Huduma gani ikitolewa bure na Serikali haitaathiri uchumi wetu?

Ongezeni tozo mtakavyo ila mkifanya haya kweli nitaamini Tanzania tunaweza na Tanzania litakuwa taifa la kuigwa ulimwenguni kote
-Elimu bure hapo tumeweza✔️
- Umeme bure
-Huduma za Afya bure
Walao tukifanikiwa katika mawili hapo juu basi Taifa hili litakuwa la kipekee sana hapa duniani

Siyo lazima tufanye yote kwa mkupuo, tukimaliza moja tunaanza lingine hata baada ya miaka mitano tukifanya moja ni maendeleo makubwa sana kitaifa, walao hadi 2035 tuyakamilishe hayo

NB Vyanzo vipya vya mapato vibuniwe ili kufidia gharama za huduma zitakazo tolewa bure. Mfano wa vyanzo hivyo ni
- Kuanzisha kiwanda cha kuunda simu, ili serikali ikusanye mapato ya kutosha baada ya kuuza simu hizo ndani na nje ya nchi
- Vyeti vyote vya ndoa vitolewe na serikali pekee, na ili kupata cheti hicho walao mhusika itabidi achangie kuanzia tsh laki moja kupitia mfumo rasmi wa kimtandao utakao wekwa
- Makanisa na misikiti yote wanapaswa kulipia kodi maana ni huduma hizo, walao kila kanisa/ msikiti wachangie kima cha chini 15000tsh kulingana na ukubwa wa kanisa/msikiti kwa mwezi na kwa makanisa makubwa au misikiti mikubwa wachangie 30000-40000tsh kwa mwezi

Ni hayo tu kwa leo,
Mpenda maendeleo
 
Yan upewe bure huduma ya maji? Unajua gharama zake? Unajua hiyo huduma imeajiri na kulisha familia ngapi? Kupitia hizo ajira zinachangia kiasi gani serikalini?

Sio tu Maji hata hiyo huduma ya vipimo vya afya jiulize hayo maswali pia.
Bure haimaanishi ya kwamba uzalishaji wa huduma ni bure anachomaanisha ni kwamba serikali ikiwa na jukumu la kwapunguzia wananchi mzigo wa gharama za maisha basi inaweza kusambaza baadhi ya huduma za kijamii bila kulipia. Nchi kama Norway huduma za matibabu ni free hii haimaniishi kwamba madokta wanajitolea isipokua ni serikali ndio inabeba izo gharama za uendeshaji. Malipo ya wabunge yakipunguzwa mpaka kima cha mishahara ya wafanyakazi wa kawaida, ripoti za CAG zikifanyiwa kazi na waliofuja mali za umma kuchukuliwa hatua mfano kurudisha pesa walizochota au kutaifisha mali zao na serikali ikiacha matumizi ya anasa mfano uagizaji wa magari kila mwaka mbona pesa itakayopatikana inatosha kabisa kusambaza huduma ya maji kwa wananchi bila malipo. Tatizo ni vipaumbele, uwajibikaji na uweledi tu wala sio gharama za uendeshaji.
 
Hivyo vipimo vinatoka wapi?Havinunuliwi?Na mchakato wa maji lazima fedha,nguvu na wakati vitumike.
Au unataka kutueleza kipi hapo?Kuathiri uchumi wa serikali yetu au uchumi wa mtu mmojammoja?Kichwa cha habari yako ni cha utata kidogo.
Nchini Ireland hakuna bill ya maji, maji ni bure. Tunaweza kujifunza kutoka kwao, Scotland bill ya maji hakuna ila unapolipa Council Tax kuna kiasi cha pesa kinapelekwa Idara ya Maji.
 
hapa nchini kwetu hata baadhi ya wananchi wenzetu fikra na mawazo yao yamekaa poa poa tu. achilia mbali hiyo serikali
 
Bure haimaanishi ya kwamba uzalishaji wa huduma ni bure anachomaanisha ni kwamba serikali ikiwa na jukumu la kwapunguzia wananchi mzigo wa gharama za maisha basi inaweza kusambaza baadhi ya huduma za kijamii bila kulipia. Nchi kama Norway huduma za matibabu ni free hii haimaniishi kwamba madokta wanajitolea isipokua ni serikali ndio inabeba izo gharama za uendeshaji. Malipo ya wabunge yakipunguzwa mpaka kima cha mishahara ya wafanyakazi wa kawaida, ripoti za CAG zikifanyiwa kazi na waliofuja mali za umma kuchukuliwa hatua mfano kurudisha pesa walizochota au kutaifisha mali zao na serikali ikiacha matumizi ya anasa mfano uagizaji wa magari kila mwaka mbona pesa itakayopatikana inatosha kabisa kusambaza huduma ya maji kwa wananchi bila malipo. Tatizo ni vipaumbele, uwajibikaji na uweledi tu wala sio gharama za uendeshaji.
Umeeleza vizuri tu. Lakini mimi sishauri hizi huduma zitolewe bure kwa sababu ya nature ya watoa huduma na wapokea huduma. Hizi huduma zikitolewa bure kutatengeneza conflict kubwa kati ya taasisi. Hata kama hela akatwe nani bado watu wanapaswa kuzilipia hizi huduma
 
