How Europe Underdeveloped Africa

How Europe Underdeveloped Africa

Labda mkoloni mwingereza mbaya kuliko wote!! Now we are turning our arrows to indian and chinese,wenzetu wanawekeza afrika,kina lowassa &co wanaweka uchumi europe.
 
Kama uwepo wa wakoloni (wazungu) umechangia uduni wa maendeleo ya waafrika.

Mbona Ni miaka takriban zaidi ya hamsini 50 tangu wazungu wameondoka Lakina hakuna jipya waafrika walicho kifanya katika mendeleo yao wenyewe.Mashule na Vitega uchumi bado ni vilevile walivyoacha wazungu na vingine vimekufa.

Badala yake mnawaita tena kwa kutumia lugha nyingine ya Uwekezaji, Gesi, mafuta na madini bado hamuwezi kuchimba wenyewe kwa miaka 50 sasa TZ bado haina wataalamu na technolojia to explore those resources. na bado bajeti nyingi za waafrika zinawategemea tena hahao wazungu.

I think we give Europeans too much credit,kutokuendelea kwetu ni uamuzi wetu sisi wenyewe,mtu akija akataka kukutapeli,unajua anakutapeli lakini bado unakubali akutapeli,nani wa kulaumiwa hapa.
Janga letu kubwa ni ubinafsi.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Rodney ameandika kitabu kabla makoloni ya Asia ikiwemo,India,Malasia,Indonesia,Honkong etc hayajapiga hatua kubwa za kimaendeleo kama iilivo hivi sasa.. Maendeleo ya nchi hizi ni ushahidi tosha kwamba tatizo siyo ukoloni mamboleo bali ni uwongozi mbovu tena mbovu haswa Afrika.

Kweli mkuu; hapo kwenye red nakubaliana na wewe 100%
 
Wala simwung mkono walter rodney....waafrika hatuendelei sabab ya ujinga na upumbavu wetu wenyewe. miaka 50 hata 70 kwa nchi nyingne baada ya ukolon kuna maendeleo gan? tunakaa kulaumu wakolon huku tunawapa rasilimal zetu wazitumie kwa faida yao. tunaona madin na meno ya tembo....ardh,gesi n.k. tunakaa tumejikunyata eti wakolon ndo wametufanya tuwe maskin...umaskin wetu upo kwenye akili na si kwenye mali.
 
Kwa mtazamo wangu naona wakoloni walikuja Afrika wakatuchota akili zetu na kutufanya tuishi maisha yanayoendana na matakwa yao yenye maslahi kwa nchi zao (walitufanya tuwategemee kiakili, kimaarifa na kiutendaji)!

Africa tulikuwa tukijiendesha wenyewe na tamaduni zetu, mila zetu, uchumi wetu ambao uli-base kwenye 'batter trade', tulikuwa na teknolojia zetu ambazo kama tungeziendeleza tungekuwa mbali kiteknolojia.

Walikuja wakavuruga mfumo wa maisha yetu ya kawaida, wakachukua nguvu kazi ya Africa na kuipeleka Ulaya, wakatuibia technolojia yetu na kwenda kuiboresha na baadaye kuturudishia kwa kutuuzia kwa bei kubwa, wamepora maliasili zetu na kwenda kuendeleza viwanda katika nchi zao. Hizi zinaweza kuwa ni baadhi tu ya factors zilizopelekea bara la ulaya kulididimiza bara la Africa kimaendeleo.

Lakini, kunatofauti gani kati ya akili ya mzungu na ile ya mwafrika? Inawewekana wao wametuzidi kiakili ndiyo maana hatuendelei kama wao?
 
Enzi izo UDSM ilkuwa ya ukweli ,waalimu wake walikuwa wanaweza kuapmbanua hasa na kujenga hoja,siku hizi nimekuwa nikiwasikia waadhiri wengi hasa wa political science wakijenga hoja dhaifu sana hadi kutia aibu,wengi wanakaribishwa kutoa maoni mfano BBC voice of America na kwingineko lakini kwa kweli wanalitia taifa aibu as if wao nao ni marecturers wa voda fasta.
 
Mimi pia nilikisoma hicho kitabu muda kidogo. Ila kwa hali ninayoiona Africa leo, nachelea kukubali sana maoni ya huyu bwana. Inawezekana kweli Europe walichangia na wanaendelea kuchangia, ila na sisi nao bwana.. dah!

Ulisoma hukumuelewa.
 
Back
Top Bottom