How I Met My Wife

Mkuu stori yako tamu ila naungana na Nai "wewe huna msimamo". Ile mimba ya kwanza hukutakiwa kuitoa. Nai hakuwa mwanafunzi wala nini hivyo hakuna msukosuko wowote kisheria ambao ungeupata. Kwa ulegelege wako ona sasa umezika watoto karibia watano na zaidi ya yote umemletea uke wenza Nai. Umenisikitisha mkuu. Nai hakupaswa kuwa kwenye ukewenza. She was a full package.
 
Mkuu, sometimes kama nataka kukubali hivii... Lakini hujawahi kukutana na sura ya Mama Nai wewe... Ndio maana!! Sometimes nilikuwa nafikiria kama naweza kupoteza shule yangu, nikawa mpole zaidi.
 
Mkuu, sometimes kama nataka kukubali hivii... Lakini hujawahi kukutana na sura ya Mama Nai wewe... Ndio maana!! Sometimes nilikuwa nafikiria kama naweza kupoteza shule yangu, nikawa mpole zaidi.
Nai aliyatoa maisha yake kwa sababu yako. She only needed a simple thing from you, a support. That is all she needed. But you let her down. Hicho chuo Wala usingekipoteza. Huwezi kufukuzwa chuo kisa eti umepiga mimba. Isitoshe hata kama ungefukuzwa kwa ajili ya Nai kulikuwa na shida gani? Nai sucrificed her family for you why couldn't you sucrifice your schooling fer her too?
 
Nzi Chuma

(i) Ahsante kwa simulizi yako

Ahsante pia kwa muda wako, nadhani umeona jinsi gani kuandika inavyokula muda.

(ii) Kuna mengi ya kujifunza kwenye simulizi yako yakiwemo:-

>> Umuhimu wa Kijana kuoa pindi akifikia umri ili aepukane na ufisadi, 'uharibifu'...

>> Umuhimu wa kuwa na msimamo na kusimamia unachoamini ili mradi umejiridhisha kuwa upo sahihi...

>> Umuhimu wa kushirikisha watu wenye busara katika mambo...

>> Umuhimu wa kutofanya ngono zembe...

>> Hatari iliyopo kwa kufanya arbotion...

>> Umuhimu wa Mabinti kujichunga hadi siku ya ndoa...

>> Umuhimu wa elimu...

>> Ubaya wa usiri (japo mara nyingine kuna faida)

>> Ubaya wa uongo...

>> Umuhimu wa mitala...

"Matumbo ya uzazi yana wivu" ni msemo ambao bado unathibiti tangia enzi za Sarah na Hajira (wake za Ibrahim baba wa Ismail na Is'haq)

Yani kama mkeo hajapata mtoto (as long as anaona siku zake za hedhi) ukioa na kuzaa kwa mke mwingine, kuna asilimia kubwa ya mkeo mgumba kupata mimba pia...

>> Ubaya wa kukata udugu... (Jitahidi umsamehe Dada, alikuwa yupo sahihi), binadamu tumetofautiana namna ya uwasilishaji...

Mfano mtu akisema, "Nzi Chuma, ndugu zako watakufa wote utakuwa mkiwa..."

Mwingine akisema, "Nzi Chuma, umejaaliwa umri mrefu zaidi kuliko ndugu zako..."

Unaweza kuchukia kauli ya mtu wa kwanza...
__
Msamehe kisha umuombe radhi nduguyo

>> Umuhimu wa kushea 'yaliyokukaba' moyoni kwa unaowaamini, naamini kuanzia sasa umetua mzigo fulani na huenda ikawa sababu ya wewe na dada yako kuunga udugu tena.

>> Umuhimu wa wazazi kuongea na watoto wao kuhusiana na 'afya na mambo ya uzazi'
__

Bila shaka umetumia majina ambayo si halisi ya wahusika.

__

Tunasubiri simulizi za wadau wengine. Na niwashauri kwamba, wote wenye nia ya kuleta simulizi hapa waanze kuandika sasa, taratibu bila kuweka post jukwaani hapa, ili simulizi moja ikiisha ije nyingine tayari ikiwa na episodi kadhaa, kusubiri sana post kipindi hiki cha sintofahamu ya Covid-19 haifai [emoji23]

James Jason
 
Mkuu nakushukuru sana, tuko pamoja..!! Mimi kwa sasa ni mwalimu mzuri sana katika haya mambo.. Dada nitafikiria namna ya kumsamehe nahisi kama naanza kuwaelewa hivi...!!
 
