Nimemsikiliza waziri,akilinganisha pesa alizolipwa mkandarasi katika mwaka mmoja wa SSH,na huko nyuma.
Pia mkandarasi abaye ni Arab Contractor ni taasisi ya serikali ya Misri ana mapungufu mengi mno,kalalamikiwa sana na Waziri Mkuu enzi za mjomba Magufuli hadi utawala huu wa Mama Samia.
Bado kuna huyo project consultant nae ni big issue.Utadhani amewekwa mfukoni na Mkandarasi.
Tanesco sio wa kumlaumu sana,tumesikia wanasiasa ndio wana kauli ya management ya Tanesco kila mara inabadirishwa.
Lakini yote haya mapungufu na kucheleweshwa mradi kukamilika,yawezekana yametokana na watawala kudhani mkandarasi huyo kujaza wataalamu wamisri wenye madegree ya Daktari kibao ndio kipimo au sifa kuu ya mkandarasi,hawakujua Misri hata bouncer ana degree tatu.