Hello Great Thinkers.
Naomba kuuliza hivi hizi Tractor za kuvuta trailers Ni ipi bora zaidi kati ya hizi za kichina HOWO na Scania ,Ndio Naomba mungu mwaka huu ninunue kichwa kimoja kati ya hizi mbili ,ndio naanza hii biashara GT.Thanks a lot you guys.
Habari kiongozi, hongera kwanza kwa kuwaza kuingia katika mambo haya ya umiliki wa vombo vya usafirishaji. Kwa upande wangu nina experience kidogo katika sekta hii kwanza ya kuwa tingo kwa mwaka mmoja, trucker kwa miaka minne na pia miezi sita katika management ya kampuni inayojihusisha na trucking na maoni nitakayoyatoa hapa ni ktokana na experience hiyo na nitachambua kwa vigezo kadhaa vya ulinganishi na vigezo hivyo itakua kwa SCANIA USED with 400000 km vs HOWO 371 Brand new na makaratasi yake.
KDUMU/DURABILITY. Hapa katika kipengele hiki tunaona kuwa scania anaongoza kwani tunashuhudia kna scania ambazo zimeingia nchini miaka ya 90 na bado zinapiga kazi kisawasawa na kwa uwezo mzuri, lakini tafuta howo namba A uone kama ipo barabarani na hii ni kwa chise products zote japo zipo namab B pale kwa ALISTAIR zinajikongoja dar-tunduma zinatumia karibu wiki. ia katika body durability scania yupo vizuri kwani body zake zimetengenezwa kwa steel kwa sehemu kubwa wakati howo hawtumii steel katika undaji wa outer body hivo mibonyeo na kubanduka kwa sehemu za magari ni kawaida yao.
SYSTEMS OPERATION. Katika kipengele hiki nitagusia system za transmission na brakes. Kwa upande wa transmission tunaona kuwa scania sio msumbufu sana kulinganisha na Howo kwani ukileta scania na ukaifanyia overhaul sahau kuhusu major fails in transmission systems kwa ujumla lakini howo sasaaa ni kisanga ukiitembeza KMs 20,000 tu tayari majanga yanaanza kufuatana.
Katika brakes hapo scania huwa hana shida sana katika systems hiyo kwani unaweza kupiga brake ya ghafla katika mwendo mkali na ikkutii fresh tu hata kama kwenye trailer brakes hazipo fresh hata kama umeuma tani 40 lakini kwa uande wa howo mamaaa yangu piga kofi kidogo halafu pata dharula uhitaji brakes za ghafla ndo utafrahi kama uliondoka kwako bila kuaga.
COMFOTABILITY. Ktika hili tunona mazingira ya ndani ya gari jinsi yalivyo rafiki kwa operator yaai driver. Kwa pande wa scania ndani kuna viti vizuri vya upepo na kunesanesa hivyo kumfanya driver kutoumiza sana kiuno na mgongo pale gari inapokua katika ruoghu roads kwani kiti kinakua na shock absobers zinazo mlinda driver, pia ukibahatika scania zina vitanda vyenye godoro zuri na linalodumu kwa ajili ya mapumziko ya driver.
Upande wa howo ni maumivu kwani viti vyake ni kama vya magari ya mwendokasi yaani hazipo friendly kwa driver na hapo bado usukani, clutch, gear lever pamoja na eksileta ni ngumu sana kiasi kwamba zinaongeza uchovu kwa driver.
RETURN ON INVESTMENT (RoI). Hapa tunagalia ni gari ipi inaweza kurudisha haraka gharama za uwekezaji katika gari husika yaani gari lipi linaweza kurudisha gharama haraka. Kwa sehem hii nathubutu kusema kuwa zote scania na howo zina viwango sawa vya RoI kwani howo likiwa jipya na likipata driver mwenye sifa za kijinga linakwenda balaa kwa hiyo mzunguko wake unakua ni mzuri.
USHAURI WANGU SASA. Kwa upande wangu, ktokana na kwamba wewe ni mgeni kwenye sekta hii nunua tu R 420 kali yenye milliage isiyozidi 400000, ikifika peleka pale SAAB waifanyie manuva vuta kichaja chako BHACHU hapokenya piga kazi.
Lakini jambo muhimu la kuzingatia sana tena siku na mchaaa ni kuhakikisha tatizo lolote la kiufundi linaloripotiwa a driver linatatuliwa haraka iwezekanavyo pia hakikisha unajali maslahi ya trucker wako na pia epuka ile kasmba ya sisi wabongo ambapo mmiliki anajikuta yeye ndo fundi mkuu, chief procurer, mtu wa masoko, mkurugenzi mkuu na wakati huo huo ndo HR mkuu nakwambia hutofika popote.
Wasalaam.