KERO Huduma kwa wateja UTT Amis ni mbovu, simu zinakatwa au hazipokelewi kabisa na kwenye mitandao ya kijamii hawajibu

KERO Huduma kwa wateja UTT Amis ni mbovu, simu zinakatwa au hazipokelewi kabisa na kwenye mitandao ya kijamii hawajibu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ewaa. Na mimi ndiyo hasa wasiwasi wangu. Kama wana uzembe wa kujibu simu kama taasisi zote za umma, huoni kuwa wana elements nyingine zote zinazopatikana kwenye mashirika ya umma? Yaani mimi nilihoji hili hili i.e. karibu taasisi zote za umma zilizoanzishwa zilifeli, hii ina nini speacial ili iaminiwe? Asante sana kwa kuthibitisha kuwa kumbe hata uzembe wa kupokea simu ni walewale.
Hilo pia limewahi kunifikirisha 😃
Maana mashirika na mifuko ya nchi ile haiaminiki.
 
Hata mifuko ya pension iko nchi nyingi sana duniani na inafanya vizuri ila kwa hii nchi yetu nadhan unaona changamoto wastaafu wanazopitia kupata stahiki zao.
UTT Amis wamewekeza vigogo ngumu kufa.
 
Basi ni bora wasihangaike kuweka namba za simu....waseme ukitaka huduma yao nenda ofisini kwao ....kuliko kuweka namba nyingi ambazo hazina maana kabisa. Inaboa sana.
 
Habari ndugu wadau!? Kuna nini kinaendelea kwenye mifuko ya uwekezaji UTT Amis?

Huduma zao kwenye upande wa kupokea simu imekuwa ni janga, hazipokelewi ziadi ya kukatwa. Hii inatia wasiwasi kwa watu tuliopo mbali na ofisi zao hatujui kinachoendelea kuhusu pesa zetu, lakini pia maswali mengi ambayo tunayo hayajibiwi kwa wakati, wakati simu zao wameweka na wameahidi kupokea na kujibu hoja za wateja wao.

Shida haiishii hapo, hata ukija kwenye mitandao yao ya kijamii utaona wanapost zao mpya kila siku lakini ukihoji nini kinaendelea, kwa nini customer care imekuwa chini hakuna anyejibu. Watujulishe wadau kama huduma ya simu haipo tena ili tujue inatulazimu kufika ofisini kwao hata kwa mambo madogo.
Hii ni kweli na hata ofisini pia huduma ni mbovu. Arusha, pale ngorongoro ukiwakuta wale wadada wawili utatamani kulia, wanakuhudumia wanapotaka wao tena kama vile kwenda kwako pale ni kuwasumbua.
 
Hao jamaa ni wapuuzi, mimi nilishachukua na form pale Mwanza niweke 30m. Nikaenda mara nerwork hakuna. Naingia kwenye App inaload tu. Nikaenda kwa wakala CRDB fyoko fyoko tu. Nikaona hawana time nikabidi niende BOT kuchukua T-bill. Nadhani wameridhika na mishahara
 
Wadau mtandao wa utt amis upo down au ni kwangu tu
 
UTT-AMIS haina ubaya wowote, mifuko kama UTT iko duniani kote. Suala la simu ni uzembe umejaa karibu taasisi zote za umma.
Bora wewe una uelewa ,Kuna kitu kinaitwa mutual funds and hedge funds wengi hatujui
 
Back
Top Bottom