Huduma ya choo kwenye mabasi ni changamoto

Huduma ya choo kwenye mabasi ni changamoto

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Nimesafiri na mabasi kampuni kadhaa ambazo sitazitaja Kwa majina ili kutochafua biashara zao

Nimejihakikishia kwamba Kwa Hapa nyumbani ustaarabu wa kutumia vyoo ndani basi gari likiwa safarini Bado hatuwezi tukubali tu

Ni heri ukasafiri na bus lisilo na choo ndani kuliko kulipa pesa nyingi ya nauli ukiltegemea huduma ya choo ambayo itakukera tu

1. Vyoo vyenyewe ni Kwa ajili ya haja ndogo tu
Mabasi yote nilisafiri nayo yote yanahidhi haja ndogo tu

2. Kifaa cha kukinga mkojo kinajaa haraka
Hiki kifaa wakiingia watu watu kimejaa na kitahitaji kumwaga
Utashangaa ukitoka Mwanza kufika tu Shinyanga wanamwaga haja ndogo

3. Milango ni midogo na hewa hamna.
Yaani kama una kilo kuanzia 90 kale kamlango hupiti au upite kiubavu Kwa taabu

4. Hakuna faragha uwapo chooni
Vyoo havijatengwa Kwa jinsia yaani basi Lina choo kimoja tu
Kwa maana jinsia zote mnatumia choo kimoja pamoja na watoto hapo hamna faragha

5. Air freshener zinatoa harufu kali.
Ukitaka uugue mafua yasiyo pona jaribu kutumia vile vyoo
Ukiingia Kuna harufu kali wanapuliza inashika nguo ukifika watu wanakuuliza umejipaka pafyumu Gani,
Kumbe ni air freshener za choo cha basi

6.usafi hamna
Kufanya usafi hamna au wanafanya lakini wanashidwa
Choo ni cha mkojo ila Kwa watu kutojua unakuta mtu kaweka haja kubwa
 
We unataka uchafue gari hali ya hewa.
Kuna watu humu duniani wameoza sema wanaishi tu.
Siku moja niliingia choo cha kulipia alikuwa ametoka mtu kujisaidia aja kubwa,hewa iliyokuwemo mule hata nzi na mende ilibidi watoke wanipishe kama nitaweza kuvumilia ule uwozo
 
We unataka uchafue gari hali ya hewa.
Kuna watu humu duniani wameoza sema wanaishi tu.
Siku moja niliingia choo cha kulipia alikuwa ametoka mtu kijisaidia aja kibwa hewa iliyokuwemo mule hata nzi na mende ilibidi watoke wanipishe kama nitaweza kuvumilia ule uwozo
Nimecheka mno
 
We unataka uchafue gari hali ya hewa.
Kuna watu humu duniani wameoza sema wanaishi tu.
Siku moja niliingia choo cha kulipia alikuwa ametoka mtu kijisaidia aja kibwa hewa iliyokuwemo mule hata nzi na mende ilibidi watoke wanipishe kama nitaweza kuvumilia ule uwozo
Ana hoja. Air freshener ziko nzuri ambazo hazina harufu kali. Infact ni watu wengi sana wanaathirika na harufu kali za perfume kwa kuumwa kichwa na kichefuchefu. Pengine hiyo sehmu ya vyoo viwe na jinsia ndiyo amekosea. Kwenye safari hata ndege vyoo vyote vinatumika na jinsia zote. Usafi nao ni muhimu. Anyways magari ya mchina always yana ''ladha'' zake.
 
Vyoo ndani ya mabasi vimewekwa kwa matumizi ya dharura TU kwa haja ndogo hasa kwa wagonjwa na wazee au watoto. Sasa watu woote mnataka mjisaidie garini wakati mngeweza kujisaidia kabla ya kuanza safari pale stendi na sehemu za kupumzika na kula. Utakuta mtu kwa sababu kaambiwa kuna choo, basi atakunywa njia nzima! hata basi likisimama kula haendi chooni kisa kuna choo kwenye basi. tuelimishane juu ya hili.
 
Me naona vyoo vya kwenye mabus ni ile dharura tu ya ghafla kuna siku nasafiri hadi mwsho wa safari hmn aliekitumia hata mtu mmoja
 
Me naona vyoo vya kwenye mabus ni ile dharura tu ya ghafla kuna siku nasafiri hadi mwsho wa safari hmn aliekitumia hata mtu mmoja
Ukisafiri safari za usiku huwa vinatumika mno
 
Taifa linaloongoza kwa ulalamishi. TANZANIA! zamani mlikua mnasafiri na mabasi yenye vyoo ndani au kuna mijitu ina laana tu kutwa kulalama. Si uondoke na private
 
Back
Top Bottom