Howo Vs Scania

goja tblj amalizie
t blj karibu.
Sorry nilikuwa mbali na simu
Ni hivi 6x2 zipo aina mbili 1: mid lift , hii ni ile ambayo diff ipo nyuma , 2: tag axle , hii ni ile ambayo diff ipo kati.

Kwa maana nyingine ni kuwa mid lift na tag axle ni gari zenye matumizi tofauti kabisa , ila tag ina advantage za kufanya kaz za mid lift .
 
Vipi kuhusu single diff isiyo na axle ya kulift (middle /rear) , inaweza kuwa sawa na tag axle katika performance na je vipi kuhusu gari ya diff mbili, inaweza kulift diff moja mfano pulling nyingi huwa naona zimenyanyua axle moja ya gari mara nyingi ni rear axle ..nifafanulie tafadhali
 
Samahani kidogo, hii comparison liyoweka hapa nadhani ni irrelevant kabisa yaani unataka kulingaisha kweli kwamba ni brand ipi ina magari mengi zaid yaliyokufa paipo kuangalia mwaka wa kuanza matumizi wa brand hizo? huwezi kuwa sahihi.

Hebu nenda popote uniletee chinese brand yenye plate number inayoanzia na A inayofanya safari za masafa marefu. Lakini ukija kwa scania kuna gari zilitoka huko kwenye TZK na hadi leo zinatoboa kipush kama kawaida
 

Habari kiongozi, hongera kwanza kwa kuwaza kuingia katika mambo haya ya umiliki wa vombo vya usafirishaji. Kwa upande wangu nina experience kidogo katika sekta hii kwanza ya kuwa tingo kwa mwaka mmoja, trucker kwa miaka minne na pia miezi sita katika management ya kampuni inayojihusisha na trucking na maoni nitakayoyatoa hapa ni ktokana na experience hiyo na nitachambua kwa vigezo kadhaa vya ulinganishi na vigezo hivyo itakua kwa SCANIA USED with 400000 km vs HOWO 371 Brand new na makaratasi yake.

KDUMU/DURABILITY. Hapa katika kipengele hiki tunaona kuwa scania anaongoza kwani tunashuhudia kna scania ambazo zimeingia nchini miaka ya 90 na bado zinapiga kazi kisawasawa na kwa uwezo mzuri, lakini tafuta howo namba A uone kama ipo barabarani na hii ni kwa chise products zote japo zipo namab B pale kwa ALISTAIR zinajikongoja dar-tunduma zinatumia karibu wiki. ia katika body durability scania yupo vizuri kwani body zake zimetengenezwa kwa steel kwa sehemu kubwa wakati howo hawtumii steel katika undaji wa outer body hivo mibonyeo na kubanduka kwa sehemu za magari ni kawaida yao.

SYSTEMS OPERATION. Katika kipengele hiki nitagusia system za transmission na brakes. Kwa upande wa transmission tunaona kuwa scania sio msumbufu sana kulinganisha na Howo kwani ukileta scania na ukaifanyia overhaul sahau kuhusu major fails in transmission systems kwa ujumla lakini howo sasaaa ni kisanga ukiitembeza KMs 20,000 tu tayari majanga yanaanza kufuatana.

Katika brakes hapo scania huwa hana shida sana katika systems hiyo kwani unaweza kupiga brake ya ghafla katika mwendo mkali na ikkutii fresh tu hata kama kwenye trailer brakes hazipo fresh hata kama umeuma tani 40 lakini kwa uande wa howo mamaaa yangu piga kofi kidogo halafu pata dharula uhitaji brakes za ghafla ndo utafrahi kama uliondoka kwako bila kuaga.

COMFOTABILITY. Ktika hili tunona mazingira ya ndani ya gari jinsi yalivyo rafiki kwa operator yaai driver. Kwa pande wa scania ndani kuna viti vizuri vya upepo na kunesanesa hivyo kumfanya driver kutoumiza sana kiuno na mgongo pale gari inapokua katika ruoghu roads kwani kiti kinakua na shock absobers zinazo mlinda driver, pia ukibahatika scania zina vitanda vyenye godoro zuri na linalodumu kwa ajili ya mapumziko ya driver.

Upande wa howo ni maumivu kwani viti vyake ni kama vya magari ya mwendokasi yaani hazipo friendly kwa driver na hapo bado usukani, clutch, gear lever pamoja na eksileta ni ngumu sana kiasi kwamba zinaongeza uchovu kwa driver.

RETURN ON INVESTMENT (RoI). Hapa tunagalia ni gari ipi inaweza kurudisha haraka gharama za uwekezaji katika gari husika yaani gari lipi linaweza kurudisha gharama haraka. Kwa sehem hii nathubutu kusema kuwa zote scania na howo zina viwango sawa vya RoI kwani howo likiwa jipya na likipata driver mwenye sifa za kijinga linakwenda balaa kwa hiyo mzunguko wake unakua ni mzuri.

