KERO Huduma kwa wateja UTT Amis ni mbovu, simu zinakatwa au hazipokelewi kabisa na kwenye mitandao ya kijamii hawajibu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hilo pia limewahi kunifikirisha πŸ˜ƒ
Maana mashirika na mifuko ya nchi ile haiaminiki.
 
Hata mifuko ya pension iko nchi nyingi sana duniani na inafanya vizuri ila kwa hii nchi yetu nadhan unaona changamoto wastaafu wanazopitia kupata stahiki zao.
UTT Amis wamewekeza vigogo ngumu kufa.
 
Basi ni bora wasihangaike kuweka namba za simu....waseme ukitaka huduma yao nenda ofisini kwao ....kuliko kuweka namba nyingi ambazo hazina maana kabisa. Inaboa sana.
 
Hii ni kweli na hata ofisini pia huduma ni mbovu. Arusha, pale ngorongoro ukiwakuta wale wadada wawili utatamani kulia, wanakuhudumia wanapotaka wao tena kama vile kwenda kwako pale ni kuwasumbua.
 
Hao jamaa ni wapuuzi, mimi nilishachukua na form pale Mwanza niweke 30m. Nikaenda mara nerwork hakuna. Naingia kwenye App inaload tu. Nikaenda kwa wakala CRDB fyoko fyoko tu. Nikaona hawana time nikabidi niende BOT kuchukua T-bill. Nadhani wameridhika na mishahara
 
Wadau mtandao wa utt amis upo down au ni kwangu tu
 
UTT-AMIS haina ubaya wowote, mifuko kama UTT iko duniani kote. Suala la simu ni uzembe umejaa karibu taasisi zote za umma.
Bora wewe una uelewa ,Kuna kitu kinaitwa mutual funds and hedge funds wengi hatujui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…