tata hiyo.

Mimi nina swali.

Hivi kama Mungu yupo, halafu Mungu anaufanya moyo wa Farao uwe mgumu, Farao afanye dhambi kwa sababu Mungu kaufanya moyo wa Farao uwe mgumu.

Siku ya hukumu kwa wanaoamini ipo, Farao atahukumiwa kwa dhambi ambazo alizifanya kwa sababu Mungu aliufanya moyo wa Farao kuwa mgumu?

Mungu akimhukumu Farao kwa dhambi ambazo alizifanya kwa sababu Mungu aliufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, Mungu huyu atakuwa hajamuonea Farao kweli?
 




Kuna Mawili.

-1 -inawezekana hivi vitabu vimejaa uongo mwingi uliopenyezwa,Sasa as time goes on watu akili zinapanuka na kuona mambo mengine hayaingii akili ,

Kwanza tukichunguza uandishi wa hivi vitabu ulivyofanyika unatia mashaka sana,mfano hivi vitabu vyote kuanzia Biblia na Quran vilikusanywa kwa maandishi kwa pamoja baada ya hao mitume kutokuwepo,Biblia imekuwa grouped na kuwa translated into dozens of language baada ya huyo Yesu,kuuliwa au kupaaa whatever,Na the interesting thing about Bible is ,Christians rely on those translations as the word of God ,utakuta mswahili kashika Biblia ya Kiswahili alafu anakwambia HILI NI NENO LA MUNGU ,How ? Kama kweli hayo mawasiliano kati ya Mungu na Yesu yalikuwepo ,then Biblia ya Kiswahili haiwezi kuwa ni neno la mungu bali ni maana ya yale maneno ya mungu ,because HIYO communication ilikuwa lazima ifanyike katika language ambayo Jesus could understand,sasa how biblia ya Kiswahili iwe ni neno la mungu ? what was the original language of bible ?

Sote tunajua kuwa unapotafsiri kitu kwanza unaharibu ualisia pili inakuwa nirahisi kubadili mambo na ku distort the message , kwahiyo uhalali na uaminifu wa hawa waandishi wa hivi vitabu tunauweka Kwenye kundi gani ?

kuwa waliweka accurate information,na I am sure it can't be accurate because the information contradicts itself thousands times ,Kwahivyo ni dhahiri kuna uongo mwingi Ambao ni old version kwa watu wa Karne yetu.

Aidha ,Quran imekuwa grouped kwa pamoja baada ya kifo cha Muhammad(saw),kwenye utawala wa khalifa wake aitwaye Abubakar Sidiq,tena inasemekana wale waliokuwa wanaikusanya walifika pahali kukawa kuna contradiction ya ayah (verse), ambayo ilikuwa imehifadhiwa na sahaba(companion) mmoja tu ,So Abubakar Sidiq akatoa rai kuwa hiyo ayah iandikwe tu kwa Sababu huyo sahaba aliyehifadhi ni sawa kama wamehifadhi masahaba wawili.kwahiyo kumbe kwenye uandishi wa hivi vitabu kulikuwa kunauwezekano wa watu kutoa rai zao,hii ni Hatari juu ya Truth .

The Interesting thing about Muslims ,90% ya non arabic speaker Muslims hawaielewi Quran ,lakini hao 90% almost wote wamehifadhi Quran ,wewe tafuta muislam hata mtaani kwako mwambie akusomee part ya Quran aliyohifadhi,I am sure lazima atasoma ,akimaliza muulize maana yake nini ,you will be surprised ,ukimuuliza Sasa how come unahifadhi something you don't understand,atakuambia hiyo ndiyo miujiza ya Quran.

-2- Haya matukio yote hayakutokea Kabisa ,and non of them existed .Ni personal idea za watu TU .
 
Maana ya kufanya moyo kuwa mgumu ni nini?
 
Mkiulizwa idea ya dini ilianza wapi hamjui ila mmeshikilia tu kuwa ni mawazo ya watu.

Mnatumia muda mwingi na maneno mengi kupinga uwepo wa mungu ila hamna muda kabisa wa kufikiri huo uwezokano wa kutokuwepo mungu? mlishawahi kufikiri pia kama ina make sense kutokuwepo kwa mungu au chochote tu kile ambacho ndiyo kitakuwa ni nafasi ya mungu?

