'Huduma Pamoja' kupitia Shirika la Posta inalenga nini?

'Huduma Pamoja' kupitia Shirika la Posta inalenga nini?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
"Tumefanya mageuzi makubwa ndani ya Shirika la @posta_tz. Lengo ni kuwa na Posta ya Kidijitali, Posta kuwa kitovu cha biashara mtandao na huduma za Pamoja.

Katika kutekeleza azma hii, Siku ya Jumatatu tarehe 6 Spetemba, tutazindua utaratibu wa Huduma Pamoja". Mhe. Faustine Ndugulile

Nimeona posta wamekusanya taasisi za serikali kwenye ofisi zao nikajiuliza hizi taasisi za serikali zinahusikaje na shirika la posta? NIDA imeshindwa kutoa vitambulisho unaipeleka posta ikafanye nn? Uhamiaji na magwanda wanaenda kufanya nn posta? Tra wanafanya nn posta? Ni utafiti gani ulionyesha nida ameshindwa kutoa vitambulisho kwa sababu anakosa one stop center? Possport zinahitaji one stop center? Link Kati ya nida card na passport na huduma za posta ipo wapi?

Nilichokigundua Ni kwamba zipo fedha za wahisani zimeletwa watu wametafuta njia ya kuzipiga wakaona wakusanye taasisi za uma sehemu moja kuwaridhisha wahisani kwamba Kuna mradi unaendelea.

Hakuna namna unaweza kunishawishi kwamba upo ufanisi katika dili hili la wakubwa....hapa fedha za wahisani zimepigwa. Mabilioni yakutengeneza one stop center kwenye ofisi za posta yangeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuboreaha miundombinu ya taasisi Kama ttcl na kukuza mtaji wa benk. Leo hakuna watu wanatuma parcel posta wanatumia DHL ambayo imejitosheleza, wanatumia mabus kwa percel za ndani, watu wanalipa kwa mtandao, ....posta posta posta mmekula pesa za wahisani au Kama Ni pesa za ndani Basi temeni ndoano
 
Mleta uzi nakuunga mkono. Labda wafafanue lengo lao la kufanya wanayofanya (kukusanya taasisi za serikali na mengineyo wayafanyayo yatasaidia vipi kuliokoa shirika).

Miaka mingi mashirika ya umma yanakuwa mzigo tu, ushindani hawawezi, na hata wakibebwa wanadondoka.

Ijapokuwa kufafanua kila kitu huenda si vyema sababu ya 'siri za kibiashara' kuibwa na mshindani lakin wangefanya la maana kutuambia wanajipanga vipi kulitwaa soko lao lililopotea na njia zipi wanakuja nazo kubuni huduma zingine au kushindana na washindani wao.

Lasivyo ndo yale yale - kama juzi na jana na kama leo. Utawaambia nini mabosi ambao hata shirika likiwa hoi bin taabani mafweza yao na kazi zao zipo palepale?
 
Nilipouona huu uzi ukiungumzia ufisadi posta nimegoogle kuona maana ya one stop center ya posta. Nakubaliana na mtoa hoja kwamba hizi fedha zingeelekezwa sehemu nyingine kuliko kuendelea kutumbua fedha za wahisani au za umma kwa mambo ya kijinga. Ntatoa mfano wa project zinazoendelea.

1. RITA Wana kampeni ya 5 years ambayo inalenga kutoa vyeti kwa watoto wasio na vyeti. Kupitia kampeni hii maafisa wanazunguka mtaani kuandikisha, lakini pia mahospitalini wameweka utaratibu wa kutoa vyeti. Kampeni hii imefanya vizuri kwa sababu imeenda kwenye kiini cha tatizo. Leo nani anaweza kutuaminisha kwamba watu walioshika kwenda ofisi za rita za mikoa na wilaya wataenda kupanga foleni posta? Lakini pia vifo na ndoa, taratibu za usajili na utoaji wa vyeti zinahitaji mtu aende one shop center? Let us be serious na miradi tunayofanya

2. NIDA amekwama kutoa vitambulisho, ofisi zao zinafanya vizuri kwenye usajili wa watu....leo tunataka kuwadanganya wananchi kwamba printing unit itapelekwa POSTA? Ni huduma gani tunaamini imeshindwa kutolewa na NIDA Hadi tuone wanapaswa kwenda posta? Kwanini tunawaza kuwakusanya watu kwenye mrundikano wa ofisi?

3. Uhamiaji, Hawa watu ukiingia kwenye website zao unaona kabisa mchakato wote unaufanya online isipokuwa vidole unaenda ofisini kwao. Na zilipo ofisi za Uhamiaji mfano Kagera si mbali na posta...je tunataka kuwaaminisha watu kwamba suala la Uhamiaji litafanyikia posta? Ofisi zao zimezidiwa? Ila pia tunataka kusema passport zote zitaprintintiwa palipo na ofisi za Uhamiaji? Uhamiaji wanaenda kufanya Nini posta?

4. Msingi wa kuanzishwa kwa Shirika la Posta.....naamini ukisoma kusudio la kuanzishwa kwa Shirika la Posta utabaini Hawa watu wameondoka kwenye core functions za taasisi wamekwenda kuvamia taasisi nyingine za serikali. Ukiona shirika limeshindwa kujiendesha kwa shughuli zake mama likakimbia kuchukua shuguli za taasisi nyingine Ni tafsiri ya shirika kufa. Posta ilipaswa kujikita kushindana na DHL lakini posta wanawatumia DHL kwa kuwalipa wafanye shughuli za kusafirisha mizigo.

Nimeona sehemu wanasema wamepata fedh za wahisani, naamini hizi fedha zinapigwa kwa sababu Kwanza, hakuna ofisi ya posta nje ya Makao makuu ya wilaya na Mikoa ambayo Yana ofisi zote za serikali. Wananchi watajigawaje? Au ofisi nyingine zitafungwa wafanyakazi wa hizo taasisi wahamishiwe posta?

Huu ni wizi wa wazi
 
Niliona kipeperushi chao hapa siku ya uzinduzi wameshindwa hata kuonyesha nini wanafanya na nini faida ya hicho wanachokifanya.

Shirika bado ni traditional saaana wanafikiri kwa kurudi nyuma.
 
Back
Top Bottom