Al-Watan
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 11,891
- 14,583
Zamani ndiyo nini sasa? hebu fafanua.
Hufahamu zamani ni nini? Angalia kamusi. Tafuta maana ya "pre-history".
Sasa ulimwengu huu wenye kuruhusu maovu unathibitisha vp kuwa hakuna mungu mwenye upendo,ujuzi na uwezo huo kuwa hayupo?
Kwa sababu Mungu mwenye upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote kuumba ulimwengu ambao maovu yanawezekana wakati anaweza kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezekani ni kujipinga yeye mwenyewe.
Ni kama baba mwenye upendo sana, uwezo mkubwa sana na ujuzi mkubwa sana ambaye uwezo wa kujenga nyumba nzuri sana ya kuishi yeye na familia yake anayoipenda, badala ya kujenga nyumba nzuri ya kuishi yeye na familia yake, ajenge nyumba ya kuishi yeye na familia yake halafu afiche mabomu katika kuta zote za nyumba, kila siku liwe linalipuka bomu na kuua watoto na watu wa familia yake.
Ukiambiwa gaidi katega mabomu nyumbani kwa adui yake hapo unaweza kuelewa habari hiyo.
Ukiambiwa baba mwenye uwezo sana, ujuzi sana na upendo sana kajenga nyumba yake mwenyewe, halafu kaijaza mabomu kibao kwenye kuta kila siku anaachia yalipuke na kuumiza na kuua watoto wake mwenyewe, utaona hii story ya uongo halafu aliyetunga hata hajui kutunga story ionekane inaaminika.
Hii ndiyo habari ya Mungu wenu huyo.
Ukweli unaenda na logical consistency. Ndiyo maana hata mahakamani watu wakitafuta ukweli wanaangalia logical consistency.
Hadithi ya kuwepo kwa Mungu wenu haina logical consistency.
Ina contradiction.
Kwa sababu hayupo.
Katungwa tu.
Katungwa na watu ambao walikuwa hawana elimu ya kuangalia logical consistency.