How Chato will look in 2025 like President Mobutu's ruined jungle paradise, Gbadolite

How Chato will look in 2025 like President Mobutu's ruined jungle paradise, Gbadolite

Hii thread inatufundisha mambo makubwa sana ya kiroho......tuheshimu na kukanyaga hii ardhi ya Mwenyezi Mungu kwa adabu sana.

Tusifanye mambo yatakayoiudhi sehemu kubwa ya jamii....

MUNGU YUPO.

Huyu Camilo Cienfuegos sio wa kumbeza....,kuna kitu alikiona , alikuwa na uhakika ,akasema bila kupepesa macho.

Yametokea.
 
Halafu watu hawajui nilivyompigania kiongozi wetu Mtukufu kwenye forum za Wakenya! Hivi ni huyuhuyu aliyekataa kupanda ndege akasema atasafiri kwa barabara leo hii anajenga uwanja wa kimataifa Chato? Haki uzalendo umenishinda daah hii kali! Hapa Ubadhirifu tuu! Huyu jamaa ana element za nepotism hili lisemwe wazi sasa bila kumuogopa...

Enzi hizo kichwa kikiwa timamu.,hahah.
 
Hivi ni nani hapa dunian alishawahi kuwafanyia binadam wenziye uovu na akaishia pazuri?!!! Mwisho wa waovu wote huwa ni mbaya tu, huwa wanarukaruka tu wakati wakiwa na madaraka au pesa lakin mwisho wao huwa ni ama mateso au aibu nzito sana..

Mwili na/au Damu ya mwanadamu ni kitu kizito sana..laiti ma ccm yangelitambua hilo mapema before its too late.
 
Umemuelewa lakini mleta mada au unakurupuka.

Mshaurini vizuri mkuu wa nchi.

Km Chache toka Mji wa Chato kuna kiwanja cha ndege cha Biharamulo eneo la Katoke.
Kiwanja hicho ni cha nyasi kilipaswa kikarabatiwe ili Kitumike kwa manufaa ya Watu wa Biharamulo na Chato.

Miundo mbinu inapaswa iangalie pia masuala ya kiuchumi. Chato haina hadhi ya kuwa na uwanja wa ndege wa kimataifa ni kupoteza rasilimali fedha za umma.

Baada ya Kuhamia Dodoma ambapo napo patajengwa Uwanja wa ndege wa kimataifa viwanja vya ndege vya miji midogo ya pembezoni vitakufa .
Watu watatoka Dodoma na kutumia usafiri wa magari mana patakuwa karibu kwenda Tabora ,Singida, Geita n.k.
Ndio maana huwezi leo ukajenga kiwanja cha ndege Kibaha kwani tayari uwanja wa mwalimu Nyerere unatosha.

Mleta mada anakuonyesha jinsi majumba na viwanja vya ndege alivyojijengea Mabuto Sese seko kwa kuamini kuwa atakua raisi wa maisha vimekufa baada ya kuja kiongozi Mwingine mwenye maono tofauti na yake.

Hata hivyo MUDA ndio utakao toa majibu sahihi kwenye awamu hii ya tano.
Muda umeshatoa majibu.
 
Back
Top Bottom