Youngblood
JF-Expert Member
- Aug 1, 2014
- 19,433
- 56,810
Utangulizi.
Kumekua na malalamiko mengi pamoja na changamoto katika huduma ambazo zinatolewa kwe Taasisi na Mashirika ya serikali kama vile elimu duni katika shule za umma, matibabu duni na ukosefu wa vifaa katika hospitali za umma, taasisi za fedha, mifuko ya hifadhi za jamii,vyombo vya usafiri na vyombo vya habari kama TBC na Magazeti.
Huduma zinazotolewa katika taasisi nyingi sio za kiwango cha kuridhisha ukilinganisha na huduma ambazo zinatolewa katika Taasisi binafsi kama vile Hospitali Binafsi au shule Binafsi,,mifano iliyo hai ni upungufu wa madawa na huduma mbovu katika hospitali za serikali,elimu iliyo chini ya kiwango katika shule za serikali pamoja na ukosefu wa vifaa vya kufundishia, madawati, usafiri wa wanafunzi Pamoja na vyoo bora,huduma duni za kijamii kama zimamoto,maji, barabara mbovu nk..
Sababu zinazochangia huduma mbovu katika taasisi na mashirika ya Umma
1. Uzembe- Kumekua na uzembe miongoni mwa watendaji wa serikali kutokana na usimamizi duni au kutokua na ufuatiliaji wa utendaji kwa kila mfanyakazi Pamoja na kukosekana sera nzuri ya kuwawekea malengo ya muda maalumu(target) au mpango kazi wa muda maalumu(work plan) itakayowaongoza watendaji katika kutekeleza majukumu yao. mfano ni kawaida kukuta suala la Fedha zilizotengwa kwa ajili ya kazi Fulani haijatumika katika kipindi kilichopangwa kutokana na sababu za kizembe kama kusubiri maagizo kutoka juu, kukosekana kwa wakandarasi au kukosekana kwa usimamizi.
2. Uduni wa huduma za teknolojia na mawasiliano katika taasisi nyingi za serikali, hivyo kufanya watu kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ambazo zingetatuliwa kisayansi,mfano ukienda katika kituo cha polisi utaambiwa nenda ukatoe nakala ya kitambulisho nje ya kituo, wakati mwingine wananchi wanakosa huduma kwa wakati kutokana na mitandao kuwa chini au barua pepe hazifunguki, kwa lugha nyingine Taasisi nyingi za serikali bado zinafanya kazi katika analojia.Mfano maombi ya ajira kwa njia ya posta,kutokuwepo na tovuti na namba za simu katika taasisi nyingi za serikali na hata namba zinapowekwa wakati mwingine hazipatikani au hazipokelewi hivyo waombaji wanashindwa kupata ufafanuzi wa maswali au utata unaojitokeza
2. Maslahi mabovu ya watumishi jambo ambalo linaondoa motisha au ari ya kufanya kazi kwa ufanisi, mfano watumishi katika serikali za mitaa (Tamisemi) ambako shughuli nyingi za serikali zinaanzia katika ngazi hiyo. Malimbikizo ya mishahara,madeni na kutokulipwa kwa stahiki mbalimbali za watumishi na vitisho kutoka kwa viongozi vinapunguza ari ya watumishi kufanya kazi hivyo kupelekea huduma duni! Wakati mwingine watumishi wanatumia muda wao wa kazi kujitafutia kipato cha ziada, mfano waalimu wengi sikuhizi wanatengeneza bidhaa kama karanga, barafu, au vitafunwa wanakwenda navyo shuleni kwa ajili ya kuwauzia wanafunzi, ukienda katika hospitali za serikali manesi wanauza bidhaa kama nepi,nguo za watoto, khanga kwa ajili ya wajawazito au taulo za kike, kwa mtindoi huu juda mwingiu wanapoteza kutangaza biashara zao kwa wagonjwa badala ya kuwahudumia wagonjwa.
3. Uchukuaji na uchepushaji fedha za miradi na mashirika mbalimbali na kuzipeleka katika matumizi mengine. Mfano pesa katika mifuko ya hifadhi ya jamii NSSF, PSSSF,na NHIF hali ambayo husababisha Uhaba wa fedha za uendeshaji katika taasisi husika hivyo kufanya kushindwa kutoa huduma zilizo bora na za kiwango.
4. Kutofuata sheria na kanuni zilizowekwa katika kutekeleza mipango mbalimbali ya serikali.,mfano kutofanyika upembuzi yakinifu au tathmini ya athari za mazingira kabla ya kuanza kwa miradi mikubwa,hivyo kupelekea serikali kuingia gharama katika uendeshaji.
5. Sheria na kanuni ambazo haziendani na uhalisia wa utendaji serikalini kama vile kuwapatia mikataba wazabuni wasio na Vigezo. Mfano ili kukabiliana na ukosefu wa dawa kutoka Bohari ya madawa MSD, serikali imeingia mikataba na wazabuni mbalimbali pasipo kujiridhisha ili hospitali za serikali zinunue dawa, Wazabuni wengi hawana uwezo wa kutoa huduma kama ilivyo kusudiwa na wakati mwingine huuza dawa kwa bei ya juu jambo ambalo husababisha gharama kwa hospitali za serikali.
Mapendekezo:Namna ya kuboresha huduma/utendaji katika Taasisi za Umma
1.Serikali ifanye tathmini na kuangalia uwezo wake wa kusimamia na kukamilisha ujenzi wa miradi mbalimbali, ili kuepusha kuchukua fedha kutoka katika mashirika mengine yanayotoa huduma kwa wananchi.
2. Serikali ijitathimini kifedha kabla ya kuanza kwa miradi mikubwa ya maendeleo,kununua ndege,matengenezo, biashara,soko,abiria, athari za mazingira,ili kupunguza gharama za uendeshaji na hasara zinazoepukika, ikiwemo faini,vifo, huduma duni.
3. Kupeleka fedha zilizotengwa zote kama zilivyotengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha husika katika kila idara,zimamoto,polisi, hospitali,shuleni Kwa wakati
4. Kuboresha Mazingira ya kazi, ofisi za serikali, nyumba za watumishi,hasa wa serikali za mitaa,matizo kama ,makato, ofisi mbovu, malimbikizo ya mishahara, ukosefu wa umeme na maji, mishahara midogo husababisha kupunguza ubunifu na ubora wa kazi.
5. Kupunguza vitisho kwa tumishi na badala yake ijikite katika kuwaelimisha namna sahihi ya kufanya kazi kulingana na miongozo iliyowekwa.
6. Serikali kufanyia kazi mapendekezo ya wataalamu kama ofisi ya mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa fedha za serikali (CAG) ili kuepuka kuendelea na makosa ya kiutendaji.
Mwisho.
Serikali ichukue hatua stahiki na Kuwajibishwa wanaofanya ubadhirifu ikithibitika badala ya kuwahamisha na kusimamisha tu,hii itasaidia kuleta nidhamu na kupunguza uzembe kazini.

Upvote
9