Huduma gani ikitolewa bure na Serikali haitaathiri uchumi wetu?

Huduma gani ikitolewa bure na Serikali haitaathiri uchumi wetu?

kwangu mm ni hizi hapa
1.vipimo vya afya
2.maji

ni mawaza yangu tu
Hivyo vipimo vinatoka wapi?Havinunuliwi?Na mchakato wa maji lazima fedha,nguvu na wakati vitumike.
Au unataka kutueleza kipi hapo?Kuathiri uchumi wa serikali yetu au uchumi wa mtu mmojammoja?Kichwa cha habari yako ni cha utata kidogo.
 
Yan upewe bure huduma ya maji? Unajua gharama zake? Unajua hiyo huduma imeajiri na kulisha familia ngapi? Kupitia hizo ajira zinachangia kiasi gani serikalini?

Sio tu Maji hata hiyo huduma ya vipimo vya afya jiulize hayo maswali pia.
Sasa kuacha watu wanakunywa maji ya kinyesi si ndio mbaya zaidi? Hospitali zinajaa wagonjwa na kuongeza gharama kwa serikali ya mama
 
Nchi hii kama viongozi wataacha kujinufaisha wao tu serikali inaweza kutoa huduma zote za msingi bure kama afya na elimu ila waache matumizi ya anasa kama kununua magari ya kifahari na maposho makubwa,sijui kuwalipa wenza wa viongozi kwani aliyekuwa akiitumikia serikali ni mume au mke tu huyo mwenza wake atamtunza mwenyewe labda iwe kwa dharura lakini isiwe ni wajibu wa serikali.
Tuwe wakweli tu kila bajeti ya serikali ikipangwa viongozi wamekuwa wakijipendelea sana.
 
Kwangu mimi ni hizi hapa
1. Vipimo vya afya
2. Maji

Ni mawaza yangu tu
3. Kutembelea makumbusho bure Kwa wazawa
4. baadhi ya mbuga za wanyama kuwa free Kwa wazawa kutembelea
5.Mwendokasi na treni kubeba wanafunzi bure
 
Ni huduma ya matibabu ya afya yote kwa ujumla!

Afya ni muhimu zaidi kwa maendeleo ya jamii yetu!
 
Back
Top Bottom