Tatizo kupinga ni rahisi tena hasa katika mambo kama haya ya imani.
 
Maana ya kufanya moyo kuwa mgumu ni nini?
Ni kumuingilia asifanye alichoweza kufanya mwenyewe na kumfanya awe mbishi kuhusu kuwaachia "watu wa Mungu" waende.

Kwa mujibu wenu:-

Mungu wenu anapoingilia uhuru wa mtu kuamua, mtu akafanya vibaya kwa sababu Mungu wenu kamuingilia uhuru wake wa kuamua, siku ya hukumu huyu Mungu akimhukumu (penalize) huyu mtu kwa kufanya kile ambacho hakuwa na uhuru wa kutokifanya kwa sababu Mungu alimlazimisha, huyo Mungu atakuwa sawa?
 
Ni utumwa wa kisaikolojia tu.

Huyu Mungu anayesemwa na hivi vitabu hayupo.

Kwa sababu unaweza kum disprove kwa kutumia kitu rahisi kama a logical truth table.
 
Kwa nini swali la idea ya dini ilianzia wapi liwe muhimu sana?

Idea ya dini ilianzia kwenye ujinga.

Kama Mungu yupo, ana uwezo wote, ana ujuzi wote, kaumba ulimwengu, kwa nini hakuuumba ulimwengu uwe hauwezekani kuwa na mabaya yoyote wakati alikuwa na uwezo huo?

Hujajibu swali hili.
 
Hujajibu swali.

Mtu ana free will ya kuwa Mungu?
Nimekuuliza bado hatujaelewana? kwa sababu uliuliza kama mtu ana freewill ya kupaa na tena unauliza kama mtu ana freewill ya kuwa mungu? ndiyo maana nauliza bado hatujaelewana kwa sababu unaweza ukaniuliza maswali hadi mia na mie sipo hapa kuulizwa tu maswali na kujibu.

Nauliza tena bado hatujaelewana?
 

Kupaa na kuwa Mungu ni sawa?

Utakuwaje na freewill ya kupaa wakati huwezi kupaa?
 
Huko kwenye ujinga ndiyo wapi?



Halafu ushasema kuwa ana ujuzi na uwezo wote, na unasema kabisa kuwa anao uwezo wa kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezekani lakini hakuumba hivyo,je ni nini tena unachotaka kuuliza?

Au unataka kusema aina hii ya ulimwengu ambao maovu yanawezekana hata wewe huo ujuzi na uwezo unao?
 
Huko kwenye ujinga ndiyo wapi?

Zamani.


Halafu ushasema kuwa ana ujuzi na uwezo wote, na unasema kabisa kuwa anao uwezo wa kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezekani lakini hakuumba hivyo,je ni nini tena unachotaka kuuliza?

Inaelekea huna uelewa wa maana ya neno "kama".

Au unataka kusema aina hii ya ulimwengu ambao maovu yanawezekana hata wewe huo ujuzi na uwezo unao?

Ujuzi na uwezo gani?

Sentensi hii haijajitosheleza kueleweka kama ilivyo, nitabashiri kwamba unamaanisha "huo ulimwengu ambao maovu yanawezekana hata wewe una ujuzi na uwezo wa kuuumba?"

Mimi kutokuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hakuthibitishi Mungu mwenye uwezo huo, ujuzi huo na upendo yupo.

Na hakujibu swali langu.

Kama Mungu yupo, ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya mengi sana yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya yoyote hayawezekani?

Hujajibu swali hili.

Hujajibu.
 
Kupaa na kuwa Mungu ni sawa?

Utakuwaje na freewill ya kupaa wakati huwezi kupaa?
Hata kuwa panya na kupaa pia si sawa,je ndiyo utaniuliza kila kitu kama kina freewill au hakuna?


Nilifikiri mfano wa baiskeli ulitosha kujibu hilo swali lako la kupaa!
 
Zamani ndiyo nini sasa? hebu fafanua.


Sasa ulimwengu huu wenye kuruhusu maovu unathibitisha vp kuwa hakuna mungu mwenye upendo,ujuzi na uwezo huo kuwa hayupo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…