Kuna wengi hapa ukiwauliza Hoyce Temu amefanya makosa gani, hawajui. Lakini wanamshushia rungu!
Wengine hapa lawama zao zinasomeka kana kwamba aliiba pesa.
Mfano kosa LA kuvujisha siri za shirika. Ni nani hajawai kufanya ili kosa? Hata huyo aliyempa dada wa Taifa siri za Hoyce amefanya kosa hilo hilo!
Nitoe tu angalizo Kwa wale ambao tupo kwenye vibarua vya kuajiriwa.
Tusijisahau sana, tukumbuke taratibu na miiko ya kazi, nimesoma hayo maamuzi ya kesi ya dada yetu nikaona jinsi ambavyo mambo madogo yanaweza kukuweka matatani.
Kama ulivyosema, wengi wanalaumu na kumrushia maneno dada wa watu bila kujua shida Iko wapi, wengine wameenda mbali kuhusisha umiss, uchaga na hili sakata.
Kwa ufupi, Hadi kufikia hapo, ni yeye alikata rufaa dhidi ya maamuzi ya kesi yake iliyomfanya akapiteza ajira pamoja na kutokupatiwa likizo ya uzazi. Huo mchuano umeenda Hadi kufika Kwa katibu mkuu wa UN. Lakini hayo ni mambo yalitokea huko awali sema kumbe alikua anaendelea kupambana chini Kwa chini, nafikiri alishauriwa vibaya na utakuwa alilenga apate fidia Kwa maamuzi ya kuonewa.
Nikirudi kwenye ushauri Kwa sie tuliopo kwenye vibarua kuzingatia miiko ya kazi, unaona kabisa inakatazwa kufanya kazi nyingine nje ya ajira Yako bila kutoa taarifa Kwa mwajiri wako, hata kama haulipwi, lazima utoe taarifa waone kama hakuna muingiliano wa kimaslahi.
Utaona aliendelea na vipindinvyake vya watu wenye shida channel ten na haikua na tatizo Kwa vile alitolea maelezo na kupata kibali Cha mwajiri.
Tumeona kesi ya EFM, mwajiri anasisitiza hayo ni maoni ya mfanyakazi binafsi na sio kampuni au taasisi ya EFM.
Mambo ya kutumia email ya ofisi Kwa vitu binafsi napo haijakaa vizuri, Iko siku linaweza kutokea jambo ukaingia matatani. Uchunguzi wa Hawa jamaa hua sio wa kubahatisha, wanafukua Kila kitu.
Wanaweza kuondoka Hadi na hard disk kwenda kufanya investigation zao, ukiweza, mambo binafsi fanyia kwenye vitendea kazi vyako ambavyo havihusiani na vile vya ofisi.