DOKEZO Huduma ya Kujifungua imekuwa gharama sana katika Hospitali ya Wilaya Ubungo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

kijazi07

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2016
Posts
1,036
Reaction score
2,240
Kiukweli ni hospitali nzuri tu, wanatoa huduma nzuri, ila changamoto ni gharama za kujifungua zipo juu.

Miaka miwili iliyopita, kujifungua kwa kawaida ilikuwa unachangia elfu hamsini, na kwa upasuaji laki na nusu. Haikujalisha umekuja na vitu vyako, ilikuwa ni lazima uchangie hivyo.

Ila kwa sasa, kujifungua kwa upasuaji imefika mpaka laki mbili na nusu, na kujifungua kwa kawaida elfu themanini.

Tunaomba mtusaidie, gharama ni kubwa na maisha ni magumu.
 
Mkuu mtoto haji kwa bahati mbaya, umepewa miezi 9 ya kujipanga
Nguo
Beseni
Pampers
Mafuta
Pesa ya Hospital
Budget ya chakula ya mama

Yani una miezi 9 ya kutafuta hivo vitu, kama miezi 9 haikutosha kutafuta pesa ya kulipia hospital basi wewe huna “PLAN” na maisha yako
 
Kiukweli ni hospitali nzuri tu, wanatoa huduma nzuri, ila changamoto ni gharama za kujifungua zipo juu.

Miaka miwili iliyopita, kujifungua kwa kawaida ilikuwa unachangia elfu hamsini, na kwa upasuaji laki na nusu. Haikujalisha umekuja na vitu vyako, ilikuwa ni lazima uchangie hivyo.

Ila kwa sasa, kujifungua kwa upasuaji imefika mpaka laki mbili na nusu, na kujifungua kwa kawaida elfu themanini.

Tunaomba mtusaidie, gharama ni kubwa na maisha ni magumu.
Gentleman,
kwenye sehemu ya bandiko lako hase kwenye ubora wa huduma katika hospitali ya wilaya ya ubungo, nakubaliana na wewe 100%

Jamaa wamejipanga vizuri sana na kwakweli huduma zaidi ni nzuri sana na bora kabisa zenye viwango vya kimataifa. Hongera sawa waganga, wauguzi na wafanya kazi wote katika hospital ya wilaya ya ubungo.
Mnafanya kazi nzuri, kubwa na ya kutukuka sana.

Gentleman,
kwenye suala la gharama naomba kutofautiana na wew kidogo.
Binafsi naona gharama za huduma za uzazi hospital ya wilaya ya ubungo ni sahihi kabisa ukilinganisha na ubora wa huduma muhusika anayoipata.

hata hivyo,
ikiwa mwenza wako ni mjamzito, ni vizuri kujipanga vizuri sana financially whether ata jifungua salama au kwa changamoto.
Si salama na sio sahihi kabisa, mwanaume anaesubiria mke wake kujifungua, kua na maandalizi ya chini ya 1m kwa kijijini na walau 2m mjini. Ikiwa pungufu sana walau uwe na laki5 mfukoni kwaajili ya tahadhari.

Na inawezekana kabisa kujipanga pole pole tangu mwanzo wa ujauzito wa mkeo. Na ukimkatia bima itapendeza zaidi.
Na hayo ni maoni tu na sio agizo au amri.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Kata Bima
Nje ya hapo tegemea lolote.
Ukishindwa Ile ya NHiF
Kata Ile ya 50k ya CHIF.
Unaiifungua bila kelele,
 
Kikawaida ukishagundua mkeo ni mjamzito.
Pamoja na kuwa utakuwa unakusanya pesa za emergency na uzazi.
Ni vizuri kabisa uwe na BIMA inasaidia sana

Mtoto wangu wa tatu mimba yake ilikuwa na mambo mengi. Kwenda Mloganzila kule Kila mara. Gharama zinakuwa juu. Hiya milioni moja inakatika kama utani tuu.
Ila ukiwa na Bima angalau baadhi ya gharama zinapungua
 
nakukubaliana na wewe 100% gentleman 👊
 
Laki 2 upasuaji unalalamika mkuu? Kama kukitokea dharura ukaingia private si utakua kichaa? Kina baba tujiandae kwa lolote pale wake zetu wanapopata ujauzito chochote kinaweza tokea
Hapo mkuu unatizama kwa mtazamo wa kipato chako, lakin sio watanzania walio wengi, wengi hiyo laki 2 ni kipengele kikubwa mkuu
 
Watu hamjamuelewa mleta mada
Serikali wanadanganya wananchi kua huduma ya kujifungua, mama na mtoto ni bure kitu ambacho SIO KWELI
Bora waweke kila kitu wazi kua huduma sio bure ijulikane moja!

Kwanini ionekane bure wakati wazazi wanalipishwa?
 
Laki tatu operation sio gharama, make wangu alijifungua Kwa operation kairuki nililipa 2.7.

Kuwa mpole mshukuru Mungu kama mama na mtoto wapo salama
 
Hapo mkuu unatizama kwa mtazamo wa kipato chako, lakin sio watanzania walio wengi, wengi hiyo laki 2 ni kipengele kikubwa mkuu
Hapana bro sijatazama kipato binafsi maana nami najitafuta ila ishu ya ujauzito ipo complicated anaweza kuambiwa akapumzike chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari mimba ikiwa ndio kwanza miezi mitatu itakuaje
 
Kiukweli ni hospitali nzuri tu, wanatoa huduma nzuri, ila changamoto ni gharama za kujifungua zipo juu.

Miaka miwili iliyopita, kujifungua kwa kawaida ilikuwa unachangia elfu hamsini, na kwa upasuaji laki na nusu. Haikujalisha umekuja na vitu vyako, ilikuwa ni lazima uchangie hivyo.

Ila kwa sasa, kujifungua kwa upasuaji imefika mpaka laki mbili na nusu, na kujifungua kwa kawaida elfu themanini.

Tunaomba mtusaidie, gharama ni kubwa na maisha ni magumu.
Mimba sio ugonjwa wala emergency.

Kama unashindwa kutunza hicho kiasi kwa muda wa miezi yote hiyo ya ujauzito mpaka tarehe za makadirio ya kujifungua ni heri uachane na suala la kubeba ujauzito .
 
Mimba miezi 9 mlishindwa kufanya uchunguzi mdogo mjue gharama za hospitali husika
Kuna baadhi ya hospitali buree kujifungua utaambiwa upeleke vifaa napo pia utalalamika
 
Matibabu kwa sasa sio kazi ya serikali ni jukumu la mwananchi, so mnapopata mimba kitu cha kwanza ni kujipanga namna mtakavyokabiliana na changamoto za uzazi. Kuna bima lakini kuna kudunduliza.

Bora hata wewe huenda mimba haikuwa na complications zozote. Maana kuna watu kuanzia kutafuta mimba hadi kulea kichanga ni sheeda!!
 
Back
Top Bottom