USHAURI WANGU SASA. Kwa upande wangu, ktokana na kwamba wewe ni mgeni kwenye sekta hii nunua tu R 420 kali yenye milliage isiyozidi 400000, ikifika peleka pale SAAB waifanyie manuva vuta kichaja chako BHACHU hapokenya piga kazi.

Lakini jambo muhimu la kuzingatia sana tena siku na mchaaa ni kuhakikisha tatizo lolote la kiufundi linaloripotiwa a driver linatatuliwa haraka iwezekanavyo pia hakikisha unajali maslahi ya trucker wako na pia epuka ile kasmba ya sisi wabongo ambapo mmiliki anajikuta yeye ndo fundi mkuu, chief procurer, mtu wa masoko, mkurugenzi mkuu na wakati huo huo ndo HR mkuu nakwambia hutofika popote.
Wasalaam.
 
Wewe SINOTRUCK inayozalisha malori ya Howo ni patnership ya nnchi za EU pamoja na China. Gari inatengenezwa kwa viwango vya kimataifa ndio gari no. Moja kwa ubora sasa.

Hapana mkuu hapa umetudanganya hivi hujui kuwa wakati akina iveco, scania,volvo, benzi na wkongwe wenzake wengine wapo na emissions za EURO 6, Howo na chinese wenzanke wapo na EURO 2?

Na kama hao akina howo ndo namba moja kwa uboro, ni lini iliingia au kushinda kwenye mtanange wa truck of the year tangu zianze kutengenezwa?? au wewe unauzungumzia ubora wa kujaza madereva maji ya mgongoni?
you cant be serious bro
 
Namba 1 kwa UBORO tena?
 
Asante sana broo. Nimependa huo ushauri wa kuipeleka SAAB.Pia kununua trailer from Kenya .Asante sana man
 
R420 isiyopungua km 400000?, that will be vey expensive bro,

Halafu iko hivi, kwenye haya magari latest yanayotumia electronic kwa kiasi kikubwa invest sana kwenye know how knowledge ,

Mara nyingi kinachosumbua huwa ni electronic parts na siyo mechanical parts, unapozungumzia km unazungumzia sana mechanical parts ie turbo rings and the likes , vitu ambavyo kwa scania henda hadi km milioni bila tatizo kama service itafuatwa vizuri , kinachosumbua ni electronic side , upande huu sasa hauna guarantee yoyote kama utakuwa abused, hata kama gari I km 0 kama Mtu ukiiabuse ika short circuit control box , jua ndio mwanzo wa gharama kubwa na zisizoisha

kiufupi ukitaka kumiliki.magari kama r420 jaribu kuwa na madereva wanaojua lugha vizuri. Hivo watajua na kuelewa kinachoandikwa kwenye dash board ,na miiko yake.
 
Mkuu you're a professional.
 
Anayetaka WOWO zipo zimepaki kwenye makampuni ya Ujenzi na uchimbaji madini kwa wachina wanaziuza zimetumika na wao wameshindwa kutengeneza. Product za wachina tuziogope hazidumu haswa kwa barabara zetu ni balaa
 
kama kweli nd kwanza unataka kuanza hiyo biashara achana na hizo habari za kununua mashine mpya alafu ni moja tu!

Hiyo biashara usijaribu kwa gari moja tu itakupasua kichwa inahitaji at least uwe nayo hata ma2 au3, chakufanya nunua tipa au vipisi vya scania320 au dizaini yoyote au mende used bei kw used ni 80-90M ,iweke chanja au tipa ndani ya mwaka tu pesa inarudi na faida unapata
 
Huo wingi wa scania zilizo juu ya Mawe vs Howo chache sio halisi. Scania ziko nyingi nchini kwa miaka mingi kwa hiyo tegemea kuziona nyingi zikiwa mbovu, Howo ziko chache kwa hiyo tegemea kuziona chache juu ya mawe.

Vv
 

Asante mkuu Kwa ushauri mzuri ulioutoa kuhusu Scania .Sasa mkuu mbona unanifanya nikate TAMAA, Uwezo wangu Ni kununua kichwa cha scania na trailer yake mkuu.

Kama ni kuongeza ingine Ni baadaye kidogo kaka

By the way ,thanks for the advice.
 
Asante mkuu Kwa ushauri mzuri ulioutoa kuhusu Scania .Sasa mkuu mbona unanifanya nikate TAMAA ,Uwezo wangu Ni kununua kichwa cha scania na trailer yake mkuu .Kama ni kuongeza ingine Ni baadaye kidogo kaka
By the way ,thanks for the advice.
nimekwambia 7bu ninao uzoefu japo c sana iyo pesa unayotaka kununua kichwa pamoja trailer unaweza ukapata vipisi viwili hadi vitatu vya scania vikiwa bado na hali nzuri kabisa na asikudanganye m2 tipa inaripa sana na haiumizi kichwa kuliko semi ikiwa moja peke yake ,ni ushauri tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…