Huba Series ndani ya maisha bongo dstv - imekosa mvuto kwa story zisizo na uhalisia katika mazingira ya kawaida

Huba Series ndani ya maisha bongo dstv - imekosa mvuto kwa story zisizo na uhalisia katika mazingira ya kawaida

Bongo film industry inaendeshwa na Ngumbaru wenzetu so utegemee jipya
 
Binafsi mimi ni mzalendo na nnapenda sana kufuatilia tamthilia za hapa bongo mara moja moja pindi nkipata nafasi nkiwa home,

Kuna hiI Huba series inayorushwa DSTV (Maisha Magic bongo) ni ya muda mrefu sana, na imepewa airtime week nzima kuanzia J3 - Ijumaa, Hii series mwanzoni iliteka sana mashabiki wanaopenda kuangalia tamthilia za bongo, ila siku za hivi karibuni imepoteza mvuto kwa kiasi kikubwa kutokana na aina ya story zisizo na uhalisia katika maisha ya kawaida ambazo wanazitengeneza lengo ikiwa ni kuvuta muda series izidi kuonekana ndefu.

Kwanza kitu kinachonshangaza kule ndani kutokana na story yao, kila mtu amesha date na kila mtu kule ndani

Mfano
Kibibi, ameshatoka na Davy,Chidi na Fabrizo
Tima, ameshatoka na Davy, Jude na Jay B
Nelly,ameshatoka na Davy, Jay B na Abby
Happy, ameshatoka na Chidi na JB
Nikole, ameshatoka na Kashaulo, Davy, Jude na Jb
Tesa, ameshatoka na Kashaulo na Roy (ambae ni mwanaye)
Monica, ashatoka na Fabrizo
Sidi, ameshatoka na Kashaulo na JB

Sasa kutokana na huu muingiliano wa hawa watu, series inakosa muelekeo na mvuto kabisa

Au wakuu mnasemaje 😃😃😃😃😃
Nikipataga muda huo bora nicheki Safari Chanel
 
Watu kuachana na kurudiana hovyohovyo,watu kuingia kwenye mapenzi na huyu kesho na yule inafundisha nini eti?yaani lengo la tamithilia ni nini?
Mpali wanajitahidi sana na ina uhalisia,ni aibu kwa mkongwe kama jb kuendelea kuigiza tamithilia ya vile ambayo lengo lake hata halijulikani
 
Watu kuachana na kurudiana hovyohovyo,watu kuingia kwenye mapenzi na huyu kesho na yule inafundisha nini eti?yaani lengo la tamithilia ni nini?
Mpali wanajitahidi sana na ina uhalisia,ni aibu kwa mkongwe kama jb kuendelea kuigiza tamithilia ya vile ambayo lengo lake hata halijulikani
Yani ni ya hovyo mnoo , Nafkir wengi pale wameenda kuvuna Mpunga hakuna kingine

Hiyo Mpali ni tamthilia nzuri sana, Naipenda sana, Wa zambia wako serious na mambo yao
 
Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mheshimiwa Rais ....
 
Yaani yaaani yaaani..lawama napeleka kwa ma director..

Serious bongo hapa hatuna ma director makini..

Ila tuna ma camera man tuuu
Pia hawa ma camera man wetu wanacheza na mind za wamama wa nyumbani si unajua wanapendaga vi drama vya ajabu ajabu..

Na soon nakuja ku change soko la movie hapa bongo..

Dua zenu wakuu....
Am caming Director subirini kuona vtu vikali..

Bongo sio waigizaji hakuna wapo wa kutosha ishu ni ma director hatuna...

Na waliopo wachache wanafanya kazi kimazoea an mtu director sio by proffesional ila ni alikua mshika camera kwa kina mussa banzi

If you're up for the challenge go for it. Tatizo la hii nchi kila mtu anapenda kulalamika fulani hajafanya this or that as if wao wamekatazwa kufanya hiyo kazi. Lalamika, toa solution au chukua hatua. Kulalamika tu is cheap.

Unakuta mtu hajasoma analalamikia wasomi as though yeye alikatazwa kusoma au kujiendeleza. Ni ujinga.
 
Back
Top Bottom