How Fisadi Kiwembe got his wife

Kutoka Sumbawanga, miaka kadhaa iliyopita kama nilivyosimuliwa

Jamaa alipata mke bila kutarajia.

Jamaa alikuwa fisadi kiwembe, kisha alijisifu kwa marafiki zake kuwa 'ameshakula madem' kila aina, mabonge, vimbaumbau, wafupi, warefu, weupe, weusi, wazungu, waasia, walemavu wa viungo nk, akawa amebakisha mwanamke albino tu.

Kwa hiyo mawindo yake yakawa ni kwa wanawake wenye ualbino.

Siku ya siku paap, akamuona binti mrembo umri unaokubalika...

Jamaa akaanza kumfuatilia na kumpiga sound nyingi...

Huku na huku baada ya kusotea wiki kadhaa jamaa akakubaliwa..

Kumbe binti albino hajawahi kuduu... Jamaa na ndom zake akaanza mchakato lakini dushe halikupita, ndipo akajuwa kuwa papuchi haijatumika kabisa...

Wakapanga siku nyingine, siku ile muda ulikuwa umeisha. Binti albino alikuwa bado anaishi kwa wazazi wake.

Siku ya ahadi kumbe yule binti alikuwa heat period, naye si mjuzi wa mambo hayo, akapeleka papuchi...

Jamaa alijiandaa kuitoa 'seal' ya albino huku tayari alikuwa ameshajisifia kwa marafiki zake...

Kweli, dushe siku hiyo likafanikiwa kupenya, hakuvaa ndom, kwa mzuka wareno hawakuchelewa...

Jamaa alirudi mtaani akijisifu kutimiza azma yake ya 'kugonga' sampuli nyingi za wanawake...

Baada ya miezi minne jamaa akatajwa na binti kwa wazazi wake kuwa ni muhusika wa ujauzito alionao...

Timu ya wazee wa Kisumbawanga ikaundwa, jamaa akatiwa mkononi, akawekwa kitimoto...

Lakini bahati nzuri alipewa option mbili...

Ya kwanza amuoe ama ya pili akubali kubeba ujauzito huo, akapewa siku saba za kufikiria ili atoe maamuzi...

Jamaa si akapuuzia...

Akasahau (sijui alijisahaulisha!)

Wale wazazi na wazee wa yule binti wala hawakumtafuta wala nini!

Baada ya mwezi yule jamaa tumbo lake likaanza kujaa [emoji1787]

Sumbawanga kiboko! Ni maeneo fulani njia ya kwenda Ziwa Tanganyika lakini ukifika somewhere Mtimbwa (sijui Mtimbwani) 5km kutoka njia kuu Sumbawanga - Mpanda road unachukua njia ya kulia, njia ya vumbi kabla ya kufika somewhere panaitwa Sintali...

Jamaa tumbo lilizidi kuongezeka, akaenda mwenyewe kwa wazazi wa yule binti...

Akaambiwa aende kesho yake...

Kesho mapema yule jamaa alienda pale na rafiki yake mmoja anayemuamini...

Alikuta tayari wazee wa mila wapo, binti yupo na wazazi pia...

Bottom line, ali-opt kumuoa yule bint...

Akaozeshwa kwa mila za Kifipa kwanza... Baadaye sana Kanisani...

Jamaa akapata mke namna hiyo.
___
Good side

Bahati nzuri yule binti alikuwa na upendo sana kwa yule jamaa, hivyo jamaa akajikuta amempenda mazima kikwelii siyo kwa kuigiza kama awali

Bado wanaendelea na maisha na wana watoto kadhaa.
******

James Jason
 
Yaan kama mtunzi usingekua wewe hii ningeita gahawa... Ila kwa heshima yako acha niweke akiba ya maneno...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama vile nimewahi kuisikia hii, kuna funzo hapa, ahsante
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama vile nimewahi kuisikia hii, kuna funzo hapa, ahsante
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…