Huduma kwa wateja ya Air Tanzania siyo nzuri

Huduma kwa wateja ya Air Tanzania siyo nzuri

Kaka sasa tutaishi maisha ya connection kwenye swala kama hili huoni kama.ni rushwa hiyo??Why connection??Huoni kama ni mbaya sanaa....Yaani ni book ticket na nilipe hela na nahitaji connection kweli ni sawa??
Mkuu ukitaka usihangaike tafuta connection mbali na hapo endelea kukomaa
 
Hili shirika liliisha kufa kuanzia miaka 70. Ufanisi ni zero na ufatiliaji ni zero.

Zamani hupati ticket unaambiwa ndege imejaa mpaka utoe chochote na watu wengi wanakosa tiket lakini ukipanda ndege unakuta kuna viti vitupu!!

Wafanya kazi wa serikali na taasisi na mashirika ya serikali wanatuangusha sana watanzania.
Inafaa kuanzisha kazi za mikataba ya muda maalum na sio kazi za maisha na mfanyakazi akiwa goigoi ndio kwa heri muda ukiisha.
 
Hao ATCL customer service yao ni utopolo mtupu, ingawa saivi nina connection ila back then nimewahi kupata tabu sana kwenye ishu ya kukata ticket.
Tiketi si inakatwa online dakika sifuri tu
 
Ongeeni na watu vizuri jengeni mahusiano yenye faida mimi swala la kupata tabu sehemu labda kama sina connection napo na hata kama sina ninayemjua najitahidi kuwa mchangamfu tabasamu la kutosha na kuongea vizuri na wahudumu ukiona mtu analalamika kweli kuna matatizo ila ushajua nchi yetu ni ya kuzingatia mambo fulani kwann usijiongeze......
Ujiongeze kwenye huduma ya kulipia...? Only in Tanzania mashirika mengine ya kimataifa hayapo hivyo kabisa...hata kwenye response yao ukiwa emergency wapo faster sana ...kuliko huduma za hapa nyumbani...!

Kwakweli tuna safari ndefu sana...!​
 
Serikali ikaribishe wawekezaji wengine nchini kwenye sekta ya anga kuleta ushindani. leo hii hakuna usafiri wa ndege Mza- Dodoma hii siyo sahihi.
 
Back
Top Bottom