Hakuna mabadiliko yasiokua na misukosuko lakini baada ya muda watu watazoea na hali itakua shwari, leo usafiri wa mbagara hata uongeze daladala 100 za kupanda bure mwanzoni watu wataendelea kugombaniana tu kwa sababu saikolojia yao ishakua programmed kwamba huo ndio utaratibu wa kila siku ila hali ikizoeleka watajua mabasi yapo mengi wataanza kuingia kistaarabu hata makato ya tozo kwenye mihamala ya simu yalivyokua introduced raia walipiga kelele lakini sasa hivi wametulia na bado tuzo tunaishi nazo kama tumezoea kukatwa tozo tutashindwa vipi kuzoea kupewa huduma bure? Serikali ambayo inawajibika kuwapunguzia wananchi wake mzigo wa gharama za maisha ikiamua kutoa izo huduma bure ni sawa kabisa. Kuna matumizi mengi sana ya anasa serikalini, kuna ufisadi mkubwa sana serikalini, kuna mlundikano mkubwa sana wa vyeo visivyokua na ulazima au vinaingiliana majukumu. Hayo yote yakirekebishwa basi sio maji tu pia zipo huduma nyingi serikali inaweza kuzitoa bure mfano elimu bure mpaka chuo kikuu, usafiri wa umma bure n.k. ni suala la uwajibikaji na kuchagua vipaumbele tu.
 
Wakiruhusu makampuni mbalimbali kuwekeza kwenye sekta ya nishati umeme italeta ushindani na kupunguza kero ya nishati umeme kwa wananchi.
 
Hakuna mabadiliko yasiokua na misukosuko lakini baada ya muda watu watazoea na hali itakua shwari, leo usafiri wa mbagara hata uongeze daladala 100 za kupanda bure mwanzoni watu wataendelea kugombaniana tu kwa sababu saikolojia yao ishakua programmed kwamba huo ndio utaratibu wa kila siku ila hali ikizoeleka watajua mabasi yapo mengi wataanza kuingia kistaarabu hata makato ya tozo kwenye mihamala ya simu yalivyokua introduced raia walipiga kelele lakini sasa hivi wametulia na bado tuzo tunaishi nazo kama tumezoea kukatwa tozo tutashindwa vipi kuzoea kupewa huduma bure? Serikali ambayo inawajibika kuwapunguzia wananchi wake mzigo wa gharama za maisha ikiamua kutoa izo huduma bure ni sawa kabisa. Kuna matumizi mengi sana ya anasa serikalini, kuna ufisadi mkubwa sana serikalini, kuna mlundikano mkubwa sana wa vyeo visivyokua na ulazima au vinaingiliana majukumu. Hayo yote yakirekebishwa basi sio maji tu pia zipo huduma nyingi serikali inaweza kuzitoa bure mfano elimu bure mpaka chuo kikuu, usafiri wa umma bure n.k. ni suala la uwajibikaji na kuchagua vipaumbele tu.
Hivi umekomaa kabisa uko serious unataka huduma ya maji bure? Issue sio kuwa programmed au vipi issue ni kwamba huduma unayopata inagharamiwa na sio kugharamiwa tu inataka maintainance ya mara kwa mara bila hivyo hupati huduma. Elimu ni rahisi kwa sababu anayesoma halipi kodi lakini mtu unafanya kazi bado upate huduma ya maji bure. Ungeniambia afya kidogo ningekuelewa lakini huduma ya maji, nitakupinga
 
Maji imetolewa kama mfano tu lakini sio lazima iyo huduma ya bure iwe maji inaweza ikawa huduma yoyote ambayo serikali inaweza kumudu. Hata ivyo embu tubaki hapo hapo kwenye maji nipigie hesabu ya bajeti ya kusambaza maji pamoja na maintanance costs zake tuone inakuja shilingi ngapi kwa mwaka na mimi nikupigie hesabu ni masuala yepi serikali ikayafanya hicho kiasi cha bajeti ya maji kinaweza kupatikana.
 
Kama serikali itaamua kubana matumizi yasiyo na tija basi ibane ipeleke kuanzisha miradi mingine watu wafaidike na sio kubana ili watu wapate huduma ya maji bure. Hiyo HAPANA mkuu
 
Kwamba huduma ya maji haina tija? Point yako ni kwamba gharama za uendeshaji na usambazaji wa huduma ya maji ni kubwa kwaiyo hazitakiwi kutolewa bure, mimi nikakwambia nipe bajeti ya maji na mimi nikuonyeshe ni kwa namna gani serikali inaweza ku-adjust mambo hicho kiasi cha bajeti kikapatikana. Suala ni vipaumbele, iwajibikaji na uweledi tu wala sio gharama za uendeshaji. Kati ya upatikanaji wa maji na manunuzi ya ndege kipi kipaumbele chenye tija? Lini wananchi wa Tanzania washawahi kuwa na hitaji la usafiri wa ndege?
 
Kwangu mimi ni hizi hapa
1. Vipimo vya afya
2. Maji

Ni mawaza yangu tu
Elimu ya Msingi na Sekondari; na ambavyo tayari hata sasa ni vya bure. Aidha huduma kama hii kutolewa bure siyo tu kwamba haiathiri uchumi, wa Nchi bali inaongeza uchumi wa Nchi
Mungu aendelee na Mama kwa kishindo kikuu
 
Labda ungesema vitolewe kwa gharama nafuu ila sio bure kwani mchakato wake unagharama pia
 
Back
Top Bottom