Magufuli haonekani kuwa kiongozi anayeweza kuongoza pasipo vituko na mikasa, na mimi naamini ni suala la muda tu kabla mtu huyu hajaanza kupamba vyombo vya habari vya ndani na kimataifa for all the wrong reasons.
Hatua yake ya kuijenga Chato na kijiji chake cha Kilimani haiwezi kuwa tofauti na hekima ya Mobutu kukijenga kijiji chake cha Gbadolite wakati akiwa Rais wa Zaire - wakati mwingine serikali yote ilikuwa ikihamishiwa huko, na vikao vya Baraza la Mawaziri na vikao vya Usalama vikiendeshwa hukohuko; hata Baba Mtakatifu John Paul wa II alipata kufika Gbadolite na kulala huko.
Kwa speed hizi za Magufuli, naamini ni suala la muda tu kabla hajataka ajengewe Ikulu ndogo Chato na serikali itakuwa ikihamishiwa huko, vikao vya Baraza la Mawaziri vitakuwa vikiitishwa huko - na sababu inaonekana kuwa Magufuli ni kiongozi anayeongoza huku akiwa na hofu kuu mno kuhusu usalama wake,hajiamini hata chembe.
Dar es Salaam anapaogopa, na akifika Dodoma pia atapaogopa - atavutiwa kwenda Chato.
God forbid.
Kuna Kiongozi wa Tanzania ambaye hajawahi kujenga kwao ukiondoa Mkapa tena ambaye anachekwa na
kulaumiwa na Watz hao hao kama wewe alipoenda kujenga Lushoto badala ya kwao Mtwara, hata hivyo Mkapa alijenga Daraja kwao lijulikanalo kama Daraja la Mkapa, alifufua Mtwara
corridor ambapo lengo ni kuunganisha Bandari ya Mtwara na Ziwa Nyasa vile vile alijenga Daraja la umoja kuunganisha TZ (Mtwara) na Msumbiji kote huko ni kwao yeye Mkapa?
Mlm.Nyerere aliijenga kwao Butiama leo hii hata mtoto mdogo anajua Butiama ni nini na wapi ingawaje hakuna chochote huo isipokuwa ni kwamba ni mahali alipotoka Mlm.Nyerere
hata Mkoa wa Mara haukuwepo wkt tunapata uhuru lkn Ml.Nyerere aliuanzisha
kwa sababu ni kwao achilia mbali Wakuu wote wa Majeshi TZ walitokea Mkoa wa Mlm.Nyerere Mara, ingawaje hiyo ni mada nyingine
, akaja Mwinyi kwetu Pwani kulikuwa hakujulikani kwanza yote tulikuwa kama sehemu ya Mkoa wa Dar kwa kuwa Mwinyi kwao asilia ni Kisarawe akaanzisha hiyo Wilaya na kuunda rasmi Mkoa wa Pwani kuutenganisha na Dar leo hii
Kisarawe imeendelea ni kwa sababu ya Mwinyi tu, akaja Kikwete hakuna aliyeijua Msoga na Chalinze ukiachia njia ya kuendea Mikoani lkn Kikwete (Serikali) aliwekeza Bagamoyo na Chalinze mambo mengi yalifanyika huko kama mradi mkubwa wa maji kwenda Chalinze, hata kulikuwa na mpango wa kujenga Airport mpya na kubwa ya Kimataifa Bagamoyo achilia mbali Bandari ya Bagamoyo na mambo mengine mengi tu,
sasa kwa nini kwa raisi Magufuli ije kuwa nongwa na tayari mnamlinganisha na Mobutu kama siyo chuki binafsi ni nini?
Inawezekana kabisa
labda ndiyo mfumo wetu na mpango wa Serikali yetu kwamba Kiongozi Mkuu wa nchi anakotoka kunapewa upendeleo fulani, kwa maana wote ni hivyo hivyo hata Monduli inajulikana tu kwa sababu ya Sokoine, Same imejengwa na kuunganishwa na Umeme na Br. kwa sababu ya Msuya kabla ya Msuya Same ilikuwa ni kijiji tu na vumbi tupu,
Manyara umekuwa tu Mkoa kwa kumegwa ktk Arusha kwa sababu ya Sumaye, yeye ndiye aliyefanikisha hilo
kwa kuwa ni kwao, Katavi imekuwa tu Mkoa kwa sababu ya Pinda ambaye ni kwao, sasa kwanini iwe ishu kwa Magufuli kama kila Kiongozi kuanzia Nyerere wote walikupa kwao upendeleo maalumu?
Kwa nini hamfananishi Mlm.Nyerere na Mobutu?