Naona akili yako imeamua kutengeneza dirisha la kuikimbia hoja yako kwa kuongeza viroja
Free will ni wewe kuamua kuvuta sigara ukijua inasababisha kansa usiwasingizie TCC kuwa wanasababisha kansa
Uzwazwa wako sio kosala muuza sigara
Habari yako Gentleman.
Let me help you to understand what's Free Will .
Free Will is the ability to have done otherwise or ability to determine your own destiny in making your own choices.
Au kwa maneno mengine wanasema wewe ndiye unaejipangia maisha yako kwa kuchagua machaguo yako unayoyaona ni sahihi kwa muktadha wako.Bimaana,wewe ndiye utakae chagua uingie motoni au peponi kwa machaguo yako utakayoyafanya hapa duniani.Lakini kumbuka kwamba tukiingia kwenye ukweli wa ulimwengu,sio machaguo yote yapo kwenye mamlaka au kwenye maamuzi yako,kuna machaguo mengi ambayo tunayafanya yapo nje ya mamlaka yetu (out of our control ) .
Mathalan ,Mara nyingi maamuzi ya busara ya mtu yanategemea sana IQ/ Intelligence ya huyo mtu,kumbuka kwamba Intelligence inakuwa determined na DNA and Genes za mwili wako ,hauwezi kuamua uwe na IQ au Intelligence ya kiwango gani ,kwahiyo ukiwa na low IQ kuna uwezekano mkubwa ukafanya maamuzi ambayo yataleta athari mbaya kubwa kwenye maisha yako na ya wengine(Ikiwa wewe ni Rais wa nchi)na matokeo yake ukaenda motoni(for those who believe in Hell ) .
Matatizo mengi kwenye hii dunia yanasababishwa na uwezo wetu wa kufikiri ambao we have no control with .Naamini kila Mtu angependa kuwa na IQ kubwa ili iweze kuleta positive impact kwenye maisha yake ,sasa wewe unaye amini una Free Will ,Je unaweza kuamua aina ya IQ uitakayo.? Kwasababu lazima ukubali kuwa huu utafauti wa maisha ni kutoka na IQ zetu kwa kuathiri uwezo wa kufikiri ambao hatuna mamlaka nao.
Unaposema kuwa una Free Will ,hivi una tafakari kuwa the universe ina nafasi kubwa ya kuingilia maamuzi yako bila ya idhini yako ? Newton's Laws Of Motion Can Explain This .
Mathalan,Je unapopija mpira ,unaweza kuamua kwa asilimia mia moja mpira ukatue wapi na kutulia wapi ? Can you decide that ?
The ultimate answer is NO,you can't decide for sure .100% .kwasababu kuna outside forces ambazo huna mamlaka nazo zita ingililiana na maamuzi yako na kuharibu kile ambacho ulitaka kukifanya ,the physical motion of your foot ,the grass on the field ,the wind in the air ,zote hizi zitaathiri makusudio yako ,,kwahiyo huwezi kuamua kwa asilimia 100 mpira utue wapi na uingie wapi.
Sasa unanipa wakati mgumu unaposema unayo Free will wakati kuna maamuzi mengi unayafanya yapo nje ya mamlaka yako ambayo ilibidi yawe ndani ya mamlaka yako ili utengeneze mwisho wako mzuri au mbaya.
Umezungumzia suala la kuvuta sigara na cancer,kwamba umepata Cancer kwa kuwa ulichagua kununua sigara,inaonekana wewe unachojua kuhusu Free Will ni ule uwezo wa kuchagua kufanya au kutofanya,My Dear Brother,Free will Is More Than That .Kadhalika pia nikufahamishe ,huko kupata hiyo Cancer pia siyo maamuzi yako na wala haihusiani na maamuzi yako ya kununua sigara,kwani kuna watu wangapi wanavuta sigara maisha yao yote na hawapati hiyo Cancer ,na wengine miaka miwili tu ya uvutaji sigara tayari ameshapata Cancer ,Je utasema huyu aliyepata Cancer ni Free Will yake ndiyo imemfanya apate Cancer ? Vipi kuhusu yule ambaye hakupata ? Free Will haijafanya kazi ama ?
—Think •
Wapi utachora mstari kuhusu Mambo ya Genetcs ,Laws Of Gravity ,Time ,Nerve Activity,Hormone Imbalance,Infertility pamoja na Free Will ? Hayo yote hapo juu yana athari kwenye hiyo unayoiita Free Will ,nini rai yako katika hili?
—Free Will does not exist ,ni illusion tu na idea ya watu wa dini Katika kupumbaza watu.•
Thanks !