Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Acha kutetea upumbavu wewe! Narudia, acha kutetea upumbavu! Kwa viongozi wengine wapi huko? Nyerere? Wapi? Unazungumzia Uwanja wa Ndege Musoma? Ina maana hufahamu kwamba Musoma ni Makao Makuu ya Mkoa? Unalinganisha vp Musoma na Chato?
Huyo Mwinyi wapi? Una habari kwamba Mwinyi kwao ni Mkuranga? Mkuranga kuna Uwanja wa Ndege pale? Mkuranga kuna investment yoyote ya kipumbavu iliyofanyika in favor of Mwinyi? Or, let's consider Mwinyi ni Mzanzibari! Ni investment gani imefanyika Zanzibar kwa sababu tu Mwinyi alikuwa Rais?
Au unamzungumzia Mkapa? Unafahamu kwamba Mkapa kwao ni Masasi? Hivi unafahamu kwamba ingawaje Masasi ni Wilaya lakini ukubwa wake na population yaeke inashindina na mikoa kadhaa Tanzania hii? Masasi kuna Uwanja wa Ndege? Uliza Wayao na Wamakuwa kama hata ndege yenyewe wanaifahamu? Au ni investment gani ya kipumbavu unaizungumzia ambayo Mkapa ameifanya kwao? Mkapa ni mtu wa Kusini na kilio ca watu wa Kusini miaka yote ilikuwa barabara! Hivi una habari hata baada ya kukaa miaka 10 madarakani Mkapa aliiacha Barabara ya Kibiti ikiwa kimeo? Sasa hao viongozi unaozungumzia wewe wanajenga kwao ni akina nani?
Au ni Kikwete? Unatakiwa kukumbushwa kwamba JK aliingia Magogoni akitokea kuwa Mbunge wa Chalinze huku akifahamika zaidi kama mtu wa Bagamoyo? Hadi ametoka madarakani kuna investment gani ya kijinga aliifanya Bagamoyo au Chalinze? Chat kuna nini hata udhanie forecast ya miaka 40 itafanya international airport iwe viable investment? Unaweza kulinganisha potential ya Bagamoyo na Chato hata kama wangejenga huko Bagamoyo? By the way, hivi unafahamu lengo la kuataka kujenga Uwanja wa Ndege Bagamoyo ni kv ilionekana Uwanja wa Dar es salaam umezungukwa na makazi ya watu kwahiyo ilikuwa ni busara kutafuta eneo lingine jambo ambalo hufanyika kwenye nchi nyingi! Pamoja na yote hayo, bado watu wakaona that's stupid idea for the time being... sasa unafananisha vp Bagamoyo na Chato? Au ndo yale yale ya kupeleka hadi taa za barabarani wakati hata magari yenyewe hakuna?
View attachment 380578
Una matatizo ya uelewa hivyo siwezi kupoteza muda wangu kujibizana na wewe, nimesema hakuna Kiongozi ambaye hakupeleka/ hakupelekewa miradi kwao alipotoka huo ndiyo ukweli kama hautaki sikulazimishi!