Hubert Velud ni kocha mpya wa Simba Sports Club kutoka Ufaransa

Hubert Velud ni kocha mpya wa Simba Sports Club kutoka Ufaransa

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
866e92e99e045c1e390866602f454437.jpg
62c9a5cb7191a981c5a2fb8af2bda3c5.jpg
d785ff15f853ccb3f3f626919657f8f7.jpg
Kocha mpya wa klabu ya Simba Sports Club kutoka Ufaransa anaitwa Hubert Velud, ambaye anatarajiwa kumrithi Joseph Omog aliyetimuliwa kazi Desemba 23, mwaka jana.

Kocha huyo imeripotiwa kwamba tayari ameshakubaliana kimsingi kujiunga na Simba Sports Club baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo.

Velud alikuwa kwenye bechi la ufundi la klabu ya FC Paris ya Ufaransa na anahusika kuibua na kukuza vipaji vya vyote wanaotamba ulaya, akiwemo mchezaji wa zamani wa Liverpool ambaye sasa yupo Crystal Palace zote za England, Mamadou Sanko na Lassana Diara aliyewahi kutamba Chelsea, Arsenal, Portsmouth na Real Madrid.

Mchezaji mwingine aliyepikwa na Velud wakati akikinoa FC Paris ni Gabriel Obertan aliyewahi kuchezea timu za Bordeaux, Lorient, Manchester United Newcastle United Wigan Athletic na nyinginezo.

Velud ndiye alikuwa kocha mkuu wa timu ya Togo kuanzia 2009 - 2010 cha akina Emmanuel Adebayor, Kilichoshambuliwa kwa risasi kilipokuwa kikisafiri kwa barabara kwenda Angola kwenye fainali za kombe la Afrika (Afcon).

Hubert Velud amewahi kuzinoa klabu mbalimbali kwa mafanikio barani Afrika zikiwemo Toulon, FC Paris, Chalons-sur-Marne, Beauvais zote za Ufaransa TP Mazembe Englebert ya Congo DRC, Etoile du Sahel ya Tunisia, Es Settif na USM Alger za Algeria, pamoja na timu ya Taifa ya Togo

Baadhi ya mataji aliyotwaa;

Kocha huyo alifanikiwa kutwaa mataji kadhaa akiwa na timu mbalimbali, likiwemo la Ligi ya Algeria maarufu kama Ligue 1 mwaka 2013 akiwa na Es Settif, Super Cup ya Algeria 2013 akiwa na USM Alger na kubeba tena ubingwa wa Ligue 1 akiwa na kikosi cha USM Alger.

Kwa rekodi hizi, inaonyesha wazi kocha huyo ni mzoefu mwenye uwezo wa kuifikisha mbali Simba SC, zaidi ikiwa ni kuwapa mataji ya ndani na nje ukizingatia ni mwenyeji wa soka la Afrika.
 
Soka la Bongo linahitaji kuwa na mashabiki kama wa Arsenal
 
Tatizo la soka la bongo akina Manara ndio wanapanga vikosi na ndio wanachagua mchezaji wa kusajiri.......kocha anakuwa yupoyupo tu.
 
Very soon utasikia hanz popo anampangia kikosi, akibisha tuu anapigwa fitna na kufukuliziwa mbali, kisha anatafutwa mwingine
 
Hawa viongozi ndio wanafundisha wachezaji kugoma kwa kocha kucheza chini ya kiwango ili kushinikiza jambo Lao
Sasa hapo mimi naona tatizo ni mchezaji. Kama huna lengo la kucheza soka nje ya nchi basi utawasikiliza hao viongozi, wachezaji wetu hawajutumi mkuu tofauti na timu nyingine
 
Back
Top Bottom