Kwa mtazamo wangu naona wakoloni walikuja Afrika wakatuchota akili zetu na kutufanya tuishi maisha yanayoendana na matakwa yao yenye maslahi kwa nchi zao (walitufanya tuwategemee kiakili, kimaarifa na kiutendaji)!
Africa tulikuwa tukijiendesha wenyewe na tamaduni zetu, mila zetu, uchumi wetu ambao uli-base kwenye 'batter trade', tulikuwa na teknolojia zetu ambazo kama tungeziendeleza tungekuwa mbali kiteknolojia.
Walikuja wakavuruga mfumo wa maisha yetu ya kawaida, wakachukua nguvu kazi ya Africa na kuipeleka Ulaya, wakatuibia technolojia yetu na kwenda kuiboresha na baadaye kuturudishia kwa kutuuzia kwa bei kubwa, wamepora maliasili zetu na kwenda kuendeleza viwanda katika nchi zao. Hizi zinaweza kuwa ni baadhi tu ya factors zilizopelekea bara la ulaya kulididimiza bara la Africa kimaendeleo.
Lakini, kunatofauti gani kati ya akili ya mzungu na ile ya mwafrika? Inawewekana wao wametuzidi kiakili ndiyo maana hatuendelei kama wao?